Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Nani kamfukuza Rais wetu Dar?

Mtazamo hafifu na finyu sana.

Mleta uzi hajasikiliza vizuri hotuba ya Rais aliposema kuwa "katika miaka minne na miezi minne ya utawala wake atahakikisha kuwa atahamia Dodoma"! Mihemko ya bajeti ya mwaka huu ya nini? Waziri mkuu anayo ofisi Dodoma kwa muda mrefu na alisema anahitaji nyumba yake ikarabatiwe haraka ili ahamie mwezi wa tisa mwaka huu. Kukarabati nyumba moja unauliza bajeti imepitishwa na nani? Pay attention to detail!!!!
 
miji iliyo karibu na dodoma kukua,biashara kuongezeka na gharama ya kusafirisha mazao ya kilimo na ufugaji kupungua,mengi yataishia dom.Uchumi wa maeneo karibu na dodoma kukua.
 
Hata katika mpango wa Maendeleo wa miaka mitano uliosomwa bungeni na waziri wa fedha jambo hilo halipo kabisa. Jee inawezekana kweli mradi mkybwa kama huo wa kuhamia Dodoma ambao ni lazima matrilioni ya fedha yatumike usiwepo kwenye mpango wa maendeleo wa taifa?
Shida yetu ni kuwa mawaziri na viongozi wote ni waoga hawana ujasiri wa kumuhoji Rais anapotoa kauli na kumu weka sawa
 
Ukawa kweli tuna tisha , ccm wanaikimbia dar ? sasa tujitahidi 2020 tuwabadilishe wagogo ili huko nako wakimbie tena ..teh teh teh ...kwnn tutaichukua manspaa ya dodoma ? Makabila yanayoichukia ccm yatahamia pale ...eg wanyakyusa ..wakinga ..wachaga ..waha ...wanyiha ...wakiingia hapo dodoma , bc inakuwa rahisi sana kuwakimbiza ccm hata hapo dodoma
mkuu wagogo wamekunywa maji ya kijani huwaambii kitu,ila ndio wanaongoza kwa kuombaomba na kula viwajesh wakati wa njaa
 
Jumanne SAA 2 na nusu asubuhi,kafanyeni kazi,hizi siasa zitawatia wendawazimu.Kama una akili kaanzishe mradi Dodoma utakutoa badala ya kukaa kuanzisha tu threads humu JF serikali ni hii hii ya JPM na huwezi ibadilisha,ukijua hilo tu Upo mbioni kupiga hatua.
povu la kijani naona lakuchuruzika pole sana
 
Sina uhakika na ikulu ya Nairobi lakini Uganda ikulu ilikuwa Kampala/Nakasero na baadae imehamishiwa Entebbe.
Kwa 'uswahili' uliopo Dar es Salaam sidhani kama pana tena hadhi ya kuwa kitovu cha shughuli za kiutawala, ni bora ibakie kuwa kitovu biashara na ujanja ujanja mwingine badala ya kuunganisha hivi vitu viwili. Pia ikulu iliyojengwa kwa matakwa na 'vision' ya mkoloni Mjerumani miaka zaidi ya 120 sidhani kama inaendana na matwakwa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiteknolojia, kiusalama nk ya Mtanzania masikini na viongozi wezi wa leo!
Katika vitu vigumu 'alivyovidandia' JPM ni hili la kuhamia Dodoma lakini kiuungwana yuko sahihi tena sana maana miaka zaidi ya 40 ambayo ni mingi sana watawala wako kwenye ngonjela tu za kuhamia Dodoma. Kwa maana hiyo ni bora achukue haya maamuzi magumu ili ikiwezekana aingie kwenye historia na hata ikishindikana basi atakuwa ametusaidia kuufunga mjadala huu wa kuhamia Dodoma.
A life spent in making mistakes is not only more honorable, but more useful than a life spent doing nothing!
 
