Nani kumrithi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo?

Hiyo Wizara igawanywe mara mbili
1. Wizara ya Nishati
2. Wizara ya Madini

Kila moja ijitegemee
Suluhisho ni kupitia upya mikataba na sera ya madini, vinginevyo hata Malaika hawezi kuiongoza wizara hii
 
Labda Bashe, wengine wengi ni wale wa kutoweza hata kufikiri wamo bungeni miaka zaidi ya 10 lakini hawana mchango wa maana zaidi ya kudumisha fikra za mwenyekiti.
Umenifungua macho, nimekukubali. Yuko fiti kwa upande wetu, lakini wanafik wa green party wanataka kumtimua ati anachonga sana.
 
kuna
Ni kweli
Nishati iwe wizara na
Madini iwe wizara kamili.
Kwani
Zote zina mambo mengi ya kuyaboresha pia umuhimu wake ni mkubwa.
Tunahitaji sana pesa za madini
Tunahitaji sana umeme.
Kweli, kuna haja ya kutenganisha Nishati na Madini, kutokana na na unyeti wake.
Sikumbuki ni waziri gani alishawahi toka salama ktk Wizara ya Nishati na Madini.
 
Wizara Hii iwe chini ya ofisi ya rais kwa sasa mpaka hapo mambo yatakapokuwa sawa.
 
Kuna Mmoja Rais anasema alihongwa na Mwingine anajiita Prof wakati ni Dkt, Magu Mtu wa nginja nginja sana

Staha hakuna kabisa, huwezi kumwita mtu aliyekuwa mtumishi chini yako kuwa anastupid answers, halafu eti mwingine anasema ni profesa kumbe ni Dr. tu, maana mkuu hajui kuwa uprofessor hausomewi, ni seniority tu kutokana na mchango fulani kwenye hiyo fani unayohudumu? So sad!!!

Ila Muhongo tutamkumbuka tu, he is a very smart guy, toka aingie pale unaona kabisa mabadiliko kuliko wale wengine hata ukiwaita kwenye makongamano pale chuo ya kulaunch program husikii hata wanaongea nini.
Politics za kijinga sana hapa nchini, halafu hao wa kwenye hiyo kamati wengi ni rivals wake toka pale Department, amewapita kwa mbali sana kuanzia exposure mpaka maisha ya kawaida.

Lol!!!!
 
Atenganishe Madini na Nishati ziwe wizara mbili, wizara hii ina changamoto nyingi sana, ukisema uzitatue za nishati, wanakupiga Kwenye madini, ukisema uangalie madini, bei ya umeme inapanda Bila kujua!! Muhongo alielekeza nguvu zake nyingi Kwenye nishati watu wakapitisha makinikia!! Atakayemrithi ahakikishe ana miguu sawa na viatu hivi vyenye rangi mbili na size mbili tofauti.
 
Mwenyekiti wa tume hii hii atalamba shavu, na kule TMAA mwenyekiti wa ile tume ya pili atalamba shavu

Namfahamu vizuri Mwenyekiti wa Kamati. Nina hakika itakuwa ni failure ya wazi.
 
Back
Top Bottom