Naomba kuelemishwa kuhusu kutoa hela kwa Check

mwalidebe

JF-Expert Member
Mar 27, 2016
424
247
Ndugu zangu Mimi ni mgeni kwenye mambo ya kibenki kuna rafiki yangu nafanya naye biashara na ilitakiwa mwezi ulioisha anipe milioni nne ila toka tarehe 28 hadi Leo ananiambia kuwa cheki inasumbua,anasema yeye cheki amechukua CRDB Benki na ameipeleka NBC kwa amefuatilia wanamsumbua wakampa siku tatu amefuatlia bado hajafanikiwa.

Anasema kuwa cheki kutoka benki tofauti huwa zinasumbua,anasema kama ingekuwa ni CRDB kwa CRDB Ingechukua muda mfupi sana. Sasa ndugu zangu naomba uelewa Wa hii mambo ya Cheki,inakuwaje ikojeikoje na je jamaa yangu ni mkweli au ni lugha ya kunipoteza kwenye lengo.
 
crdb kwa crdb ni hapo hapo unachukua hela ila kwenda bank nyingine zaman ilikuwa n 7days ila sas hivi ni 24 hrs mzigo tayar ....USHATAPELIWA....
 
Ni kweli kabisa anaweza kuwa anakupoteza. Tangu tarehe 28/02 mzigo ungekuwa umeshaingia. Anaposema hundi amechukua CRDB anamaanisha nini? Yeye ndo amelipwa kwa hundi ya CRDB au wewe ndo amekuandikia hundi ya CRDB? Na kama wewe ndo anakulipa kwa hundi kwa nini hakukupatia wewe mwenyewe hiyo hundi uende uingize mwenyewe kwenye akaunti yako? Hapo mkuu kuna kila dalili za kulizwa!!
 
Anakudanganya ,kama anakulipa kwa cheque,mwambie akupe hiyo cheque ili ukachukuwe hela;
 
crdb kwa crdb ni hapo hapo unachukua hela ila kwenda bank nyingine zaman ilikuwa n 7days ila sas hivi ni 24 hrs mzigo tayar ....USHATAPELIWA....
Asante kwa kunielimisha maana mpaka sasa anasema bado hajachukua hela.
 
Pole sana aisee.... Sisi watanzania sijui wakoje aisee. Mimi nimefanya biashara na rafiki yangu nimemwamini nikatoa mtaji alafu yeye asimame kwenye utendaji kwa maana ya uzoefu anao. Daaah jamaa biashara imekaa vizuri kalala mbele na Pesa zote.

Nimekuja huku nika kutana na mkuu anaomba tumuungishe kwenye biashara yake ya kuagiza vitu nje ya nchi nikaamua nimuungishe nikamtumia Pesa aninunulie mashine Fulani Daah kalala mbele na Pesa yangu yote (Kelvin Isaya).

Kelvin Isaya popote ulipo.... Kama kweli mdomo unaumba naomba ulaaniwe wewe na Uzao wako wote... Huto ishi maisha ya Amani na furaha kwa Pesa ya Kutapeli.
 
Hakuna cha cheque wala nn hapo. Mweke ndani tu huyo.Wamekubashite tayari
 
Back
Top Bottom