Nina tatizo la pingili za uti wa mgongo kubanana. Naomba kujua tiba

chipelele

Member
Apr 5, 2020
8
45
Habari wapendwa,

Nasumbuliwa na maumivu ya kiuno na mgongo nilipima Dtk. kaniambiwa pingili za uti wa mgongo zimebanana chaajabu nimeanza kutibiwa tangu January hadi Leo nakunywa dawa kila siku bado maumivu yapo hasa wakati wa kukaa pingili ya chini kwenye mkia makalioni.

Tafadhali kama kuna mtu aliwahi pitia hii shida naomba msaada wa matibabu au kama kuna dawa nzuri nikanunue maana nahudhuria klinik kila mwezi hadi kuna mda nakata tamaa.

Msaada tafadhali
 

Steph JK

Member
Sep 14, 2018
74
125
Nina tatizo Kama hilo Ila Mimi sikuwahi Pima nikiuno kilikuwa kinasumbua na performance kwa bed ilianza kupungua, nikaelekezwa kwa mtaalamu wa dawa asili ambaye alinifanyua massage ya mgongo baada ya kumaliza akaniambia pingili mbili zilianza kuchomoka na akazirudisha akanipa na majani kwa ajili ya kukanda na nilipona.

Aidha kabla ya hapo niliona dalili ambazo nilienda hospital wakanipa madawa bila mafanikio yoyote. Mtaalamu huyo nilimlipa sh. 10,000 tu Ila baada ya wiki mbili nilirudi Tena kwa ajili ya check up nilimlipa Tena sh. 10,000 yupo Korogwe eneo la msambiazi.
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Dawa za kutibu hakuna
Tiba ni
Dawa za kumeza
Dawa za kuchua
Kuoga maji ya moto si uvuguvugu
Mazoezi ya mgongo
Massage ya mgongo na miguu tokea pajan hadi kwenye vidole
Acha kazi za kuinama
Punguza kutembea muda mrefu
Acha mazoezi ya jumla kwa sasa pia kukimbia
Kaa posture nzuri ambayo mgongo unasimama
Kalia viti ambavyo haviumizi makalio yaan viwe na sponji nzuri
Tafuta msaada wa shughuli za nyumban
Mwisho lala bila mto na chali muda mrefu


Ukiyafanya haya utaishi vizuri kwan shida halisi si disk bali ni misuli ya uti wa mgongo imebana kutokana na aina yako ya
Mgongo ambao unaweza kuwa umenyoooka kwan 40% ya watu dunian wako hivyo

Najua kwakuwa niliteseka mwaka mzima ila siku nilipogundua hayo nikaishi nikaishi vizur bila maumivu na yakitokea najua nimefanya niliyokataza hapo juu

Kwa ushaur na matibabu nenda moi ukawaone wadaktari bingwa wa mgongo pia ufanye Mri uuone mgongo wako vizur
 

jamesjaco

Member
Jul 27, 2014
35
95
Tatzo lako ni vigumu kupona kabisa kwa dawa za hospitali au kienyeji kwani km pingili zimebanwa au kuhama lazma zirudishwe mahali pake ndio zitakaa sawa la sivyo utaendelea kunywa dawa na tatzo litakua sugu.. kwa ushauri Waone physiotherapist(dr wa mazoezi na viungo)! Km upo Dar unaweza nitafuta nikuelekeze clinic niliyopo kwa ajili ya checkup
 

Pan AM

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
214
250
Pole sana, ndugu yangu wa karibu alikuwa na tatizo linalofanana na hilo,yeye pingili ilitoka katika mpangilo na kukaa pembeni
alihangaika hospiatri zote,akafankiwa kupata ufadhili na kwenda India ndipo alipoponea..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom