Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
Ule uharaka ndo unahojiwa mkuu, kumbuka Dodoma inatakiwa ipangwe upya na miundombinu iboroshwe kama uwanja wa ndege, kituo cha mabasi, kuwe na hotels kubwa tena za 5 star, huduma nzur ya hospital,maji n.k. Hivyo si suala la muda mfupi ivyo, na kumbuka bajet ya serikal ipo fixed maeneo mengine as PM kasema mpaka sept atakuwa Dom...Je, hiyo hela inatoka wapi kuwezesha hilo?
 
Jumanne SAA 2 na nusu asubuhi,kafanyeni kazi,hizi siasa zitawatia wendawazimu.Kama una akili kaanzishe mradi Dodoma utakutoa badala ya kukaa kuanzisha tu threads humu JF serikali ni hii hii ya JPM na huwezi ibadilisha,ukijua hilo tu Upo mbioni kupiga hatua.
Tehe umefikaje hapa wewe.
 
Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
ishu si mpango ulikuwepo.. bali kwanini ghafla hiv wakati ilikua mpango uwe wazi sana kwa muda mrefu kiutekelezaji
 
Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
sasa hiyo mika ishirini tulikuwa tnafanya nini au tunangoja nini tusihamie?
 
SONGOKA, umeandika hoja tano kutetea msimamo kwamba huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar na hivyo kukimbilia Dodoma. Hoja zako zikiwa zimehaririwa ili kuzipa muundo wa kimantiki unaoonyesha major premise, minor premise na conclusion, ni hizi hapa:
  1. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, katika bajeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama. Lakini atika bajeti ya 2016/2017 hakuna fungu la serikali kuhamia Dodoma. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  2. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Waziri Mkuu angetoa taarifa hii katika majumuisho yake katika bunge la bajeti ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. Lakini, Waziri Mkuu hakutoa taarifa hii katika majumuisho yake katika bunge la bajeti ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  3. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji la Dar. Lakini, CCM walihangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji la Dar kutokana na wasiwasi kwamba rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na upinzani. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  4. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, nina uhakika Rais asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga. Lakini, Rais amepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  5. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Rais asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma anakotaka kuhamia ni nyembamba kama mti a kitendo cha kuhamia Dodoma kinaweza kupunguza foleni Dar. Lakini, Rais amejikita katika ujenzi wa flyover Dar ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma anakotaka kuhamia ni nyembamba kama mti na kitendo cha kuhamia Dodoma kinaweza kupunguza foleni Dar. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  6. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Rais, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka Dodoma kwa sababu ya kuhamia huko, asingezuia miradi mipya ya NHC kule Dodoma. Lakini, Rais, bila kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka Dodoma kwa sababu ya kuhamia huko, amezuia miradi mipya ya NHC kule Dodoma. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
Nazikataa hoja zote tano kwa sababu mbili. Kwanza, major premises (blue text) zote zinaelea hewani. Hazina supporting evidence. Nauliza: ni kwanini unafikiri kwamba major premises (blue text) zako zinapaswa kukubalika?

Na pili, sioni kama hitimisho lako linafuata kimantiki kutoka kwenye premises. Nauliza tena: Ni kwa nini ufikirie kuwa rais kafukuzwa badala ya kufikiria sababu nyingine, kama vile kupeleka serikali karibu na wananchi ili kuharakisha monotoring and evaluation?
 
Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
Jibuhoja kwanini hakupitisha wazo hilo bungeni likatengewa bajeti, lakini pia kwa nini aliliingiza Taifa kwenye matumizi makubwa Dar es Salaam kujenga fly oover wakati anahamia Dodoma. Maana bajeti ya fly over angeipeleka Dodoma kupanua barabara na miundo mbinu mingine
 
Na pili, sioni kama hitimisho lako linafuata kimantiki kutoka kwenye premises. Nauliza tena: Ni kwa nini ufikirie kuwa rais kafukuzwa badala ya kufikiria sababu nyingine, kama vile kupeleka serikali karibu na wananchi ili kuharakisha monotoring and evaluation?[/QUOTE]
Monitoring na evaluation ilishafanyika kipindi cha Nyerere. Hoja iliyopo ni kwanini ghafla aamue kuhamia na si mwanzoni mwa maelezo na hotuba zake za namna ya serikali yake itakavyofanya kazi wakati anaingia madarakani.
 
