Nani kumrithi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo?

Kufuatia Rais Magufuli kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aachie ngazi kutokana na sakata la 'mchanga wa bandarini'.

Tutoe mapendekezo yetu wakuu ni nani anayefaa kumrithi maana hii Wizara ina changamoto siyo kidogo!


Dr Kalemani anapandishwa kuwa waziri kamili
 
Napenda wampe Mwenyekiti wa tume turudi kwenye Gao wa umeme ndio ajue utendaji siyo hayo makabrasha yake.
 
Sijui ndo Huyu?

Ila Rais amekosea kumtukana aliekuwa Katibu Mkuu wa Wizara yake kwa Matusi yale,Eti Ana stupid Answer Mara anasaliti Taifa wakat kasomeshwa bure na blaa blaaa kibao, amewavunjia heshma kwa Yale Matusi
Na hizo pesa zilizopotea sio matusi kwa Taifa? Kama alikuwa hafahamu si angesema hajui! Kwa nini aseme uongo? Tena raisi wangu kampatia neno zuri kuliko ZUZU.
 
Na hizo pesa zilizopotea sio matusi kwa Taifa? Kama alikuwa hafahamu si angesema hajui! Kwa nini aseme uongo? Tena raisi wangu kampatia neno zuri kuliko ZUZU.

Ton 15.2 za Dhahabu /( Kontena 277 X 20 za Kila Contena) Jibu unalopata kwny asilimia Ni sawa na 0.002%.

Prof alisema kwny Yale Makontena 277 yenye ujazo wa Tons 20 kila Moja dhahabu ni only 0.002% na Hiyo ni kwa Mujibu wa TMAA

na Tume ya Rais Jana imesema kwny Yale Makontena 277 yenye Ujazo wa 20 tons wamekuta kiwango cha dhahabu ni 15.2 Tons.

Tons 15.2 ni sawa na 0.002%

Kama hujapitia hesabu za asilimia na za kugawanya na kuzidisha lazima umuone Yule Prof ni Zuzu!
 
'Most probably' atakuwa Naibu wake Dr. Medard Kalemani.. Ameshapata uzoefu, anayajua makandokando ya mikataba ya madini na anatoka ukanda wa madini..
Ivi inawezekanaje mwanawani waziri aondoke naibu abakie...si wote walikuwa ofisi moja..au sielewi vizuri majukumu yao...haiingii akilini kwamba waziri pekee ndie anajua kinachopikwa jikoni leo na naibu hajui...
 
Mrithi wake ni Profesa kutoka vyuo vya Tanzania , kama unabisha subiri uone.
 
Hilo ni wazo: Tatizo Raisi wetu yuko biased na Waislam pamoja na Wachagga. Hilo linadhihirika katika teuzi zake nyingi. Pengine na kama anavyosema yeye kuwa walimwombea sana Kanisani. Anasahau kuwa Waislam pia walimwombea na kumchagua kwani Lowasa alishaonyesha sura yake Rasmi kwenye kampeni kuwabagua waislam.

Ifahamike kuwa katika Imani ya kiislamu Mwenyezi Mungu anataka watu wafanye Uadilifu kwa yeyote hata kama una chuki naye hilo lisikufanye kutotenda haki. Ile hofu ya mungu ipo. Ukichanganya na mapenzi ya nchi Magufuli anaweza kupata watendaji wengi wazuri ikiwa atajaribu kuweka balance.

wale washauri wake wa karibu wamweleze haya. Ona sasa wateule wake anaowakumbatia kwa sababu zake binafsi wanavyomwangusha kuanzia tume ya madini, Bodi ya Madini, wakala wa TMAAA, katibu wa madini mpaka na waziri. NI AIBU SANA KWAKE!

Kipofu hatayaona mawazo yangu (kwa kuwa system inam-favour) lakini wachache wenye uoni wa kinachoendelea watayaona haya.
Huyo Prof ni mpare kama sijakosea...haya mengine ni maoni yako na una haki ya kusema kile unacho amini..ila kwenye kaya yetu watu wanapewa vyeo kwa kuzingatia taaluma zao na uzoefu wao na si vinginevyo.na daima tuachane na kasumba za kutazama watu wanaoteuliwa kwa misingi ya dini zao,kabila lao au ukanda.tuipende nchi yetu kwanza..na tuwakatae watu wote wanaotaka kutugawa kwa misingi ya kabila,dini au ukanda..Mungu ibariki Tanzania..
 
Hivi ni kipi kilichofanya amteue mtu aliyetoka kwenye kashfa ya ufisadi?..amwache tu aendelee au awe mwenyewe akiona makonda anafaa sawa maana anaweza pia kumteua mbunge aliyemteua akawe balozi kama kawaida yake.
hesabu janga la taifa. tukija kustuka tutajiona upuuzi wetu
 
Kufuatia Rais Magufuli kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aachie ngazi kutokana na sakata la 'mchanga wa bandarini'.

Tutoe mapendekezo yetu wakuu ni nani anayefaa kumrithi maana hii Wizara ina changamoto siyo kidogo!


Prof. Lipumba anafaa kumrithi Prof. Mu..ongo.
 
Hiyo wizara aisimamie mwenyewe(Magu) ili ainyooshe maana ndiko uliko mwanga wa Tanzania tajiri
 
Back
Top Bottom