Nani mkubwa ki-protokali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mkubwa ki-protokali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jul 28, 2011.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,066
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Asalam-aleikhum wenzangu katika Mfungo haswa wa visiwani,
  naomba kuuliza ati katika picha hiyo ya hao viongozi nani chief hapo? au ndiyo zile bifu zetu za Uunguja na Upemba huyu Makamo wa Rais wa Bara alitaka hicho kiti cha Rais wa Zanzibar akakosa sasa ni Makamo wa Rais wa Muungano anakosa heshima anamvimbia Rais wa Zanzibar! Wajameni nimeiskia hii baraza watu wakibishana baada ya kula daku huko Stone town! Je ukweli upo wapi? wapi FF atueleze!
   
 2. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  ​Hao walikuwa wameshiba tu...........
   
 3. egbert44

  egbert44 JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2006
  Messages: 361
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inaonyesha hapakuwa na protocali hapo maana naona kuna watu baki tu nao wapo kwenye safu ya Bilali au inaweza ikawa kama mbio ndefu kuna kipindi humjui wa kwanza wala wa mwisho maana wa mwisho anaweza zungukwa hata mara nane na wa kwanza, kwa hiyo hata na hapa Shein anamalizia na Bilali anaanza
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeuliza kiprotokali,Makamu wa rais wa jamhuri ni mkubwa kiprotokali zaidi ya rais wa Zanzibar.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kiprotokali Makamo wa Rais ni Mkubwa kuliko Raisa Zanzibar. Kwenye muungano Rais wa zanzibar ni kama waziri tu na anaingia kwenye vikao vya baraza la mawaziri kama waziri anavyoingia Ngereja
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Hii inasaidiaje wanaokosa futari jamani?
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />

  Hehehehehehe
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Aug 6, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,228
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Je Seif akija bara anakuwa kama nani? Katiba ya bara haimtambui je anastahili king'ora akija dar?
   
 9. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimekutana nae hivi majuzi akiwa kwenye gari ya kawaida bila ving'ora ila gari lilokuwa nyuma yake nadhani ni ecort bila shaka, kama unavyomuona Bi Kiroboto na Mkuu wa geshi letu mara nyingi wanakatiza kimya kimya na wakati mwingine tunakuwa nao kwenye foleni, isipokuwa anapokuwa na issue fulani ya kiserikali inayomuwahisha basi utakuta pikipiki pale mbele na kwa mgeshi ni ile wanteni yao
   
 10. P

  Pure Black man New Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  God Bless Tanzania,
  God Bless Adfrica.
   
 11. t

  takeurabu JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kiprotokali iko kama ifutavyo:
  1. Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania
  2. Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania
  3. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  4. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  5. Speaker wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  6. Makamu wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  7. Makamu wa Pili wa Rais wa seriksli ya Mapinduzi ya Zanzibar
  8. Jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  9. Jaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
  10. waheshimiwa mawaziri wa pande zote mbili
  11. waheshimiwa wabunge/wajumbe wa baraza la wawakilishi
  12. makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara mbalimbali
  13. wakuu wa mikoa
  14. wakuu wa Wilaya
  15. wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Miji
  16. Wataalamu Mbalimbali
  17. wasomi
  18. mabibi na mabwana (akina pangu pakavu tia Mchuzi)
   
 12. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Asante sana sikuwa na idea nani zaidi.
   
 13. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  asante kwa kutufahamisha
   
 14. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mwema na mwamunyange wako wapi?
   
 15. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Madiwani? Dah! Kweli hatupo!
   
 16. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa Majeshi Vipi? inabidi upangue hiyo mkuu.
   
 17. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Spika na Jaji mkuu wanalingana maana wote ni wakuu wa mihilili ya serikali
  Makamu wa Zanzibar hawatambuliwi na Katiba ya nchi umewa rank juu wnastahili kutokuwepo kwenye list
   
 18. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi hii "ranking" ina uhusiano na ukosekanaji wa nishati ya umeme na mafuta?
   
 19. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unaposema Spika wa bunge na Jaji mkuu wanalingana kwa kuwa wote ni wakuu wa mihimili ya serikali, Basi Sika , Jaji Mkuu na RAIS wote wako sawa maana serikali ina mihimili mitatu, ambayo ni Bunge, Mahakama na RAIS na wakuu wake ni Spika(Bunge) Jaji Mkuu ( Mahakama) na Rais! so si kweli kuwa wanalingana! Hivi madiwani nao wanasimama wapi ki protocali!
   
 20. t

  takeurabu JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unakumbuka wakati wa utawala wa mkapa; yeye rais alisafiri, makamu wake alisafiri, na waziri mkuu sumaye pia alisafiri ; speaker wa bunge alikaimu nafasi ya rais wa nchi; kwa nn hakupewa jaji mkuu? kuhusu makamu wa kwanza na wa pili wa zanzibar, walipatikana baada ya kuvunjwa kwa cheo cha waziri mkuu kiongozi wa zanzibar ambaye alikuwa anatambuliwa na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, kwa kuwa katiba hiyo bado haijafanyiwa mabadiliko ndio maana nikawauhisha hapo kwani hata kama hawatambuliwi na katiba lakini wapo!
   
Loading...