Naomba ifanywe kwa dharura: Napendekeza kuanzia Jumamosi iwe ni marufuku mtu kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa/ barakoa/ scarf

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,082
40,735
Napendekeza katika hali ya dharura sana, serikali itangaze kuanzia jumamosi hii iwe ni marufuku kwa mtu yeyote kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa au scarf, na kama ana uwezo wa kununua barakoa basi avae barakoa.

Japo barakoa/ scarf haikukingi moja kwa moja na maambukizi kwa sababu bado macho yapo wazi, lakini inasaidia kuwalinda wanaokuzunguka pale unapokohoa au kupiga chafya, shida inayokuja sasa hivi ni kwamba mtu kwa nia njema kabisa unapotaka kuvaa barakoa watu wanakushangaa na kukugeuza kituko.

Its very unnerving, ndio maana wengi tumeacha kuvaa hizo barakoa, ila Serikali ikitangaza kwamba ni lazima basi kila mtu atavaa na hakutakuwa na wa kumshangaa au kumgeuza mwenzie kituko /kivutio cha utalii na kumshangaa shangaa anapopita.

Natoa masaa 12 tu hili lifanyike. NB: Sitaongeza muda.
==================================

Update: 18/04/2020
Paul Makonda: Kuanzia jumatatu kuvaa barako, leo, kipande cha khanga kufunika uso ni lazima, sio hiari, huna kaa ndani! - JamiiForums











====================================
Update: 29/04/2020
Nasikia wasiovaa barakoa wanatembezewa kichapo sasa..
Polisi wameweka kambi Ilala Sokoni, wanashusha abiria wasio na barakoa na kuwacharaza bakora - JamiiForums
 
Nakuunga mkono.
Serikali imechelewa na inachelewa sana kutoa tamko la kujikinga zaidi ya kunawa mikono.

Watu wote tungeanza mapema kukinga midomo na pua ingesaidia kupunguza maambukizi kwa njia ya chafya na kukohoa.

Unakuta basi zima hakuna hata MTU mmoja aliyefunika USO. Watu wanaingia msikitini na kusujudi bila kuvaa maski wakati anapogusa ardhini ndipo mwngine alipogusa dk chache zilizopita.

Pia watu wanunue gloves wavae kwani zinafaa kuosha kwa sabuni na kuvaliwa tena na tena. Mana sio kwamba zinatumika hospitalini Bali ni kugusa vitu na kisha zinaoshwa na sabuni kisha MTU asiye na uwezo anavaa tena kuliko kuuza vitu sokono mikono mitupu na mdomo na pua wazi.

Watoa huduma wote wavae maski kwa kweli mana huenda bidhaa wanazouzia watu wanazipigia Chafya au kukoholea halafu wateja wananunua.

Wauza vyakula na vinywaji nao wavae maski na mikononi wavae gloves.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kweli tumeanza kuambukizana wenyewe kwa wenyewe inabidi ingawapo kwenye miji husika kama dar sheria hiyo iwekwe pamoja na kuzuia mikusanyiko hatarishi.
 
So kwa kuwa wewe umenunua kiboksi Cha maski umekosa pa kutumia unaforce serikali ikuwekee mazingira ya kuitumia..HV unahisi hicho kiboksi utakaa nacho kwa muda gani? Umewafikiria wenzako lakn ambao wanatafuta Ela ya kula Sasa wrwe unataka uwaongezee kazi ya kutafuta Ela ya mask!
Trubarg
Si ajabu huyo jamaa akawa mjasiriamali ambaye ana kiduka chake, sasa anatafuta njia ya "kutupiga"
 
Ndugu yangu usijali nani anakucheka wewe kama unazo za kuvaa endelea kuvaa suala la afya ni la kwako binafsi, hata hao wanaoumwa wanaumwa kila mtu lwake na maumivu yake. Yatakapokukuta usijesema niliacha kwa sababu watu walinicheka.
 
Sijawahi kujua tuna watu wa hovyo kiasi hiki, tunafanya masiala kwenye Afya za watu. Tutakwisha tukiendelea na kupuuzia mambo ya msingi. Huenda Tanzania tungekua mbali but tunapuuzia kila kitu ni business as usual. Tutaisha
 
Napendekeza katika hali ya dharura sana, serikali itangaze kuanzia jumamosi hii iwe ni marufuku kwa mtu yeyote kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa au scarf, na kama ana uwezo wa kununua barakoa basi avae barakoa.

Japo barakoa/ scarf haikukingi moja kwa moja na maambukizi kwa sababu bado macho yapo wazi, lakini inasaidia kuwalinda wanaokuzunguka pale unapokohoa au kupiga chafya, shida inayokuja sasa hivi ni kwamba mtu kwa nia njema kabisa unapotaka kuvaa barakoa watu wanakushangaa na kukugeuza kituko, its very unnerving, ndio maana wengi tumeacha kuvaa hizo barakoa, ila serikali ikitangaza kwamba ni lazima basi kila mtu atavaa na hakutakuwa na wa kumshangaa au kumgeuza mwenzie kituko /kivutio cha utalii na kumshangaa shangaa anapopita.
Natoa masaa 12 tu hili lifanyike. NB: Sitaongeza muda.
Wewe kama unazo vaa tu hakuna shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom