Naanza kuwa na wasiwasi na PM naona kila anachosema mkuu wake anakimbilia utekelezaji wa kasi ya ajabu baadaye anafeli.Mfano ni ile issue ya sukari walikurupuka vibaya mpaka sasa sukari haijashuka bei. Anapaswa kuwa mshauri sio bendera liyo na woga.Miezi miwili unahamisha serikali yote kwa bajeti gani? Nashauri Rais awe anaandikiwa hotuba na akubali kusoma ama sivyo matamko haya yatatimizwa bila kufuata utaratibu na uvunjaji wa sheria na viongozi wengi wanofanya kazi kwa woga kutetea vyeo vyao na matumbo yao.