Baba Joseph17
JF-Expert Member
- Jul 15, 2013
- 9,518
- 9,722
Utawanunulia?Napendekeza katika hali ya dharura sana, serikali itangaze kuanzia jumamosi hii iwe ni marufuku kwa mtu yeyote kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa au scarf, na kama ana uwezo wa kununua barakoa basi avae barakoa.
Japo barakoa/ scarf haikukingi moja kwa moja na maambukizi kwa sababu bado macho yapo wazi, lakini inasaidia kuwalinda wanaokuzunguka pale unapokohoa au kupiga chafya, shida inayokuja sasa hivi ni kwamba mtu kwa nia njema kabisa unapotaka kuvaa barakoa watu wanakushangaa na kukugeuza kituko.
Its very unnerving, ndio maana wengi tumeacha kuvaa hizo barakoa, ila Serikali ikitangaza kwamba ni lazima basi kila mtu atavaa na hakutakuwa na wa kumshangaa au kumgeuza mwenzie kituko /kivutio cha utalii na kumshangaa shangaa anapopita.
Natoa masaa 12 tu hili lifanyike. NB: Sitaongeza muda.