Naomba kazi, nina shahada ya Uuguzi napatikana Mbezi Beach

Doreen27

Member
May 9, 2021
8
75
Habari wanajamii?

Mimi ni S jinsia Ke, umri miaka 28, elimu yangu ni shahada ya Uuguzi bado sijapata leseni ila nategemea kuipata mwezi wa 7 mwaka huu,

Naomba kazi yoyote kwa sasa inayoweza kuniingizia kipato muda huo nikisubiria leseni na ajira, Nina uzoefu huu;

1) Naweza kukutafutia research title pia kuandaa na kuandika Concept note kwa ajiri ya reserch proposal kwa upande wa afya.

2) Naweza kuandaa na kuandika research proposals.

3) Naweza kufanya data analysis kwa kutumia SPSs na kuandaa research report za kwa fani za Uuguzi.

4) Naweza kufanya kazi kwenye clinic za mama na mtoto kama mkunga na muuguzi.

5) Niko mahiri kwenye kazi/shughuli zote za uuguzi mahospitalini na kwenye vituo vya afya, nina uzoefu wa ICU, Emergence department, nina uzoefu wa kazi za medical ,surgical/orthopedic, pediatric, maternity, Labour ward, Dialysis, RCH clinic, MOT, na Psychiatry.

6) Naweza kufanya kazi kwenye maduka ya huduma za fedha kama vile airtel money, M-pesa n.k

7) Naweza kusimamia biashara au kazi na ikaenda vizuri kwa uaminifu mkubwa sana.

8) Naweza kutoa home based care za kiuguzi, na naweza kuwa muuguzi wa familia.

9) Naweza kutoa palliative care.

10) Naweza kufanya kazi ya sales representative kwa bidhaa za kampuni za dawa.

11) Naweza kufanya kazi ya kuuza duka la; vifaa vya umeme, vyombo, nguo, vifaa vya ujenzi, funitures n.k

12) Naweza kufanya kazi za stationery na nina uzoefu mzuri wa kutumia komputa.

14) Ninaweza kufundisha masomo ya Chemistry, biology na Geography kwa umahiri mkubwa.

15) Ninao uzoefu wa kutoa uhauri na nasaha kwa watu waliokata tamaa either ya shule/kusoma, maisha na afya kwa ujumla.

16) Naweza pia kuwa business partner kwa mtu mwenye mtaji, Mimi shida nj mtaji.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wewe uliye soma hapa.

Naomba mwenye kazi au connection ya kazi ani pm tafadhari.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,921
2,000
Namba 5 inapingana na namba 11 na 12.
Base sana kwenye mambo ya afya hasa unesi uliosomea.
Niliona Tangazo la K'S Hospital Mbeya jaribu ku-search uombe.
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,255
2,000
Namba 5 inapingana na namba 11 na 12.
Base sana kwenye mambo ya afya hasa unesi uliosomea.
Niliona Tangazo la K'S Hospital Mbeya jaribu ku-search uombe.
Nadhani hapo anajaribu kuelezea ni namna gani alivyokua multipurpose. Kwamba zisipopatikana fursa za professional yake basi anaweza akafanya na mengineyo (11 na 12) ili mradi maisha yaende.

Sioni kama kuwa na sifa za namba 5 kunazuia au kukanganya kuwa na sifa namba 11 na 12.
 
jannelle

JF-Expert Member
Feb 8, 2020
407
1,000

Yes, hasa kwa dunia ya leo tunayojihusisha na ajira za nje ya taaluma zetu, hongera mwaya wengine tupo tu kwa sasa
 
Infoax

Member
Jun 17, 2021
6
45
Doreen, naomba nikushauri. Jiulize unataka utaalamu wako wa UUGUZI uwe vipi baada ya miaka 10 au 15 ijayo? Kwa maneno mengine unataka uwe unajua kila kitu kidogo kidogo, au unataka UBOBEE kwenye kitu gani hasa? Ukishapata jibu, sasa elekeza utafutaji wako wa kazi katika mambo yatakayokujenga kuelekea huko unakotaka kwenda.

Usitumie njaa ya muda mfupi kupoteza lengo la kudumu. Yaani usifanye kazi ilimradi kazi tu. Usipoangalia utapotea. Wazo langu ni kuwa tafuta hata hospitali za kujitolea kwa masaa BURE KABISA ili mradi unajenga ujuzi wako katika kile unachokitaka. Kwa mfano, unaenda hospitali fultani hivi kisha unaomba japo kwa muda wa masaa 4 tu kwa WIKI ufanye kazi pale.

