Nanyimwa unyumba kisa mimi ni mwana UKAWA

Hedex

Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
26
Reaction score
11
Habari zenu wakuu!!

Imepita takribani week tatu tokea mheshimiwa waziri mstaafu ENL ajiunge na UKAWA na kusema ukweli mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa natamani na naendelea kutamani mheshimiwa Mamvi ashike hatamu ya urais wa nchi hii tokea akiwa CCM.

Sasa alivyohama CCM na mimi nilihama nae na kuwa Mwana Umoja Wa Katiba ya Wananchi. Tokea hapo shemeji na wifi yenu ameninunia kwa kuwa yeye ni mwana ccm na ni mgombea wa viti maalum mkoa fulani. Sipewi unyumba na ndani hatuongeleshani. Ila majukumu mengine anayatekeleza kama kawaida. Nimejaribu kukaa nae kuongea nae kwa kituo lakini hataki kabisa kuweka maelewano baina yetu.

Na mimi kama mwanaume nahitaji huduma ya mke wangu mpenzi. Hivyo basi wanabodi naombeni ushauri wenu nifanyeje na mimi siwezi kuitema UKAWA.
 
Umeharibu ulivyomuita ENL mamvi.Sintokushauri hadi aidha uhariri uzi wako au ufute kauli.Na uking'ang'ania sana nakupa baridi:thumbdown::thumbdown:😀😀
 
Hata mimi sipati unyumba lakin i nitashughulikia baada ya uchaguzi kuisha ngoja kwana ENL aingie
 
Jaribu kumuelewesha asihusishe siasa na haki ya msingi ya ndoa.Siasa ni huko nje mkisha ingia chumbani ninyi ni mwili mmoja.Ideological different za parties doesn't constitute any rights to empower a woman to run from her basic responsibilities.

Mpendachapati
 
Tafuta mwanaUKAWA mwenzako, CCM na UKAWA wapi na wapi.
 
Habari zenu wakuu!!

Imepita takribani week tatu tokea mheshimiwa waziri mstaafu ENL ajiunge na UKAWA na kusema ukweli mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa natamani na naendelea kutamani mheshimiwa Mamvi ashike hatamu ya urais wa nchi hii tokea akiwa CCM.

Sasa alivyohama CCM na mimi nilihama nae na kuwa Mwana Umoja Wa Katiba ya Wananchi. Tokea hapo shemeji na wifi yenu ameninunia kwa kuwa yeye ni mwana ccm na ni mgombea wa viti maalum mkoa fulani. Sipewi unyumba na ndani hatuongeleshani. Ila majukumu mengine anayatekeleza kama kawaida. Nimejaribu kukaa nae kuongea nae kwa kituo lakini hataki kabisa kuweka maelewano baina yetu.

Na mimi kama mwanaume nahitaji huduma ya mke wangu mpenzi. Hivyo basi wanabodi naombeni ushauri wenu nifanyeje na mimi siwezi kuitema UKAWA.

Mkuu kuwa makini usije kukuta wife anamegwa na vijana wa redbrigade na kuahidiwa ukuu wa wilaya
 
yaan ww akili zimedumaa. mkeo anagombea unaamua kumtosa kwa sbb ya ushabiki wako kwa lowasa. assume ungekuwa ww unagombea halafu yy anakuwa against you. ungejisikiaje. funguka kidogo basi au nenda ukaombewe.
 
Back
Top Bottom