Nani ungempendekeza awe Rais wa Tanzania?

Ndani na nje ya chama tawala nani? Angefaa kuliongoza hili taifa pendwa bila migogoro ya ovyo nani? Mnayemwamini kupita kiasi ambaye ataweza kuifikisha nchi yetu kwenye maendeleo ya kueleweka

Tuna watu wengi na makini sana kwenye taifa letu na wengine wanaonekana kabsa hawana uchu wa madaraka wamewaachia wenye uchu watoane roho na kuvuana utu na wana elimu ya kutosha ya uongozi na vipawa vikubwa vya kusikilizwa na kueleweka

Nani? Ungependa awe raisi wa Tanzania ambaye unaamini lazima atafanya vizur kwenye uongozi wake

Kizuri hakikosi kasoro hatusemi kama atafanya mazuri 100% hapana lakini at least 80-85% tutajie hapa nani? Anaweza kulisongesha gurudumu hili Kwa nguvu zote

Taja unayemwamini hata kama hajawahi kuwa mbunge au waziri labda ni diwani huko wewe mtaje!! Tu au labda aliwahi kuwa hata raisi miaka iliyopita tutajie

Na ukimtaja kwa chaguo zuri utaweza kukutana naye kwenye kinyang’anyiro cha uraisi 2025-2030

Lowasa
 
Pascal Mayala
 
Tunamtaka dictator haswa kwa mijitu inayoshiba mlungula
1.polepole
2.mtaka
3.Bashiru Ally
4.mpango
 
Mpango anafaa, lakini ni mpole sana mwenye kuongozwa na jazba zaidi.
Mpango akipewa nafasi ya urais, ningumu sana kumaliza hata awamu moja kwasababu atakua hatarini sana kupata mashambulizi ya maradhi ya moyo kwasababu hana uwezo wa kucontrol hasira zake.
Sababu ya mashiko kwangu pia.
 
Majaliwa sio kwamba ni muoga ila mfumo unambana kwa nafasi yake yaani ni kama anatengenezewa mazingira awe hivi tunavyo muona.
But believe me, Majaliwa anauwezo mkubwa wa kuongoza hii nchi.
Hii nchi kwa ilipofika haitaki kiongozi lelemama inataka kiongozi ambaye atasimama kama kiongozi kweli regardless dunia itamtazama kama dictator or not .
Most ya nchi nyingi za Afrika mfumo wa kuongoza ulio bora ni udikteta mambo ya demokrasia ni uongo na kuendeleza umaskini
Hoja yako ina mashiko kwangu mimi, huwa nasema uongozi siyo lelemama. Laiti hii falsafa ingetiliwa maanani tungekuwa mbali. Ajabu uongozi imekuwa fursa, ikimaanisha mwenye sifa na asiyekua nazo wote wapo ndani, unaweza ona matokeo yake ndiyo uozo uliojengeka ktk system nzima.
 
Back
Top Bottom