Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

mode usiunganishe huu uzi popote

Mh Rais na Serikali yake hawakuwa na mpango wa kuhamia Dodoma at least mpaka may mwaka huu na sijui hii ghafla kashauliwa na nani. Hebu angalia yafuatayo
  1. Kama angekuwa na huu mpango katika bujeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama, lakini hakuna fungu la serikali kuhama katika bajeti hii
  2. Kama angepanga kuhama mapema kiasi hiki waziri mkuu katika majumuisho yake katika bunge la bajeti angetoa taarifa hii ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. lakini hili halikufanyika
  3. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji (wote mnakumbuka zile sarakasi). Hii ni kwasababu wangujua kuwa wanahama na DODOMA ni ngome yao hivyo wasingepata wasiwasi wa eti rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na UKAWA.
  4. Kama angekuwa na mpango wa kuhama, nna uhakika asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga.
  5. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar eti ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma ni nyembamba ka mti, angesubili serikali ihamie Dodoma ili wafanye assessment kama bado kuna ulazima wa hizo flyover Dar hasa baada ya wafanyakazi wa serikali kuhamia Dodoma
  6. Kama angekuwa anampango wa kuhama mapema, asingezuia miradi mipya ya NHC kuendelea hasa ile ya Dodoma, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka katika mji huo mkuu
Kwa sababu hizi na nyingine lukuki, napatwa na wasiwasi, nani kamfukuza Mh Rais Dar? magogoni kuna nini?
Mtizamo mdogo sana ndugu. Wakati nyerere anasema serikali itahamia Dodoma ukawa ilikuwepo?
 
tunahoji uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi, kumbuka mwezi wa tisa WAZIRI MKUU anahamia , that means wizara zote ziwe Dodoma before mwezi wa TISA
Maandalizi ya nini?
Tunapeleka muswada,makao makuu ya vyama vyote vya siasa yahamie Dodoma by December,2016,vinginevyo vitakuwa vimejifuta vyenyewe
 
UKAWA tunatisha baada ya Dodoma tutaambiwa MWANZA hiyo Dodoma toka nimezaliwa nasikia watahamia leo ghafla bin vuu muasisi alitamani sana ahamie lakini CDA ikamuangusha itasababisha wagogo wapangishe chumba kimoja 150,000/=
 
UKAWA ni Kiboko
Wamewafukuza mafisadi kwenye jiji la kimataifa DSM. Nendani huko kwa wagogo mtuachie Dsm yetu!! Hatutawaachia hadi dahari!! Yaliogopa kufanyia siku ya mashujaa DSM kwa woga wa Meya kushiriki!!
Ok Dsm ni Mji mkuu wa UKAWA na Dodoma mji mkuu wa CCM!!
Very good!!
Muda wa kupimwa akili umefika
 
Mkuu mimi nimeshangaa sana. Kwanini waziri mkuu anafanya monkey business? Yaani mzuku umepanda nahamia Dodoma!!!! Je budget hiyo imepitishwa na nani? Mawaziri wanaenda huko na naibu wao budget hiyo imepishwa wapi? Wakuu wa taasisi wote na idara zao wataishi huko kwa pesa za budget ipi? it's monkey business
Naanza kuwa na wasiwasi na PM naona kila anachosema mkuu wake anakimbilia utekelezaji wa kasi ya ajabu baadaye anafeli.Mfano ni ile issue ya sukari walikurupuka vibaya mpaka sasa sukari haijashuka bei. Anapaswa kuwa mshauri sio bendera liyo na woga.Miezi miwili unahamisha serikali yote kwa bajeti gani? Nashauri Rais awe anaandikiwa hotuba na akubali kusoma ama sivyo matamko haya yatatimizwa bila kufuata utaratibu na uvunjaji wa sheria na viongozi wengi wanofanya kazi kwa woga kutetea vyeo vyao na matumbo yao.
 
Kama wana hama waheme kweli sio kuhama nusu nusu na kuacha ofisi nyingine Dar hivyo kuwa na ofisi mbili na kuanza kuongeza gharama za serikali. Ikulu tuigeuze iwe jumba la makumbusho tuweke huko na mwenge na mambo mbali mbali au iwe Chuo kikuu maana majengo yale hayawezi kubaki wazi na haiwezekani kuwa na ikulu 2 Safari njema jamani na tuko tayari kuwasaidia kubeba mizigo yenu kwa upendo msiache familia Dar maana hamtatulia huko Dodoma
 
He is a man of action. .what did you expect. ..hivi bila kuthubutu tutafika? Tuiombee nchi yetu huu ndiyo wakati muafaka. ..Mwenye Enzi Mungu ni mwaminifu sana tutafika. .kuwa na imani. Ubarikiwe my friend
 
Amesema mpaka 2020 serikali yote itakuwa imehamia dom, hakusema mwaka huu au ujao, acha kukurupuka na mambo usiyo kuwa na uhakika nayo
 
Mtazamo hafifu na finyu sana.
Unaona miguuni tu huoni mbali kama mawazo yako yanavyodhirisha, hii ishu ya Dom faster imekuwa km ishu ya elimu bure alivyoidandia toka opposition bila kujipanga, matokeo ni amri za kukimbiza, madawati mengi ni feki, toka lini mbao mbichi ikatengeneza fenicha??????? Walimu waliandaliwa vya kutosha kupokea idadi kubwa ya wanafunzi? Madarasa yaliandaliwa, think twice.
 
Amekimbia foleni za dar, mgao wa umeme na mgao wa maji unafanya mchezo nini, dodoma kuna kila kitu
Awamu yenu ni moja na ni ya mwisho, hongereni mmeandika historia na haita kujatokea tena. Uchaguzi ujao kama mtapata viti vitano vya ubunge basi mshukuru Mungu sana.
UKAWA ni Kiboko
Wamewafukuza mafisadi kwenye jiji la kimataifa DSM. Nendani huko kwa wagogo mtuachie Dsm yetu!! Hatutawaachia hadi dahari!! Yaliogopa kufanyia siku ya mashujaa DSM kwa woga wa Meya kushiriki!!
Ok Dsm ni Mji mkuu wa UKAWA na Dodoma mji mkuu wa CCM!!
Very good!!
 
CHDEMA, maana anasema hataki Mikutano CHADEMA/UKAWA wanataka mkutano sasa anaona ubishi umekuwa mwingi bora aende zake.
 
Hizo "qualifiers" hutumika pale mtu anapokuwa hana uhakika na anachokisema.
.
Kwa hiyo una uhakika na maneno haya?:

"Dar imeshakuwa mali ya CHADEMA /UKAWA"

"Mtifuano una...endelea kati ya viongozi wa ccm na chadema huko Dar"

"Sasa hv ... haijulikani nani mwenye sauti ya mwisho kati ya halmashauri (chadema) na serikali kuu (ccm),"

"ccm imeona kuwa ikiendelea kukomaa na mipango ya maendeleo hapo Dar mwisho wa cku sifa zitaenda kwa ukawa"

"hivyo kitengo kimemshauri mkulu aende akafanyie mambo yake dodoma ambayo ni ya ccm 100%."
 
Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?

Makao Makuu Dodoma yalianza kujengwa kati ya mwaka 1974 na 1975
 
Back
Top Bottom