Nani kaua kwa michano katika hii ngoma mpya ya Izzo Bizness inayoitwa "Nilipotoka”

Mmea Jr

JF-Expert Member
May 20, 2016
551
1,222
Wazee wazee wazee, recently hizo bizness kaachia chuma ambacho ndani yake kuna wakali kibao wa hip hop waliotupia verse zao.

Versa ya kwanza kabisa unakutana na one the incredible akiwa kafanya yake, verse ya pili anaipokea izzoo naye katupia swagger zake pale verse ya tatu ni mnyama chaba toka pande za chugaa wazeee wazee sina chakusema juu ya alichokifanya huyu jamaa.

Then anakuja P Mawenge kama kawaida yake hajawai haribu after that anakuja kaa la moto akifuatiwa na lugombo mwisho kabisa dizasta vina.

Ikumbukwe ngoma za hip - hop za style hii (ambayo ndani yake kuna kuwa na wasanii wengi );bongo tumeshaziona sana hapo nyuma mfano nako2nako walishawai fanya style hii pia.

Sasa wakuu hebu tuje tuongee nani kawakimbiza wenzie? mimi upande wangu kura yangu inaenda moja kwa moja kwa huyu jamaa anayeitwa chabaa aisee huyu jamaa kafanya niamini ule usemi kuwa hip - hop ipo Arusha.
 

Attachments

  • Izzo Bizness Ft. One The Incredible, Chabba, P The MC, Kaa La Moto, Lugombo, Di.mp3
    7.4 MB
Nadhani hii Ngoma ipo kwenye Album yake mpya nilijaribu kuisikiliza Ila Ngoma iliyonikosha kabisa ni moja Tu...

Inaitwa "Trust God" kamshirikisha Nikki mbishi... Ile track Kali sana
 
Back
Top Bottom