Naomba kazi, nina shahada ya Uuguzi napatikana Mbezi Beach

Utafanya kazi na njaa na kulala nje? Hii habari ya kujitolea mbona mnaichukulia simple sana au sababu bwana wako alikuwa amekupangia chumba na kukulisha free ndio unahisi wanawake wenzio wote wana madanga ya kuwa support?
 
2) Naweza kuandaa na kuandika research proposals kwa wanvyuoa wanaofanya research for the awards za Degree kwa gharama nafuu kabisa

Unajua kama hili la kumwandikia mtu research ni kosa linaloweza kusababisha discontinuation kwa mwanachuo? Matatizo yasifanye tukiuke sheria na misingi ya nchi.

Usirudie tena kumfanyia mwanachuo research haujengi graduate bora bali unabomoa na unapaswa kushtakiwa
 
Pole sana Doreen. Inasikitisha sana kuona muuguzi kama wewe unakosa ajira pamoja na kuwa kuna upungufu mkubwa sana wa Wauguzi nchini. Ni rahisi watu kusema jitolee ufanye BURE wakati hata hiyo nauli ya kwenda na kurudi huko utakajitolea huna. Pesa ya kulipia pango au ya kupata hata mlo mmoja kwa siku huna. Pole sana.

Habari wanajamii?

Mimi ni S jinsia Ke, umri miaka 28, elimu yangu ni shahada ya Uuguzi bado sijapata leseni ila nategemea kuipata mwezi wa 7 mwaka huu,

Naomba kazi yoyote kwa sasa inayoweza kuniingizia kipato muda huo nikisubiria leseni na ajira, Nina uzoefu huu;

1) Naweza kukutafutia research title pia kuandaa na kuandika Concept note kwa ajiri ya reserch proposal kwa upande wa afya.

2) Naweza kuandaa na kuandika research proposals kwa wanvyuoa wanaofanya research for the awards za Degree kwa gharama nafuu kabisa.

3) Naweza kufanya data analysis kwa kutumia SPSs na kuandaa research report za kwa fani za Uuguzi.

4) Naweza kufanya kazi kwenye clinic za mama na mtoto kama mkunga na muuguzi.

5) Niko mahiri kwenye kazi/shughuli zote za uuguzi mahospitalini na kwenye vituo vya afya, nina uzoefu wa ICU, Emergence department, nina uzoefu wa kazi za medical ,surgical/orthopedic, pediatric, maternity, Labour ward, Dialysis, RCH clinic, MOT, na Psychiatry.

6) Naweza kufanya kazi kwenye maduka ya huduma za fedha kama vile airtel money, M-pesa n.k

7) Naweza kusimamia biashara au kazi na ikaenda vizuri kwa uaminifu mkubwa sana.

8) Naweza kutoa home based care za kiuguzi, na naweza kuwa muuguzi wa familia.

9) Naweza kutoa palliative care.

10) Naweza kufanya kazi ya sales representative kwa bidhaa za kampuni za dawa.

11) Naweza kufanya kazi ya kuuza duka la; vifaa vya umeme, vyombo, nguo, vifaa vya ujenzi, funitures n.k

12) Naweza kufanya kazi za stationery na nina uzoefu mzuri wa kutumia komputa.

14) Ninaweza kufundisha masomo ya Chemistry, biology na Geography kwa umahiri mkubwa.

15) Ninao uzoefu wa kutoa uhauri na nasaha kwa watu waliokata tamaa either ya shule/kusoma, maisha na afya kwa ujumla.

16) Naweza pia kuwa business partner kwa mtu mwenye mtaji, Mimi shida nj mtaji.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wewe uliye soma hapa.

Naomba mwenye kazi au connection ya kazi ani pm tafadhari.
 
2) Naweza kuandaa na kuandika research proposals kwa wanvyuoa wanaofanya research for the awards za Degree kwa gharama nafuu kabisa

Unajua kama hili la kumwandikia mtu research ni kosa linaloweza kusababisha discontinuation kwa mwanachuo? Matatizo yasifanye tukiuke sheria na misingi ya nchi.

Usirudie tena kumfanyia mwanachuo research haujengi graduate bora bali unabomoa na unapaswa kushtakiwa
Kwani hapo amesema research au research proposal?
 
Pole sana Doreen. Inasikitisha sana kuona muuguzi kama wewe unakosa ajira pamoja na kuwa kuna upungufu mkubwa sana wa Wauguzi nchini. Ni rahisi watu kusema jitolee ufanye BURE wakati hata hiyo nauli ya kwenda na kurudi huko utakajitolea huna. Pesa ya kulipia pango au ya kupata hata mlo mmoja kwa siku huna. Pole sana.
Uyo hana hata leseni kwaiyo ni ngumu kupata izo kazi labda umuajiri at your own risk
 
Back
Top Bottom