Naomba kujua tiba mbadala ya mgongo

Joyce Gaitan

Member
Dec 29, 2017
45
52
Habarini za majukumu ndugu zangu.

Nasumbuliwa sana na mgongo, niliwahi piga X-ray na imeonyesha pingili hazina mpishano mzuri kutokana na ukaaji chini muda mrefu. Dr alinishauri niwe navaa mkanda kwajili ya kunyoosha pingili lakini naona hali bado sio shwari.

Nilijaribu kwenda kwa wale madokta wanaounga mifupa kwa vijiti, wakanambia wananyoosha pingili kwa gharama ya laki 5 (500,000) naomba msada wenu kwa yeyote anayefahamu tiba mbadala ya hiyo anifahamishe kwakuwa sina pesa hiyo ya kwenda kunyooshwa.
Asanteni
 
Asante ndugu,,,nitafanya hivyo.
Je ni kwa siku ngapi?

Sina uhakika na idadi sahihi ya siku, hii tuliwahi kushauriwa na mtaalamu mmoja wa afya, anasema kwa sababu ya muda mwingi kuinamia computer, mgongo inabidi uunyoshe kwa kulala kwenye mkeka walau mara kadhaa kwa wiki.

Mimi huwa nafanya hata mara 2 kwa wiki au 3.
 
Asante sana..nitafanya hivyo.
 
Habarini za majukumu ndugu zangu.

Nasumbuliwa sana na mgongo, niliwahi piga X-ray na imeonyesha pingili hazina mpishano mzuri kutokana na ukaaji chini muda mrefu. Dr alinishauri niwe navaa mkanda kwajili ya kunyoosha pingili lakini naona hali bado sio shwari.

Nilijaribu kwenda kwa wale madokta wanaounga mifupa kwa vijiti, wakanambia wananyoosha pingili kwa gharama ya laki 5 (500,000) naomba msada wenu kwa yeyote anayefahamu tiba mbadala ya hiyo anifahamishe kwakuwa sina pesa hiyo ya kwenda kunyooshwa.
Asanteni
 
Jaribu tiba za Kichina, kwa tiba za asili wale ninawaamini.
Una uhakika unacho kisema dada? unajuwa Wachina wanazo dawa za artificial herbs? Sio dawa organic Herbs. Dawa zao hazitibu maradhi yoyote yale ni dawa za biashara tu.Haya maneno aliwahi kusema Mwalimu wangu wa Tiba Marehemu Doctor Sebi kuwa wachina dawa zao ni nyingi dawa feki .
 
Unafanya kazi gani Mkuu?
Je ulishawahi kubadili mazingira ?
Je unaishi maisha ya stress?
Chakula unakulaje ?
 
Back
Top Bottom