tulieni niwape stori msitingishike!. kulikuwa na binti mmoja anaitwa
farkhina alikuwa anataka kuolewa na wakajitokeza wachumba wawili wanataka kumuoa mmoja anaitwa
Ngongoseke na mwingine
Jerrymsigwa. binti akawa kwenye dilemma kubwa, amuache nani amchukue nani!?. basi akapata wazo la kuwaandalia msosi (ugali wa muhogo na dagaa wa kigoma). ngongoseke hata nusu ya ugali hakufika akasema ameshiba (@jawilat na
Valentina wakasema huyu ndo mwanaume). jerrymsigwa alimaliza ugali wote akataka kula na aliobakiza ngongoseke sema mshenga alimkataza.
sasa farkhina akaulizwa umemchagua nani?. akajibu jerrymsigwa!!.
mimi49 akapigwa na butwaa akamuuliza dada unachaguaje mume mrafi?. farkhina akamwambia, huyo unaemwita mmrafi atafanya kazi kwa bidii kuleta chakula nyumbani sababu atahitaji kula sana ila huyo sharobaro atakuwa ananilisha mahindi ya kuchoma na juisi ya ukwaju. kusikia hivyo mi na
Nambe tukabaki midomo waaazi kwa busara za farkhina.