Ule uharaka ndo unahojiwa mkuu, kumbuka Dodoma inatakiwa ipangwe upya na miundombinu iboroshwe kama uwanja wa ndege, kituo cha mabasi, kuwe na hotels kubwa tena za 5 star, huduma nzur ya hospital,maji n.k. Hivyo si suala la muda mfupi ivyo, na kumbuka bajet ya serikal ipo fixed maeneo mengine as PM kasema mpaka sept atakuwa Dom...Je, hiyo hela inatoka wapi kuwezesha hilo?

Kitu rahisi tu, sheria na Kanuni zinaruhusu kufanya mabadiliko ya Bajeti, Spika atakuwa safarini, Naibu ataongoza kikao, UKAWA watakuwa nje ya Bunge. Sitegemei kama kuna mbunge wa CCM atapinga mabadiliko.😛😛😛😛😛
 
Nimemsiliza Mbunge wa Geita Vijijini maarufu kama Msukuma anasema itakuwa karibu na Geita. Naamini Rais anarahisisha kwenda Chato kipindi cha mapumziko maana usafiri wa ndege ana allergy nao
 
Jibuhoja kwanini hakupitisha wazo hilo bungeni likatengewa bajeti, lakini pia kwa nini aliliingiza Taifa kwenye matumizi makubwa Dar es Salaam kujenga fly oover wakati anahamia Dodoma. Maana bajeti ya fly over angeipeleka Dodoma kupanua barabara na miundo mbinu mingine

Wingi wa magari ndio unaopelekea kujengwa kwa flyover, sio uwepo wa makao makuu ya serikali. Mfano Lagos kuna flyover, makao makuu ni Abuja.

Hiki ni kipindi cha sayansi na technologia, shughuli nyingine zitafanyika kwa mtandao sio lazima zihamie Dodoma, pia sio lazima taasisi zote zihamie Dodoma kwa mkupuo.
 
Wale wabunge wanaohamia DSM na kurudi majimboni kipindi cha uchaguzi sijui watasingizia nini maana walikuwa wanasingizia kwenda wizara mbali mbali kushughulikia kero za wapiga kura wao. Sasa mambo yote yatakuwa yamerahisishwa watafute sababu nyingine....Mahudhurio bungeni yataongezeka.
 
Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
Mleta mada anahoji maandalizi na sio kuhama.... kwa vyovyote vile hili ni zoezi ghali sana....
 
Ina maana magogono patabaki kama makumbusho ya taifa auu?? Afadhal tupatege pa kupigia picha
 
Mh Rais na Serikali yake hawakuwa na mpango wa kuhamia Dodoma at least mpaka may mwaka huu na sijui hii ghafla kashauliwa na nani. Hebu angalia yafuatayo
  1. Kama angekuwa na huu mpango katika bujeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama, lakini hakuna fungu la serikali kuhama katika bajeti hii
  2. Kama angepanga kuhama mapema kiasi hiki waziri mkuu katika majumuisho yake katika bunge la bajeti angetoa taarifa hii ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. lakini hili halikufanyika
  3. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji (wote mnakumbuka zile sarakasi). Hii ni kwasababu wangujua kuwa wanahama na DODOMA ni ngome yao hivyo wasingepata wasiwasi wa eti rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na UKAWA.
  4. Kama angekuwa na mpango wa kuhama, nna uhakika asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga.
  5. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar eti ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma ni nyembamba ka mti, angesubili serikali ihamie Dodoma ili wafanye assessment kama bado kuna ulazima wa hizo flyover Dar hasa baada ya wafanyakazi wa serikali kuhamia Dodoma
  6. Kama angekuwa anampango wa kuhama mapema, asingezuia miradi mipya ya NHC kuendelea hasa ile ya Dodoma, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka katika mji huo mkuu
Kwa sababu hizi na nyingine lukuki, napatwa na wasiwasi, nani kamfukuza Mh Rais Dar? Magogoni kuna nini?
Ngoja nikufurahishe: maana najua una hamu... Ya kufurahi...

itakua anamkimbia mwenye mvi nyingi..

Si unajua tena Jiji mmelishika wazee misuso..
 
SONGOKA, umeandika hoja tano kutetea msimamo kwamba huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar na hivyo kukimbilia Dodoma. Hoja zako zikiwa zimehaririwa ili kuzipa muundo wa kimantiki unaoonyesha major premise, minor premise na conclusion, ni hizi hapa:
  1. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, katika bajeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama. Lakini atika bajeti ya 2016/2017 hakuna fungu la serikali kuhamia Dodoma. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  2. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Waziri Mkuu angetoa taarifa hii katika majumuisho yake katika bunge la bajeti ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. Lakini, Waziri Mkuu hakutoa taarifa hii katika majumuisho yake katika bunge la bajeti ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  3. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji la Dar. Lakini, CCM walihangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji la Dar kutokana na wasiwasi kwamba rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na upinzani. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  4. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, nina uhakika Rais asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga. Lakini, Rais amepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  5. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Rais asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma anakotaka kuhamia ni nyembamba kama mti a kitendo cha kuhamia Dodoma kinaweza kupunguza foleni Dar. Lakini, Rais amejikita katika ujenzi wa flyover Dar ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma anakotaka kuhamia ni nyembamba kama mti na kitendo cha kuhamia Dodoma kinaweza kupunguza foleni Dar. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
  6. Kama mpango wa Mh Rais na Serikali yake kuhamia Dodoma ulikuwepo tangu Mei mwaka huu, basi, Rais, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka Dodoma kwa sababu ya kuhamia huko, asingezuia miradi mipya ya NHC kule Dodoma. Lakini, Rais, bila kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka Dodoma kwa sababu ya kuhamia huko, amezuia miradi mipya ya NHC kule Dodoma. Hivyo, huenda, kuna mtu kamfukuza Mh Rais Dar.
Nazikataa hoja zote tano kwa sababu mbili. Kwanza, major premises (blue text) zote zinaelea hewani. Hazina supporting evidence. Nauliza: ni kwanini unafikiri kwamba major premises (blue text) zako zinapaswa kukubalika?

Na pili, sioni kama hitimisho lako linafuata kimantiki kutoka kwenye premises. Nauliza tena: Ni kwa nini ufikirie kuwa rais kafukuzwa badala ya kufikiria sababu nyingine, kama vile kupeleka serikali karibu na wananchi ili kuharakisha monotoring and evaluation?

nimeishia kucheka tu mkuu, mimi professionally am not a journalist. thanks anyway
 
Inasemekana kuna makafara ya hatari na mikataba ya kuzimu vilifanyika pale ikulu na hivyo rais anayeingia kwa chama chochote atalazimishwa kuyafuata bila kupenda.Yasemekana pia ishara ya maagano hayo hutembezwa nchi nzima(asomaye afahamu) ili kuendeleza ibada hiyo inayoiweka nchi wakfu kwa shetani.Nyerere alijua hili na alitamani wale watakaomfuata wasiingie katika vitu wasivyovijua ingawa hakuwaambia wazi.Wao walitakiwa kutekeleza uamuzi huo mapema kwa vile walikuwa wamewekewa mazingira ya kuhama tayari.Ila kwa kupenda raha za mjini na upepo wa beach walijifanya wamesahau kuutekeleza mpango huo.
 
Kitu rahisi tu, sheria na Kanuni zinaruhusu kufanya mabadiliko ya Bajeti, Spika atakuwa safarini, Naibu ataongoza kikao, UKAWA watakuwa nje ya Bunge. Sitegemei kama kuna mbunge wa CCM atapinga mabadiliko.😛😛😛😛😛
definitely
 
Inasemekana kuna makafara ya hatari na mikataba ya kuzimu ilifanyika pale ikulu na hivyo rais anayeingia kwa chama chochote atalazimishwa kuyafuata bila kupenda.Yasemekana pia ishara ya maagano hayo hutembezwa nchi nzima(asomaye afahamu) ili kuendeleza ibada hiyo inayoiweka nchi wakfu kwa shetani.Nyerere alijua hili na alitamani wale watakaomfuata wasiingie katika vitu wasivyovijua ingawa hakuwaambia wazi.Wao walitakiwa kutekeleza uamuzi huo mapema kwa vile walikuwa wamewekewa mazingira ya kuhama tayari.Ila kwa kupenda raha za mjini na beach walijifanya wamsahau kutekeleza mpango huo.
hii kali kuliko zote
 
Back
Top Bottom