Nani unamu-admire hapa JF?

Nani unamu-admire hapa JF?

Kule kwenye jukwaa la Siasa balaa! Ukiingia utapata wengi wanaoboa na wengine wanafurahisha. Binafsi nawependa Baba Desi na Mzee mwanakijiji ni watu wenye Busara, Uporoto pia ananifurahisha huwa anatia chachandu kwenye mada nyingi
 
Kwa kweli sijawahi kuboreka ndani ya jf, zaidi kila siku ninapoingia humu nafurahia kila mchango unaotolewa na kila memba. Zaidi members wa jukwaa hili huwa wananikuna sana!
 
Mimi nawapenda watu wa aina hii:

a. Wanaouliza maswali wasiokubali kirahisirahisi: Hili ni kunddi la watu ambao lolote litakalosemwa kuhusu jambo lolote mwitikiio wao wa kwanza ni "je ni kweli", "nani kashuhudia", "Lete picha", "ushahidi uko wapi". Yaani ni kundi la inquisitive minds. Hawa ni watu ambao wakijiridisha kiakili basi huamini moyoni. Kundi la Wanafilosia.

b. Wanaofikiri kabla ya kuanza kujibu: Kundi hili pia lina watu ambao wakisoma kitu hata kikiwagusa vipi hawakurupuki kujibu mara moja bali hutumia muda kurudia kusoma tena, na hata kama kinawagusa wanafikiria kujibu kwanza kwani wanataka wazungumza wanachomaanisha na wamaanishe wanachozungumza. Kundi hili halijibu kutoka katika hisia bali katika kufikiria. Hili mara nyingi ni kundi la watu ambao tunaweza kusema walipoingia darasani na darasa liliwaingia; siyo walioingia darasani na darasa likawapita! Kundi la Wasomi

c. Watu ambao hawakasiriki kirahisi na hawana tahamaki ya pupa. Mara nyingi watu tunaposikia vitu tunaweza kuumizwa, kushtushwa, kutishwa au hata kukasirishwa sana. Katika maisha ya kawaida unaposoma JF unaweza ukajikuta unapata hasira za ghalfa au taharuki ya aina yake. Sasa wapo watu ambao JF imewafundisha ustahimivu na uvumilivu wa aina yake. Mambo ambayo zamani yalikuwa yanawasumbua kwenye mtandaao huu wamejifunza kuyachukulia "with a light sense of humor" kiasi kwamba hawakasiriki kirahisi. Nakumbuka zamani kulikuwa na watu wakianza kupingwa humu wanakimbia na kuisusa JF na kuhuzunika na wengine hata kujisikia kulia kwani walisema walichomaanisha lakini watu "wakawaelewa vibaya". Kumbe baada ya muda wakaja kujua sisi sote humu ni ndugu moja, na tunataniana, kuchokozana na wakati mwingine kukasirishana and then kuchekeshana! Utaona watu wamejifunza uvumilivu ambao umewasaidia hata katika maisha nje ya "virtual world" tunayoishi sasa. Kundi la Wachekeshaji.

d. Watu ambao wanapenda kujenga urafiki kuliko uadui. Kuna kundi limo humu ambalo watu wake wanapenda kuwa marafiki na watu na hawana jambo lolote la kutafuta ugomvi na mtu. Hawa hawapendi kusema kitu kitakachomuudhi mtu au kufanya kitu ambacho kitasababisha mtu ajisikie kaonewa, kadhalilishwa, katukanwa au kwa namna moja au nyingine kafanywa duni. Kundi hili liko sensitive sana kwa hisia za watu wengine, ni wapole, wanajali na hawachelewi kuja na kuwa wapatanishi wakiona mambo yanaanza kukorogeka kati ya wanachama. Hili ni kundi la Wapatanishi.

Naam! Kwa namna moja au nyingine na kutegemeana na siku kwa siku sote tunajikuta wakati mmoja au mwingine tukiwa katika mojawapo ya makundi haya. Wachache huishi katika "box" la kundi mojawapo na hawatoki humo. Wachache waliwahi kuwemo kwenye box moja na wameweza kutoka katika kile kinachoitwa "kufikiri nje ya sanduku". Na wengine wako kwenye makundi yote hayo na zaidi. Ana kheri yule aliyeko mwote. Huyo is my best inspiration, my best friend, my best company and is the best of the best.

M.M.
 
kuna watu wanaridhika na michango ya wengine, sio hata kama hauna la kuchangia basi uropoke tu eti kisa uchangie thread ya fulani,ndio mwisho wake unatoa tu pumba
 
Gaga I love you (and that is genuine) not bcoz niko kwenye list ya marafiki.....
You are one of the most carefree person hapa jamvini
:A S-heart-2:huna pretense... now that is a good person period!:A S-heart-2:
Thanx AshaD for loving me, i love you so much, uko so aggresive and i love you for that, being me others don't like it, but i know deep down in their hearts i have a small place they just dont recognize it!!!!
 
Hivi nyie hii lovefest mtamaliza lini? Imetosha sasa. Anzeni ku love na wengine jamani.

Spread the love....say something like....I love you Nyani Ngabu...I love you till infinity and beyond. Geeeez
 
Hivi nyie hii lovefest mtamaliza lini? Imetosha sasa. Anzeni ku love na wengine jamani. Khaaaa!!

Spread the love....say something like....I love you Nyani Ngabu...I love you till infinity and beyond. Geeeez

SoA loves you alot Nyaniizzo!!Haya acha wivu....!
 
Thanx AshaD for loving me, i love you so much, uko so aggresive and i love you for that, being me others don't like it, but i know deep down in their hearts i have a small place they just dont recognize it!!!!


Gaga watu woote wakikupenda sio nzuri... if you understand kua wapo
tunaokupenda then that is a good thing and it is enough... wasiokupenda wacha wasepe...
na sio kwamba hawana umuhim... wana umuhimu for wanakukumbusha you are not perfect thus a perfect human being....
 
Kwa kweli sijawahi kuboreka ndani ya jf, zaidi kila siku ninapoingia humu nafurahia kila mchango unaotolewa na kila memba. Zaidi members wa jukwaa hili huwa wananikuna sana!
Nilisahau unajua humu kuna memba wengi sana huyu katavi nilimsahau ananifurahisha sana kwanza nikiiona tu Avatar yake nasikia furaha, halafu michango yake huwa inanifurahisha sana ni mtu wa utani asiyependa kuudhi watu. Nakukubali kaka kama hujaoa nitakuachia wa kwangu si unatua wamasai......... Usijichekee natania tu.
 
Hivi nyie hii lovefest mtamaliza lini? Imetosha sasa. Anzeni ku love na wengine jamani. Khaaaa!!

Spread the love....say something like....I love you Nyani Ngabu...I love you till infinity and beyond. Geeeez



Nyani Ngabu I love you despite the fact you think am a guy.... are you good sasa??? Let the above statement in Purple do its thing bana....lol
 
hahaha, NN, ulishawahi kukutana na '' the penguins of madagascar''? U sometimes remind me of King Julian, afu kuna mtu ananikumbusha Maurice...,lol!
Hivi nyie hii lovefest mtamaliza lini? Imetosha sasa. Anzeni ku love na wengine jamani. Khaaaa!!

Spread the love....say something like....I love you Nyani Ngabu...I love you till infinity and beyond. Geeeez
 
Back
Top Bottom