Nani Role model Wako?

Nawasalimu Wote!

Kuna Msemo " We are What
We are Because of Other people"

Ni Ukweli Kabisa Kwenye
Hekaheka Zetu Za Kila Siku
Tuna Fanya Mambo Mengi
Makubwa Kwa Kuiga Mfano
Toka Kwa Mtu Au Watu Fulani

Niwe Muwazi Kwa Hapa Bongo
Ninao Watu Wanaonifanya Niwe
Mtu Wa Tofauti Kwenye Nyanja
Mbalimbali Kwa Mfano Kwenye
Siasa Namkubali Sana Andrew
Chenge, Kwenye Sheria Lissu,
Kwenye Utajiri Nimrod Mkono.

1. Andrew Chenge - Amenifanya
Nidhamirie Kuwa Mwanasiasa
Wa Aina Yake. Sijui Nitampataje
Nionane Nae Uso kwa Uso.


2. Tundu Lissu - Amenifanya
Niipende Taaluma Ya Sheria
Ukiachalia Mbali Nilikuwa Mpenzi
Wa Sayansi Lakini Huyu Mtu
Amenifanya Nigundue Wito Wangu
Ni Kuwa Lawyer.

3. Nimrod Mkono -Mbali Na Utajiri
Wake Kutotangazwa Hovyo Naamini Hakuna Mtanzania Anaye
Mvaa Kifedha. Anyway, Nimevutiwa
Na Style Ya Utajiri Wake.

Ningependa Kujua Kutoka Kwenu
Watu Walio Saidia Kukubadilisha
Kimtazamo, Kifikra, Kitabia, Kimaendeleo nk....
Role model wangu ni Floyd Mayweather , ukimuona Floyd jua umeniona mimi.
 
1. My mom - Malezi aliyonipatia kwa ujumla...najitahidi na mimi niwapatie watoto wangu


2. Jennifer ( Alaska Tanzania ) kanifundisha kutokata tamaa pale unapohitaji kufanya kitu....kikubwa ni nia na uthubutu...alianza na mayai ila mpaka sasa ana bidhaa nyingi..mafuta, mchele n.k


3. Ruge -ni mtu ambae ukimfuatilia hukosi cha kujifunza kupitia yeye... kwenye fursa msimu wa kwanza nilipata idea ambayo ilinisaidia sana ....
 
Lakini huyu bwana amezungumzia "mtu" kwa maana ya binadamu.

Mi role model wangu ni "watu wasiojulikana"

Natamani siku moja nikutane nao wanipe mbinumbinu...

Kuna watu ningekuwa nshawahamishia ahera, sema nashindwa kwakuwa najulikana...

Sipendi kuona watu wenye mioyo ya kikatili na wenye roho mbaya zilizopitiliza wakiendelea kuwatesa watu wasio na hatia hapa duniani... kwa sababu tu ya chuki za kisiasa.
af22b3e2f6bd8a009434ed6405d7bcb9.jpg


Pokea Wanakupigia Muonane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom