Nani mkubwa kati ya binadamu na malaika?

Nani mkubwa kati ya binadamu na malaika?

Kwa Mujibu wa Uislamu Mwanadamu akifanya matendo mema na kuacha kumuasi Allah anakua bora kuliko malaika bcz Mwanadamu amepewa matamanio ila akaweza kuyahimili matamanio yake na kutofanya maasi basi Mwanadamu hapo hua bora kuliko Malaika ambae yeye hana matamanio ila kazi yake kubwa ni kumuabudu Muumba tu
Ungeambiwa uchague uwe malaika au binadamu ungechagua kuwa nani?
 
Malaika, haugui, hafi, hana stress, hasomeshi, hana madeni, ana uwezo mkubwa wa kutembea popote, anaona mbali zaidi ya binadamu, hahisi njaa, wanapendana wao kwa wao, wapo karibu zaidi na Mungu n.k
Hahahaha HASOMESHI, hana MADENI, hana STRESS, hahisi NJAA hahaha hivyo vipengele ni vya moto sana huku chini ya jua.
 
Malaika, haugui, hafi, hana stress, hasomeshi, hana madeni, ana uwezo mkubwa wa kutembea popote, anaona mbali zaidi ya binadamu, hahisi njaa, wanapendana wao kwa wao, wapo karibu zaidi na Mungu n.k
Thibitisha.
 
Nani mkubwa na wa hadhi ya juu kati ya binadamu na Malaika ?

Nani ana maisha mazuri zaidi kati ya binadamu na malaika?
📖 1 Wakorintho 6:3 (SUV)
“Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?”

Hii inamaana sisi ni wakuu wao

USSR
 
📖 1 Wakorintho 6:3 (SUV)
“Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?”

Hii inamaana sisi ni wakuu wao

USSR
Kwa mantiki hiyo kumbe hata malaika nao wanafanya makosa? Binadamu atatumia Sheria ipi kuwahukumu malaika?
 
Thibitisha.
Luka 20
35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi;

36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.
 
Asante.
 
Soma zaburi 8:5

Pia binadamu ana uhuru wa kuchagua, kifalsafa malaika ana utii kamili bila uhuru! Malaika ana nguvu kubwa kuliko sisi lakini mbele za muumba tuna thamani zaidi.😎
huu nao ni uongo eti hana uhuru?? kama hana uhuru mbona shetani alichagua kutotii yeye pamoja na mapepo na vibwengo na majini?
 
Back
Top Bottom