Nanyimwa unyumba kisa mimi ni mwana UKAWA

Nanyimwa unyumba kisa mimi ni mwana UKAWA

Swala dogo sn Mr Hedex, km kakushinda kwa dogo hilo ina maana yapo mengi ambayo hujayasema huwa mnashindwana, usilegeze uzi anabeep tu hy mfano we ni mshabiki wa yanga na mkeo ni simba mbona huwa ukifungwa anakucheka na wewe hujawai kumnyima unyumba?, kwenye unyumba hakuna baunsa labda km anajusaliti toka ck nyingi, unacheza na tamu Hedex.
 
mwambie akikupa unyumba utampa Laptop ........... hapo hakika atakupa.
 
haya ndio anayofanyiwa na ccm na ndio maana ww ukawa hupewi unyumba
 
Attachments

  • 1439762245739.jpg
    1439762245739.jpg
    18 KB · Views: 382
Msapoti mkeo hivi akifanikiwa si mtakula wote pesa za bunge.
 
Bora unyimwe unaweza ukaleta mtoto nusu chizi nusu timamu. Huyo mkeo ni akili kibwaw
 
Ulipoanza kunyimwa tu ujue tayari kishapata mwingine huoni?? kama kusoma hujua na rangi pia huoni??? Imekula kwako uache kukurupuka. Naye mama hamnazo kabisa, sasa anakulazamisha upende tu hayo magamba na wewe ukimlazimisha apende makamanda si ushindani in the house??? Mijitu mingine bana. hapa ushauri ni mukichwa yako peke yako aisee
 
Mi nikinyimwa huwa silalamiki, najua nini cha kufanya...
 
Habari zenu wakuu!!

Imepita takribani week tatu tokea mheshimiwa waziri mstaafu ENL ajiunge na UKAWA na kusema ukweli mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa natamani na naendelea kutamani mheshimiwa Mamvi ashike hatamu ya urais wa nchi hii tokea akiwa CCM.

Sasa alivyohama CCM na mimi nilihama nae na kuwa Mwana Umoja Wa Katiba ya Wananchi. Tokea hapo shemeji na wifi yenu ameninunia kwa kuwa yeye ni mwana ccm na ni mgombea wa viti maalum mkoa fulani. Sipewi unyumba na ndani hatuongeleshani. Ila majukumu mengine anayatekeleza kama kawaida. Nimejaribu kukaa nae kuongea nae kwa kituo lakini hataki kabisa kuweka maelewano baina yetu.

Na mimi kama mwanaume nahitaji huduma ya mke wangu mpenzi. Hivyo basi wanabodi naombeni ushauri wenu nifanyeje na mimi siwezi kuitema UKAWA.

Fukuza huyo chukua chombo cha UKAWA wewe.
 
Tiketi ya kuchepuka hiyo kaka changamka wewe
 
Mkuu kwanza una moyo mimi siwezi vumilia kulala kitanda kimoja na ccm aisei...!
 
Unafaa Sana Kuwa Mke Wangu Wewe kwa maana Una Maono Na Majibu Sahihi... Karibu Lumumba Japo Upate Hata Kitenge cha Wax

Mambo si ndio hayo sasa! Haya nipe maelekezo nafikaje?
 
Back
Top Bottom