Jumanne SAA 2 na nusu asubuhi,kafanyeni kazi,hizi siasa zitawatia wendawazimu.Kama una akili kaanzishe mradi Dodoma utakutoa badala ya kukaa kuanzisha tu threads humu JF serikali ni hii hii ya JPM na huwezi ibadilisha,ukijua hilo tu Upo mbioni kupiga hatua.

Wewe mwenyewe uko hapa macho kodo kusoma na kujibu Thread hizo unazoziponda,kwa maana hiyo na wewe ni Jobless tu kama unaowaponda,wanaofanya kazi hawana hata muda wa kuingia JF muda huu.
 
Ni meya wa UKAWA ndiye kawafukuza Dar, Maana kama jana sikukuu ya mashujaa ingefanyika Dar basi ni yeye angeweka sime kwenye mnara wa mashujaa.
 
Wewe mwenyewe uko hapa macho kodo kusoma na kujibu Thread hizo unazoziponda,kwa maana hiyo na wewe ni Jobless tu kama unaowaponda,wanaofanya kazi hawana hata muda wa kuingia JF muda huu.
Punguza Munkari,
 
Ukawa kweli tuna tisha , ccm wanaikimbia dar ? sasa tujitahidi 2020 tuwabadilishe wagogo ili huko nako wakimbie tena ..teh teh teh ...kwnn tutaichukua manspaa ya dodoma ? Makabila yanayoichukia ccm yatahamia pale ...eg wanyakyusa ..wakinga ..wachaga ..waha ...wanyiha ...wakiingia hapo dodoma , bc inakuwa rahisi sana kuwakimbiza ccm hata hapo dodoma
Umefikiria kwa undani sana. Good analysis
 
Sasa we kila asubuhi unapoamka, rais mstaafu huyo mlangoni halafu mmoja tu wengine hamna. Kwanini usikimbilie dodoma?
 
Mh Rais na Serikali yake hawakuwa na mpango wa kuhamia Dodoma at least mpaka may mwaka huu na sijui hii ghafla kashauliwa na nani. Hebu angalia yafuatayo
  1. Kama angekuwa na huu mpango katika bujeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama, lakini hakuna fungu la serikali kuhama katika bajeti hii
  2. Kama angepanga kuhama mapema kiasi hiki waziri mkuu katika majumuisho yake katika bunge la bajeti angetoa taarifa hii ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. lakini hili halikufanyika
  3. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki CCM wasingehangaika kulazimisha kuchakachua matokeo ya umeya wa jiji (wote mnakumbuka zile sarakasi). Hii ni kwasababu wangujua kuwa wanahama na DODOMA ni ngome yao hivyo wasingepata wasiwasi wa eti rais hawezi kuwa katika jiji linaloongozwa na UKAWA.
  4. Kama angekuwa na mpango wa kuhama, nna uhakika asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga.
  5. Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar eti ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma ni nyembamba ka mti, angesubili serikali ihamie Dodoma ili wafanye assessment kama bado kuna ulazima wa hizo flyover Dar hasa baada ya wafanyakazi wa serikali kuhamia Dodoma
  6. Kama angekuwa anampango wa kuhama mapema, asingezuia miradi mipya ya NHC kuendelea hasa ile ya Dodoma, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka katika mji huo mkuu
Kwa sababu hizi na nyingine lukuki, napatwa na wasiwasi, nani kamfukuza Mh Rais Dar? Magogoni kuna nini?
Lakini cha kushangaza, pamoja na maswali yako haya yanayohitaji majibu mazuri kwa Mustakabali wa Ustawi wa Taifa letu, kati ya jana na leo, WASOMI wamepongeza uamuzi huu wa kuhamia Dodoma. Ni jambo jema lakini lilihitaji ratiba kamili.
Hao ndo wasomi wetu, hata kujenga hoja zenye ushauri hawana. Wasomi washiriki kutoa maoni chanya yenye kujenga. Kipekee, mimi binafsi naona kama Taifa, tunayo mambo mengi ambayo tulitakiwa kuyatekeleza kwanza, hilo la kuhamia Dodoma lingepewa kipaumbele, lakini baadae kidogo.
 
Back
Top Bottom