Nani Mwenye Jukumu La Malezi ya Watoto???

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Hali hivi sasa ni mbaya kimaadili, wazazi wanatukana matusi ya nguoni mbele ya watoto na watoto nao wanatukanana bila wowote. Hii nimeishuhudia hapa mtaani, mama alikuwa anamtukana mwanae wa miaka miwili matusi ya nguoni.....ms..nge wewee, una....mbwa, unaf... na wachawi...na matusi mengine ya nguoni.

Mwanzo nilidhani anatukanana na mtu mzima kumbe ni mtoto, kisa alikuwa analia na huyo mama kambembeleza bila mafanikio ndio kaanza kumporomoshea matusi na majirani wengine walikuwa wakishangilia. Sasa najiuliza jukumu la kulea watoto kama hawa ni la nani, ikiwa kazungukwa na jamii ya watu waliopinda..
 
kuna wengine wanazaa na kulea watoto, kuna wengine wanazaa na kukuza watoto

MPE MWALIMU WA ST ....MPELEKE AKIWA NA MIAKA ANGALAU MITATU. AKIKUA UTAFURAHI SANA YAANI HAKUSUMBUI SIJUI MAMA BABA wala MJOMBA. NA AKIFIKA CHUO HANA TIME NA PESA YA WAZAZI WAKE. Watoto wa dot.com si tunaona walivyo?
 
<span style="font-family: comic sans ms"><font color="#000080"><b><font size="4">kuna wengine wanazaa na kulea watoto, kuna wengine wanazaa na kukuza watoto </font></b></font></span>
Kweli...
 
MPE MWALIMU WA ST ....MPELEKE AKIWA NA MIAKA ANGALAU MITATU. AKIKUA UTAFURAHI SANA YAANI HAKUSUMBUI SIJUI MAMA BABA wala MJOMBA. NA AKIFIKA CHUO HANA TIME NA PESA YA WAZAZI WAKE. Watoto wa dot.com si tunaona walivyo?
Gharama tatizo!
 
@Katavi!
Hapo kuna kitu cha kujifunza
1. Je huyo mtoto alizaliwa wakati sahihi
2. Je, wazazi wa huyo mtoto walijiandaa
3. Je, mazingira yalikuwa tayari kumpokea huyo mtoto
4. Je, huyo ni mzazi sahihi .
Kwa huyu mama sina la kuongeza hapo.....

Ni kweli kwa sasa tuna changamoto kubwa sana katika makuuzi za watoto wetu, tusishangae watoto wetu wakawa na tabia ambazo hata sisi wazazi hatujui zilipotoka....
Imagini mtoto toka akiwa na miezi mitatu yuko chini ya malezi ya mahouse Girl (DADA), na sisi wazazi tuko busy na kazi na kuachia hao wamlee. chakula cha mtoto, kulala, kuoga na matumizi ya dawa yote ni hawa madada. Jua hawa wametokea katika familia na makuzi tofauti na wana matabia yao tofauti hivyo ni rahisi kwa watoto kuiga kwa mtu alie karibu yake.
Tunahitaji neema ya Mungu katika hili, ni Mungu mwenyewe anatutunzia watoto wetu, Tuwaombee sana kwa Mungu awalinge na kuwakuuza katika njia yake. napenda sana watoto we acha tuu!!
 
.....kizazi kilichopotea. Ni sawa na kumnyanyapaa na kumtukana baba mtu mbele ya watoto,
au baba mtu kumtukana na kumkung'uta mkewe mbele ya watoto.
 
.... Sasa najiuliza jukumu la kulea watoto kama hawa ni la nani, ikiwa kazungukwa na jamii ya watu waliopinda..

Kaka mtoto unafundisha kile unachojua wewe... Kama unajua takataka ni chakula basi utamfundisha mtoto takataka ni chakula..

Wewe unaona hayo ni matusi..lakini huyo mzazi anaona huo ni wimbo... Nyuma ya mawazo ya huyo mzazi kuna vitu vingi sana kama..elimu, Matatizo ya uchumi, matatizo ya ndoa, Tanesco..yote yamebadili mawazo ya mzazi toka kuona tusi ni baya hadi kuona tusi ni wimbo..

Kutatua matatizo hayo uliyosema inabidi utatue kwanza matatizo yanayomfanya mzazi kufikira tusi ni wimbo badala ya kufikiri tusi ni tusi....Ukiweza kutatua hayo ..basi utaweza tatua hayo matatizo ya kufundisha maadili mzuri kwani mzazi atakuwa naye ana mtazamo mzuri.
 
<font size="3"><span style="font-family: century gothic"><font color="#ff0000">uswazi ndo wanatukana hasa huweze hata kuyaandika hapa.</font></span></font>
Uswazi hakufai kabisa watoto kuishi...
 
Back
Top Bottom