Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
na Deo Temba (Tanzania Daima)
KATIKA hali inayoonyesha kutishwa na azma ya wanaharakati kuandaa maandamano ya nchi nzima kupinga utendaji wa kazi wa Bunge, serikali imetoa tamko la kupinga kusudio hilo.
Tamko hilo la serikali linalofanana na ushawishi ulioanza kujengwa katika siku za hivi karibuni na kikundi kimoja cha watu kinachojiita Amani Forum, limepokewa kwa upinzani kutoka kwa wanaharakati wanaoratibu maandamano hayo yaliyochochewa na uamuzi wa Bunge kutangaza kuzima mjadala wa Richmond.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philipo Marmo, amesema hakuna haja ya maandamano kwa maelezo kuwa Bunge linapaswa kuheshimiwa.
Alisema wananchi hawana uwezo wa kuhoji mamlaka za maadili au za uteuzi ambazo hata Bunge limeshindwa kuzihoji, kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kiutawala.
Waziri huyo alisema Bunge limeridhika na utekelezaji wa maazimio yake uliofanywa na serikali, ndiyo maana liliamua kuhitimisha na kuifunga hoja hiyo.
Bunge limeridhika na utekelezaji ndiyo maana mliona waliridhia kulihitimisha jambo hilo, ninyi mlitaka liendelee hadi lini au ni kitu gani kipya ambacho mnakiona kifanyike? alisema Marmo.
Alisema baadhi ya maazimio ambayo hayajatekelezwa, serikali bado inaendelea kuyashughulikia na inahitaji muda wa kuyafanyia kazi.
Bunge limeshindwa kuzihoji mamlaka hizi, tunashangaa wanaharakati wanataka kuzihoji, Bunge lina kanuni zake ambazo ni kama sheria za nchi na zinapaswa kuheshimiwa na kutovunjwa na mtu yeyote hata nje ya Bunge, kwahiyo tusikubali watu kuingilia kanuni za Bunge na kuzivunja, alisema Marmo.
Alipoulizwa kama serikali imewasiliana na wanaharakati kuwataka wasitishe nia yao ya kuandamana, Marmo alisita kujibu, akasema serikali itaendelea kuwaelimisha wanaharakati na wananchi wengine ili waelewe kilichotokea.
Lakini mratibu wa maandamano hayo, Mkurungezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema kauli ya Waziri Marmo haiwatishi. Alisisitiza kwamba maandamano yako pale pale.
Napenda kumwambia Marmo kuwa mpango wa maandamano uko pale pale ndugu yangu, sisi hatutishwi katika hili... tunaendelea na taratibu zetu za kuandaa maandamano haya... tunataka kuwasaidia wananchi wetu, alisema Nkya.
Alisema kitendo kilichofanywa na Bunge hakivumiliwi hata kidogo na watu wanaopenda nchi yao kwani mamilioni ya fedha yamepotea wakati wananchi wakihangaika kwa kukosa huduma muhimu kama vile zanahati, madarasa na maji safi.
Hatujasema ni tarehe ngani tutaandamana, tumedhamiria kuwakomboa Watanzania... wote ni mashuhuda jinsi wananchi wanavyoishi katika ufukara huku kundi la watu wachache wakineemeka kila kukicha, alisema Nkya
My Take:
Hivi kwanini Marmo anajifikilia ni dikteta wa aina fulani mweye ukarimu? Hilo Bunge si Bunge la Watanzania au limekuwa Bunge la Mbinguni? Hao wabunge si wanachaguliwa na wananchi inakuwaje wananchi washindwe kuwahoji hata kulalamikia? Hivi Bunge la Tanzania na Rais wa Tanzania wako juu ya Watanzania?