Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Dodoma ndipo yalipo makao makuu ya nchi. Na hili si la Magufuli. Tatizo nchi hii ina vijana wengi ambao historia hawana. Zaidi ya miaka 20 tangu uamuzi wa kuhamia Dodoma, leo hii tunahoji nini?
kwa nini ndani hiyo miaka unayodai ni ishirini (pamoja na kuwa ni zaidi) kwa nini serikali ya ccm ilishindwa kuhamia Dodoma?
 
UKAWA ni Kiboko
Wamewafukuza mafisadi kwenye jiji la kimataifa DSM. Nendani huko kwa wagogo mtuachie Dsm yetu!! Hatutawaachia hadi dahari!! Yaliogopa kufanyia siku ya mashujaa DSM kwa woga wa Meya kushiriki!!
Ok Dsm ni Mji mkuu wa UKAWA na Dodoma mji mkuu wa CCM!!
Very good!!
how about Arusha,?

nikuuliza tu na si kingine.
 
Wewe mwenyewe uko hapa macho kodo kusoma na kujibu Thread hizo unazoziponda,kwa maana hiyo na wewe ni Jobless tu kama unaowaponda,wanaofanya kazi hawana hata muda wa kuingia JF muda huu.
Ajira tunasubiri uhakiki kwanza ndipo watu wakafanye kazi
 
Duh hili jambo hata mimi limenitatiza kweli kweli.Bajeti ya kwanza ya serekali ya awamu ya 5 sikuona senti tano ya kuhamia Dodoma.Halafu majengo ya wizara na nk yatafanywa nini au yatapigwa mnada kama nyumba za serekali.

Mbunge wa Mbeya Mjini aliwakusema serekali inaendeshwa kwa mzuka nikadhani anatania kumbe alikuwa sahihi.Kuhamia Dodoma ni maamuzi ya mzuka hayajafanziwa kazi kuona gharama zake na faida na hasara watakayoipata.
 
Mh Rais na Serikali yake hawakuwa na mpango wa kuhamia Dodoma at least mpaka may mwaka huu na sijui hii ghafla kashauliwa na nani. Hebu angalia yafuatayo
  1. Kama angekuwa na huu mpango katika bujeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama, lakini hakuna fungu la serikali kuhama katika bajeti hii
  2. Kama angepanga kuhama mapema kiasi hiki waziri mkuu katika majumuisho yake katika bunge la bajeti angetoa taarifa hii ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. lakini hili halikufanyika
  3. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji (wote mnakumbuka zile sarakasi). Hii ni kwasababu wangujua kuwa wanahama na DODOMA ni ngome yao hivyo wasingepata wasiwasi wa eti rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na UKAWA.
  4. Kama angekuwa na mpango wa kuhama, nna uhakika asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga.
  5. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar eti ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma ni nyembamba ka mti, angesubili serikali ihamie Dodoma ili wafanye assessment kama bado kuna ulazima wa hizo flyover Dar hasa baada ya wafanyakazi wa serikali kuhamia Dodoma
  6. Kama angekuwa anampango wa kuhama mapema, asingezuia miradi mipya ya NHC kuendelea hasa ile ya Dodoma, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka katika mji huo mkuu
Kwa sababu hizi na nyingine lukuki, napatwa na wasiwasi, nani kamfukuza Mh Rais Dar? Magogoni kuna nini?
nadhani huwa kuna fungu la dharura, litatumika hilo
 
Lazima magamba yakimbie dar,maana iko chini ya ukawa.......
 
Mkuu mimi nimeshangaa sana. Kwanini waziri mkuu anafanya monkey business? Yaani mzuku umepanda nahamia Dodoma!!!! Je budget hiyo imepitishwa na nani? Mawaziri wanaenda huko na naibu wao budget hiyo imepishwa wapi? Wakuu wa taasisi wote na idara zao wataishi huko kwa pesa za budget ipi? it's monkey business
Unajua mara nyingi bajeti ya Magufuli iko kichwani mwake, hukumbuki alimpa jaji mkuu bilioni 12 kwani mrejesho wa pesa ile unaujua? ile trilioni itakuwa imepatikana.

Mahakama ya mafisadi itawabana mafisadi watauza mpaka viatu na soksi kufidia walivyoiba.

Mapesa yote hayo hayamo kwenye bajeti lakini yapo na ndiyo anayoyabajetia.
 
Ndio ujue jamaa ana chuki na upinzani mno. Hataki kuwa chini ya ukawa maana Dar iko chini ya upinzani. Sasa natoa wito kwa kina Benson Kigaila nao waiteke na Dodoma kisha tuone watakimbilia wapi. Huu mchezo kweli hautaki hasira
 
You never know labda ameoteshwa! Hii ni Tanzania ya kusubiri rais kesho ataongea nini au waziri ataamukaje. Mipango ya nini wakati mambo yanaende kuelekea kwenye Tanzania mpya.
 
UKAWA ni Kiboko
Wamewafukuza mafisadi kwenye jiji la kimataifa DSM. Nendani huko kwa wagogo mtuachie Dsm yetu!! Hatutawaachia hadi dahari!! Yaliogopa kufanyia siku ya mashujaa DSM kwa woga wa Meya kushiriki!!
Ok Dsm ni Mji mkuu wa UKAWA na Dodoma mji mkuu wa CCM!!
Very good!!

Akili hizi
Nizakutupa
 
Back
Top Bottom