Naomba kujua walipo waimbaji wa kwaya ya Ulyankulu Bara barabara ya 13

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,851
15,259
Hii kwaya Ilivumaga sana miaka ya 90 huko, Nyimbo zao maarufu ni pamoja na
Samson na Delilah, Katika viumbe vyote Ayoub.

Hii kwaya ilijipatiaga umaarufu sana enzi hizo, naomba kujua kama hawa waimbaji bado wote wapo hai? Na wengine wapo wap leo hii?

Asante
 
Hii kwaya ni kiboko. Album yangu ya nyimbo za dini za muda wote ni " Katika Viumbe Vyote".

Na kuna wimbo wao mmoja unaitwa " Bwana Alizaliwa" Nimejaribu kuutafuta siupati ninaupenda sana.

Pia nasikia wale waimbaji wengi walikua ni wakimbizi toka Burundi walisharudi huko kwao.
Ooh no, hope sahiv watakuwa wazee jamani 😭😭, niliwapenda sana, na nyimbo zao ni bomba mbaya
 
Hivi hiyo Album imetoka mwaka gani.?
Kinachofanya nizipende hizi nyimbo Mama alikua anapenda sana kuimba akiwa anatuogesha au akitwanga muhogo huo wimbo wa viumbe vyote. Kwaya nyingine ni ile ya kasulu waliimba Mke mwema..sijui wako wapi. Na wale wa Tabata waliimba sipati picha sijui walipotea wapi
Screenshot (46).png
 
Back
Top Bottom