Na unawaambia utafanya bure kabisa. Ila omba ufanye kazi chini ya SPECIALIST wa hiyo fani unayoitaka. Faida utakazopata ni nyingi. Kwanza, hao jamaa wanaweza kukuajiri wao wenyewe kama nafasi ikitokea na wakiridhika na wewe. Pili, SPECIALISTS wengi wanafanya kazi hospitali zaidi ya moja, akiona kazi yako nzuri anaweza kukuunganishia nafasi hata hospitali nyingine. Tatu, unajenga wasifu mzuri wa kikazi.

Hata siku yoyote utakapoomba kazi mahali unaweza kutumia jina la hiyo hospitali na huyo Specialist kama reference yako. Hilo ni jambo kubwa sana. Na hapo hakutakuwa na suala la ulifanya eti masaa 4 tu kwa wiki. Itasomeka miaka 2 au 3! Nne, ujuzi wako utakua na utaongeza kitu katika kile ulichosomea.

Tatizo la wengi hawataki kujitolea. Wanataka walipwe tu. Natumaini wewe ni tofauti maana unajua fika ni wahitimu wangapi wako mitaani bila kazi. Sasa yale masaa mengine yaliyobaki katika wiki yatumie kufanya hayo mambo mengine unayoyajua ili kujiongezea kipato.

Na wakati huo huo endelea kurusha maombi ya kazi sehemu mbali mbali. Huenda ukapata kazi mara moja.

Barikiwa.
 
Doreen27

Member
May 9, 2021
8
75
Doreen, naomba nikushauri. Jiulize unataka utaalamu wako wa UUGUZI uwe vipi baada ya miaka 10 au 15 ijayo? Kwa maneno mengine unataka uwe unajua kila kitu kidogo kidogo, au unataka UBOBEE kwenye kitu gani hasa? Ukishapata jibu, sasa elekeza utafutaji wako wa kazi katika mambo yatakayokujenga kuelekea huko unakotaka kwenda...
Watu mnadhani kujitolea bure ni sifa, sasa nijitolee bure nitaishije?, try to think outside the box ndugu, mpaka kuja kuomba kazi nje ya fani yangu ni wazi kuwa I need some cash ili niweze kujikimu kwa maisha yangu ya kila siku for the time being.

Kujitolea nitajitolea baada ya kupata kazi ya kunipatia angalau kiasi kidogo nachoweza kujikimu.

But anyway thanks kwa ushauri.
 
Abuu abdurahman

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,179
2,000
Doreen, naomba nikushauri. Jiulize unataka utaalamu wako wa UUGUZI uwe vipi baada ya miaka 10 au 15 ijayo? Kwa maneno mengine unataka uwe unajua kila kitu kidogo kidogo, au unataka UBOBEE kwenye kitu gani hasa? Ukishapata jibu, sasa elekeza utafutaji wako wa kazi katika mambo yatakayokujenga kuelekea huko unakotaka kwenda.

Usitumie njaa ya muda mfupi kupoteza lengo la kudumu. Yaani usifanye kazi ilimradi kazi tu. Usipoangalia utapotea. Wazo langu ni kuwa tafuta hata hospitali za kujitolea kwa masaa BURE KABISA ili mradi unajenga ujuzi wako katika kile unachokitaka. Kwa mfano, unaenda hospitali fultani hivi kisha unaomba japo kwa muda wa masaa 4 tu kwa WIKI ufanye kazi pale.

Na unawaambia utafanya bure kabisa. Ila omba ufanye kazi chini ya SPECIALIST wa hiyo fani unayoitaka. Faida utakazopata ni nyingi. Kwanza, hao jamaa wanaweza kukuajiri wao wenyewe kama nafasi ikitokea na wakiridhika na wewe. Pili, SPECIALISTS wengi wanafanya kazi hospitali zaidi ya moja, akiona kazi yako nzuri anaweza kukuunganishia nafasi hata hospitali nyingine. Tatu, unajenga wasifu mzuri wa kikazi.

Hata siku yoyote utakapoomba kazi mahali unaweza kutumia jina la hiyo hospitali na huyo Specialist kama reference yako. Hilo ni jambo kubwa sana. Na hapo hakutakuwa na suala la ulifanya eti masaa 4 tu kwa wiki. Itasomeka miaka 2 au 3! Nne, ujuzi wako utakua na utaongeza kitu katika kile ulichosomea.

Tatizo la wengi hawataki kujitolea. Wanataka walipwe tu. Natumaini wewe ni tofauti maana unajua fika ni wahitimu wangapi wako mitaani bila kazi. Sasa yale masaa mengine yaliyobaki katika wiki yatumie kufanya hayo mambo mengine unayoyajua ili kujiongezea kipato.

Na wakati huo huo endelea kurusha maombi ya kazi sehemu mbali mbali. Huenda ukapata kazi mara moja.

Barikiwa.
Umeshauri vyema sana, ila!

Maisha Magumu Mzee.. Unakuta Mtu hana uhakika hata wa Mkate wa kula, anakosa hata Mahitaji ya Msingi, kasoma ivo ivo tuu kwa Shida Siku zimalize..
Huyu anaanzaje kujitolea!

KUJITOLEA KUNATAKA UTULIVU WA NAFSI.. NA UTULIVU WA NAFSI UNATAKA UWE NA UHAKIKA WA CHOCHOTE KITU
 
Mkuu, ukitaka kuwa tofauti, ukitaka uwe mahali pa mafanikio lazima ufanye kitu tofauti. Ndiyo maana waliofanikiwa ni wachache. Sio bahati mbaya. Walijinyima mengi
 
Infoax

Member
Jun 17, 2021
6
45
Watu mnadhani kujitolea bure ni sifa, sasa nijitolee bure nitaishije?, try to think outside the box ndugu, mpaka kuja kuomba kazi nje ya fani yangu ni wazi kuwa I need some cash ili niweze kujikimu kwa maisha yangu ya kila siku for the time being.

Kujitolea nitajitolea baada ya kupata kazi ya kunipatia angalau kiasi kidogo nachoweza kujikimu.

But anyway thanks kwa ushauri.
Umesoma vizuri hapo juu? Nimekuambia unaweza kujitolea hata siku 2 tu kwa wiki. Au ukishindwa hata siku moja. Halafu unasema eti tunafikiri kujitolea ni sifa! Hivi wewe ukijafanikiwa mimi niliyekushauri napewa BILIONI ngapi? Huwezi kutofautisha ushauri wenye nia mbaya na nzuri? Huwezi kufa njaa utaishi tu. Ila ambacho hutakipata kirahisi maishani ni mafanikio. Wewe hutaki ushauri siyo?

Okay, sasa ngoja nikushauri sawa sawa na unavyopenda.

Nenda kituo chochote cha daladala. Kila dala dala inayoingia ipigie debe. Utaachiwa sh 50 au 100 na kondakta kwa kila daladala. Kufika jioni utakusanya 3000 au 4000 hivi. Si ndiyo unataka hivyo? BURE GHARAMA!!!
 
Doreen27

Member
May 9, 2021
8
75
Umesoma vizuri hapo juu? Nimekuambia unaweza kujitolea hata siku 2 tu kwa wiki. Au ukishindwa hata siku moja. Halafu unasema eti tunafikiri kujitolea ni sifa! Hivi wewe ukijafanikiwa mimi niliyekushauri napewa BILIONI ngapi? Huwezi kutofautisha ushauri wenye nia mbaya na nzuri? Huwezi kufa njaa utaishi tu. Ila ambacho hutakipata kirahisi maishani ni mafanikio. Wewe hutaki ushauri siyo?

Okay, sasa ngoja nikushauri sawa sawa na unavyopenda.

Nenda kitu chochote cha daladala. Kila dala dala inayoingia ipigie debe. Utaachiwa sh 50 au 100 kwa daladala. Kufika jioni utakusanya 3000 au 4000 hivi. Si ndiyo unataka hivyo? BURE GHARAMA!!!
Umesomeka mkuu
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,349
2,000
Bado sijapata naombeni kazi jamani, Hata kama malipo ni 7,000 kwa siku nafanya tu, msingi nipate mahitaji jamani please naombeni kazi ilimradi tu iwe halali sio lazima iwe niliyosomea kwa sasa,

Nakuahidi hautajuta kufanya kazi na mimi,

Kila la heri kwenye mapambano yako, nina ndoto ya kuanzisha nursing home dar.. na sehemu ya mazoez kwa wazee.. nina imani utanisaidia ushauri mzuri..
 
RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,378
2,000
Habari wanajamii?

Mimi ni S jinsia Ke, umri miaka 28, elimu yangu ni shahada ya Uuguzi bado sijapata leseni ila nategemea kuipata mwezi wa 7 mwaka huu,

Naomba kazi yoyote kwa sasa inayoweza kuniingizia kipato muda huo nikisubiria leseni na ajira, Nina uzoefu huu;

1) Naweza kukutafutia research title pia kuandaa na kuandika Concept note kwa ajiri ya reserch proposal kwa upande wa afya.

2) Naweza kuandaa na kuandika research proposals kwa wanvyuoa wanaofanya research for the awards za Degree kwa gharama nafuu kabisa.

3) Naweza kufanya data analysis kwa kutumia SPSs na kuandaa research report za kwa fani za Uuguzi.

4) Naweza kufanya kazi kwenye clinic za mama na mtoto kama mkunga na muuguzi.

5) Niko mahiri kwenye kazi/shughuli zote za uuguzi mahospitalini na kwenye vituo vya afya, nina uzoefu wa ICU, Emergence department, nina uzoefu wa kazi za medical ,surgical/orthopedic, pediatric, maternity, Labour ward, Dialysis, RCH clinic, MOT, na Psychiatry.

6) Naweza kufanya kazi kwenye maduka ya huduma za fedha kama vile airtel money, M-pesa n.k

7) Naweza kusimamia biashara au kazi na ikaenda vizuri kwa uaminifu mkubwa sana.

8) Naweza kutoa home based care za kiuguzi, na naweza kuwa muuguzi wa familia.

9) Naweza kutoa palliative care.

10) Naweza kufanya kazi ya sales representative kwa bidhaa za kampuni za dawa.

11) Naweza kufanya kazi ya kuuza duka la; vifaa vya umeme, vyombo, nguo, vifaa vya ujenzi, funitures n.k

12) Naweza kufanya kazi za stationery na nina uzoefu mzuri wa kutumia komputa.

14) Ninaweza kufundisha masomo ya Chemistry, biology na Geography kwa umahiri mkubwa.

15) Ninao uzoefu wa kutoa uhauri na nasaha kwa watu waliokata tamaa either ya shule/kusoma, maisha na afya kwa ujumla.

16) Naweza pia kuwa business partner kwa mtu mwenye mtaji, Mimi shida nj mtaji.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wewe uliye soma hapa.

Naomba mwenye kazi au connection ya kazi ani pm tafadhari.
Unapatikana wapi,,, je waweza uza duka la madawa??? Nicheki
 
MissM4C

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,634
2,000
Njooo Simiyu ujitoleee hutakosa ya vocha na unga wakati ukisubiri kupata kazu, anza na zero, mnatanguliza pesa wahitimu wa leo
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,369
2,000
Umeshauri vyema sana, ila!

Maisha Magumu Mzee.. Unakuta Mtu hana uhakika hata wa Mkate wa kula, anakosa hata Mahitaji ya Msingi, kasoma ivo ivo tuu kwa Shida Siku zimalize..
Huyu anaanzaje kujitolea!

KUJITOLEA KUNATAKA UTULIVU WA NAFSI.. NA UTULIVU WA NAFSI UNATAKA UWE NA UHAKIKA WA CHOCHOTE KITU
Kujitolea waacheni wazungu tu ndio wanaliwezaga hili la “Internship” kwa sisi waafrika ni kupumzikiana tu! Mtu anataka ufanye kazi ofisini kwake akupelekeshe kama vile punda wake halafu asikupe kula wala nauli!

Eti unajitolea yani unabembelezea ujuzi wako akupe mkataba,huu ujinga sijawahi kufanya na wala kufikiria kufanya! Mtu una shida na hela ya kujikimu mtu anasema ujitolee upuuzi mtupu!
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,369
2,000
Njooo Simiyu ujitoleee hutakosa ya vocha na unga wakati ukisubiri kupata kazu, anza na zero, mnatanguliza pesa wahitimu wa leo
Utafanya kazi na njaa na kulala nje? Hii habari ya kujitolea mbona mnaichukulia simple sana au sababu bwana wako alikuwa amekupangia chumba na kukulisha free ndio unahisi wanawake wenzio wote wana madanga ya kuwa support?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom