Nani bora kati ya jk na mkapa kwa miaka mtano ya mwanzo

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Kwa mtazamo wangu RAIS JK ameongoza kwa miaka 5 vitu alivyofanya ni hivi:-
  • Uhuru wa vyombo vya habari hii ana asilimia 80%
  • Kupanda kwa bidhaa mara kwa mara
  • Migomo isiyoisha
  • kudanganywa na viongozi
  • Mawaziri bomu esp wale wa viti maalumu
  • Shule za kata pindi Lowasa yupo kwenye Uwaziri mkuu lakini baada ya pinda kuingia ndo ameshindwa kila kitu
  • Udini umeingia
  • Maisha kuwa magumu kwa kila lika, Umeme hali ni mbaya sana, Mafuta hali ni tete,
  • Suala la Muungano amejitahdi
  • Ameshindwa kuwatimua wanaomsaliti
  • Kuporomoka kwa maadili katika kipindi chake cha miaka 5 ndani ya serikali
  • Mikataba feki ya Umeme na TRL
  • Air TANZANIA KUFA

MKAPA ALICHOFANYA NDANI YA MIAKA MITANO 1995-2000
  1. Miundo mbinu alijenga kwa asilimia 70
  2. Kubana uhuru wa vyombo vya habari
  3. Maisha kuwa sawa katika hali nzuri
  4. MME kufanikiwa
  5. Kujenga uwanja mpya
  6. TRL ilikuwa vizuri kwa 70%
  7. Umeme ulikuwa kwa 75%
  8. Uchumi ulikuwa vuzuri sana
  9. Hakuna migomo ya kila mara
  10. Viongozi kumuogopa mkapa
  11. Mkapa na mikataba feki ya madini ingawa hatukujua
  12. Mkapa alijitahidi suala la kutopanda kwa mafuta yalikuwa 800
  13. Alikuwa mkali
  14. Hakukuwa na malalamiko kama ilivyo sasa
  15. Kuuza NBC
  16. Kuuza NMB
  17. Kuuza Mgodi
  18. Ufisdi ulianza
  19. Ni tajiri na marafiki zake wote

Kama kuna mawazo yenu tafadhari you can add, MKAPA ALIFANYA VIZURI KULIKO JK KWA HII TATHMINI INGAWA NAYE ALIKUWA NA MATATIZO YAKE.

MAWAZO YANGU MUNGU AMULINDE KIKWETE AMALIZE MIAKA MITANO HII SALAMA ili tusonge mbele labda upinzani sasa utachukua kwa hali ilivyo sasa.
 
Ni kweli Mkapa alikuwa kiongozi, hata wananchi walimwamini nawakampa kura awamu ya pili 71% kutoka 61%. Jk kafulia mbaya. Akimaliza muda wake hata jumuiya ya kimataifa haitamkumbuka kama alivyo Mwinyi.
 
Mimi nafikiri hata ukilinganisha kwa umbumbumbu marais wote duniani lazima kikwete aibuke kidedea. Kumlinganisha Mkapa na kikwete ni sawa na kulinganisha Mlima Kilimanjaro na kichuguu cha mchwa, respectively. Mathematically, you can say Mkapa = 1,000,000,00....xKikwete.
 
Wote bomu tu hakuna hata aliye na afadhali wameingiza nchi yetu kwenye mikenge ya kifisadi na wao kufaidika kwa ufisadi huo.
 
KWA UJUMLA WAO NAWAPA ASILIMIA KWA KILA KITU KAMA IFUATAVYO


NYERERE 1%


MWINYI 0.98%

MKAPA 2%

KIKWETE 0.100%

tusubiri upinzani uchukue madaraka na utawala wa nchi hii 2015
 
Mkapa is far more better than Kikwete. Myself I supported Kikwete, but he disappointed not only me but majority of his supporter. To be honest they are some people perform better when they are working under supervision of somebody. If you make them lead it is a total disaster. This is what deceived most of Tanzanian about the capability of Mr. President. Thats why he was elected at 81% in 2005.
 
Mkapa kafanya biashara kiwa Ikulu hadi hii leo hataki kusema ni biashara gani aliifanya. Alipokuwa madarakani alihusika moja kwa moja na ufisadi wa kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa, ununuzi wa rada pamoja na kupingwa sana na Watanzania, magari na helicopters za jeshi, kuwaingiza wale makaburu TANESCO kwa mtutu wa bunduki pamoja na kuwa hawakujua lolote kuhusu umeme aliweka mbele kulipa madeni ya nje badala ya kuinua uchumi wa nchi na hata kufanya pesa kuota mbawa na kuwa ngumu kupatikana na hatimaye awamu yake kuitwa awamu ya UKAPA. Aliuza mashirika yetu mengi hata yale ambayo yalikuwa yakiingiza faida kwa kisingizio cha privatization ambayo hadi hii leo hatujaona manufaa yoyote kwa Watanzania, Alisaini mikataba ya kuruhusu uchimbaji wa madini na kuifanya siri kwa Watanzania ambayo tunaambulia 3% tu na mitakaba hiyo bado iko valid hadi hii leo. Kipindi chake ndiyo ule wizi mkubwa wa EPA, Meremeta na Kagoda ulipotokea.

Sasa huu ubora wa Mkapa unatoka wapi ikiwa katika awamu yake kulikuwa na madudu kiasi hiki?
 
KWA UJUMLA WAO NAWAPA ASILIMIA KWA KILA KITU KAMA IFUATAVYO


NYERERE 1%


MWINYI 0.98%

MKAPA 2%

KIKWETE 0.100%

tusubiri upinzani uchukue madaraka na utawala wa nchi hii 2015

SAHIHI MKUU ILA NAONA KAM aNYERERE UMEMPENDELEA,HATA KAMA HAKUFANYA UFISADI ALIKUWA NA UCHU WA KUTAWALA AFRICA NA AKATUMIA RASILIMALI ZETU NYINGI KWA AJILI YA ULAFI WA MADARAKA MIMI NAONA UMEMBEBA

NYERERE 0.1%

MWINYI 0.98%

MKAPA 2%

KIKWETE 0.00000%
 
SAHIHI MKUU ILA NAONA KAM aNYERERE UMEMPENDELEA,HATA KAMA HAKUFANYA UFISADI ALIKUWA NA UCHU WA KUTAWALA AFRICA NA AKATUMIA RASILIMALI ZETU NYINGI KWA AJILI YA ULAFI WA MADARAKA MIMI NAONA UMEMBEBA

NYERERE 0.1%

MWINYI 0.98%

MKAPA 2%

KIKWETE 0.00000%

Pwambafu wewe. Acha kutumia makamasi kufikiri. Nani alikwambia Nyerere alikuwa anataka kutawala Afrika. Ndiyo tatizo la visomi vya shule za kata. 'A wise man talks because he has something to say, but a fool talks because he has to talk'. Narudia tena pwambafu!
 
watu wote wana mapungufu lakini Nyerere mtoe ktk listi hii. Alikuwa na maono na nchi, nchi ilikuwa ktk hali ngumu na alijitahidi sana mzee huyu! Put yourself in his shoes, utamsamehe mwenyewe kwa mapungufu yake. At least he was thinking of citizens.

Back to the topic, frankly maisha yalikuwa bora wakati wa mkapa kuliko kikwete! So ukiwapambanisha wawili hawa mkapa is better, hata ubadhirifu umeongezeka kipindi cha Dr Kanali! Sisemi mkapa is clean or dirty but ujilinganisha maisha bora big Ben!
 
Naamini Mkapa amefanya kitu sahihi katika nchi yangu. Nikiwa na ufahamu mzuri nimeshuhudia ma rais watatu sasa yaani Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Nilimpenda sana Kikwete 2005 lakini alinivunja moyo sana baada ya miaka 2 tu ya utendaji kazi wake. Siyo mie tu niliyevunjika moyo tuko wengi ndo maana mwaka 2010 alipata 61% toka 81% tena kukiwa na uchakachuaji.

Katika ubora pamoja na kuwa wote ni bomu lakini Mkapa namkubali zaidi. Amefanya ambayo hayakuwahi kufanyika Tanzania kama mageuzi katika serikali (Maboresho - yaliyouawa na Kikwete) pili ujenzi wa barabara n.k
 
Mimi naweza kusema kuwa ni awamu mbili tu zimeweza angalau kusaidia Taifa hili. Awamu 1 na ya 3 hizi zingine zinapoteza muda wa Wantanzania tu ki maendeleo. Na katika hizo mbili awamu ya 3 imekuwa bora zaidi, walikuwa wanaiba lakini tulikuwa hatujui kwani walikuwa wanaiba kwa kupuliza kuliko sasa wanaiba kwa wazi wazi. Awamu ya 3 watu walipata Jeuri kidogo ya kiuchumi hasa baada ya kudhibitiwa kwa mfumuko wa Bei. I can dare to mention that, Mkapa is better than others because the country seems to be on a move.
 
Kumlinganisha kikwete na mkapa ni sawa na kushindanisha baiskeli na cruser,kikwete haingii kwa mkapa hata chembe sawa alituibia lkn alibakiza kias sio mkwele ametumaliza kabisa.
 
Hmmm inaelekea wachangiaji wengi wanampa Ben alama nyingi zaidi kuliko JK. Lakini kama mchangiaji mmoja alivyosema wote mabomu. Ben alifanikiwa tu kuwa dikteta zaidi. Baada ya uchaguzi alisimamia watu wengi zaidi kuuwawa kule Pemba. Alibadilisha katiba kurudisha vipengele vya hovyo kama vile kuteua wabunge. Alichakachua matokeo ya uchaguzi mwaka 2000 kwa kupeleka vijana wa CCM kujifunza mbinu za kuiba kura kule Kenya. Waliporudi vijana hao walipiga kura mara kadhaa katika vituo mbali mbali. Hata wino wa kidoleni kujua nani keshapiga kura ulifanywa rahisi kufutika. Ben alipanga wizi mkubwa kama vile EPA, Kagoda, uuzaji wa benki NBC, nk. Tofauti tu kwamba udikteta wake ulifanikiwa kufunika maovu yake mengi ya kukosa uadilifu. Mwenzie JK anashindwa tu kufunika uovu wake. Kati ya hawa wawili hatujapata aliye bora. Kwa hiyo mwaka 2015 tuchague wagombea wa vyama vingine vinavyoonesha muelekeo.
 
Hmmm inaelekea wachangiaji wengi wanampa Ben alama nyingi zaidi kuliko JK. Lakini kama mchangiaji mmoja alivyosema wote mabomu. Ben alifanikiwa tu kuwa dikteta zaidi. Baada ya uchaguzi alisimamia watu wengi zaidi kuuwawa kule Pemba. Alibadilisha katiba kurudisha vipengele vya hovyo kama vile kuteua wabunge. Alichakachua matokeo ya uchaguzi mwaka 2000 kwa kupeleka vijana wa CCM kujifunza mbinu za kuiba kura kule Kenya. Waliporudi vijana hao walipiga kura mara kadhaa katika vituo mbali mbali. Hata wino wa kidoleni kujua nani keshapiga kura ulifanywa rahisi kufutika. Ben alipanga wizi mkubwa kama vile EPA, Kagoda, uuzaji wa benki NBC, nk. Tofauti tu kwamba udikteta wake ulifanikiwa kufunika maovu yake mengi ya kukosa uadilifu. Mwenzie JK anashindwa tu kufunika uovu wake. Kati ya hawa wawili hatujapata aliye bora. Kwa hiyo mwaka 2015 tuchague wagombea wa vyama vingine vinavyoonesha muelekeo.

Alifunika maovu lakini alifanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei na hil ndilo analotaka mwananchi wa kawaida kama mimi. Lakini jk amewaachia mafisadi waendelee kuitafuna nchi. Sasa ona bei inavyopanda kila kukicha! Ndiyo tatizo la kuongozwa na 'mswahili'.
 
Tofauti ya Kikwete na Mkapa ni kama ifuatavyo:
KIELIMU
(1) Mkapa MA (1) Kikwete BA

DINI ZAO
Mkapa Kikwete
(2) Mkatoliki Mkereketwa anayeufahamu ukatoliki wake na kuutetea kwa hali na mali (2) Muislam poa asiyejua A or B
MFANANO KATI YAO
Mkapata
(1) Mwizi wa mali za watanzania kajiuzia migodi kwa bei hewa, kajenga mahoteli kibao (2) Richmond, EPA, ni ulaji tupu
huko South Afrika. Mkewe kajilimbikizia mali kwa kisingizio cha kuwasaidia wanawake
 
Back
Top Bottom