Naomba kujua vyanzo vya mapato vya Lowassa!

Naomba kujua vyanzo vya mapato vya Lowassa!

Wadau naombeni kujua vyanzo vya mapato vya huyu brother, Me nilisikia ni mfugaji mzuri tu.Ya Richmond tatizo lilikua ni uwaziri mkuu.Tusimshutumu tuu kua anagawa rushwa wakati pengine tunajua biashara zake na hua anasaidia wenye shida na si kugawa rushwa. Tatizo lake nini? kaiba wapi? lini alitangaza kugombea uraisi?Alisema aliyepata kapata jamani.

nani kakwambia yupo humu muulize yeye
 
ukishafahamu itakusaidia nini

Yaani waTZ bwana! huo ndo mwisho wa upeo wa fikra zako.Tulishasema anapigiwa kelele kila kona kua anagawa sana rushwa, mara fisadi, hapa sisi tunataka kujua ni tajiri kiasi gani mpaka hata ndani ya chama chake wanamshambulia sana. Sijawahi kumsikia takukuru wala hata mahakamani sababu ya rushwa.Au ni ile nia ya kuutaka ukuu wa kaya japo sijawahi sikia wazi kua anatangaza hiyo nia yeye binafsi.
 
Nachojua mie Edo ni mmiliki wa Zara Tours ya Arusha pia Ngurdoto hotel,Mashamba mengi,majengo mengi.....
 
Vipasua anga vyote vinavyoota kama uyoga maeneno mbalimbali ya jiji na hasa Upanga, na vinavyomilikiwa na wenzetu wenye asili ya kiasia...kila mjengo jamaa ana asilimia 10%.Pesa kukauka rahisi.
 
Kipindi cha mwalimu ndo waliona kuna umuhimu wa kuulizana vyanzo vya mapato lakini sasa ni wewe tu na spidi yako, kidoogo mzee Warioba airudishe ile hali kwa kuweka UWAZI kuwa tunu ya taifa lakini waelewa wamekipiga chini kipengele hicho ili mambo yaendelee freestyle
 
Nilisikia Lowasa ni kiongozi wa wamasai wote africa mashariki,yaani mpaka kenya ye ndo kiongozi mkuu wa wamasai na huwa wanamzawadia ng'ombe,imagine wamasai wangapi matajiri,wengine wanafuga mpaka ng'ombe zaidi ya 5000,kama watu 10 wakimpa tu ng'ombe 1000 ni hela ndefu
 
Hakika tatizo la ajira nchi hii ni kubwa mno;watu hawana kazi wameamua kuwa wambeaaaa!

Well,keep on discussing Lowassa if at all that turns out to be an occupation;Go ahead and get lost if that at all earns you a slice of bread
 
Ni rahisi kuona wapi watu hawa wanapata utajiri wao:

1.) Mengi - IPP Media
2.) Bakhressa - Azam Enterprises
3.) Dewji - Mohammed Enterprises
4.) Lowassa - Mimi sijui... Naomba kufah
amishwa.
 
Acha kuchunguza mambo ya watu . Na kama una wasiwasi nenda TAKUKURU. Au huna jambo la kufanya, usijaze sever zetu kwa hoja zisizo na msingi. Watanzania huwa siku zote badala ya kuchapa kazi mnaendekeza umbea.
 
Lowassa atawanyima hata kwenda choo mwaka huu!
 
Acha kuchunguza mambo ya watu . Na kama una wasiwasi nenda TAKUKURU. Au huna jambo la kufanya, usijaze sever zetu kwa hoja zisizo na msingi. Watanzania huwa siku zote badala ya kuchapa kazi mnaendekeza umbea.
Mbona yeye anataka kuongoza nchi ya watu?!
 
Back
Top Bottom