Nani atamfunga kinywa Marmo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atamfunga kinywa Marmo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 2, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  na Deo Temba (Tanzania Daima)

  KATIKA hali inayoonyesha kutishwa na azma ya wanaharakati kuandaa maandamano ya nchi nzima kupinga utendaji wa kazi wa Bunge, serikali imetoa tamko la kupinga kusudio hilo.

  Tamko hilo la serikali linalofanana na ushawishi ulioanza kujengwa katika siku za hivi karibuni na kikundi kimoja cha watu kinachojiita ‘Amani Forum’, limepokewa kwa upinzani kutoka kwa wanaharakati wanaoratibu maandamano hayo yaliyochochewa na uamuzi wa Bunge kutangaza kuzima mjadala wa Richmond.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philipo Marmo, amesema hakuna haja ya maandamano kwa maelezo kuwa Bunge linapaswa kuheshimiwa.


  Alisema wananchi hawana uwezo wa kuhoji mamlaka za maadili au za uteuzi ambazo hata Bunge limeshindwa kuzihoji, kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kiutawala.


  Waziri huyo alisema Bunge limeridhika na utekelezaji wa maazimio yake uliofanywa na serikali, ndiyo maana liliamua kuhitimisha na kuifunga hoja hiyo.


  “Bunge limeridhika na utekelezaji ndiyo maana mliona waliridhia kulihitimisha jambo hilo, ninyi mlitaka liendelee hadi lini au ni kitu gani kipya ambacho mnakiona kifanyike?” alisema Marmo.


  Alisema baadhi ya maazimio ambayo hayajatekelezwa, serikali bado inaendelea kuyashughulikia na inahitaji muda wa kuyafanyia kazi.


  “Bunge limeshindwa kuzihoji mamlaka hizi, tunashangaa wanaharakati wanataka kuzihoji, Bunge lina kanuni zake ambazo ni kama sheria za nchi na zinapaswa kuheshimiwa na kutovunjwa na mtu yeyote hata nje ya Bunge, kwahiyo tusikubali watu kuingilia kanuni za Bunge na kuzivunja,” alisema Marmo.


  Alipoulizwa kama serikali imewasiliana na wanaharakati kuwataka wasitishe nia yao ya kuandamana, Marmo alisita kujibu, akasema serikali itaendelea kuwaelimisha wanaharakati na wananchi wengine ili waelewe kilichotokea.


  Lakini mratibu wa maandamano hayo, Mkurungezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema kauli ya Waziri Marmo haiwatishi. Alisisitiza kwamba maandamano yako pale pale.


  “Napenda kumwambia Marmo kuwa mpango wa maandamano uko pale pale ndugu yangu, sisi hatutishwi katika hili... tunaendelea na taratibu zetu za kuandaa maandamano haya... tunataka kuwasaidia wananchi wetu,” alisema Nkya.


  Alisema kitendo kilichofanywa na Bunge hakivumiliwi hata kidogo na watu wanaopenda nchi yao kwani mamilioni ya fedha yamepotea wakati wananchi wakihangaika kwa kukosa huduma muhimu kama vile zanahati, madarasa na maji safi.


  “Hatujasema ni tarehe ngani tutaandamana, tumedhamiria kuwakomboa Watanzania... wote ni mashuhuda jinsi wananchi wanavyoishi katika ufukara huku kundi la watu wachache wakineemeka kila kukicha,” alisema Nkya


  My Take:
  Hivi kwanini Marmo anajifikilia ni dikteta wa aina fulani mweye ukarimu? Hilo Bunge si Bunge la Watanzania au limekuwa Bunge la Mbinguni? Hao wabunge si wanachaguliwa na wananchi inakuwaje wananchi washindwe kuwahoji hata kulalamikia? Hivi Bunge la Tanzania na Rais wa Tanzania wako juu ya Watanzania?
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo ya unicameral legislature... tunahitaji bicameral legislature
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Haya ni maajabu,hivi ni kweli hawa watu huwa wanachaguliwa na kushinda kwa kupigiwa kura hawa?Kuna haja ya kuangalia kwa karibu huu upigaji kura maana haiwezekani eti waseme wananchi hawawezi kuwahoji halafu wananchi hao hao waendelee kuwapigia kura,lazima tufanye uchunguzi hawa watu wanapata vipi kura?
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Maneno hayo ya Marmo yanatia sana uchungu , yanahuzunisha kuliko maelezo.

  Ninapenda aendelee kuyatoa haya maneno tena na tena, nadhani yeye atafanyika kiberiti cha kuwasha moto. Ninaona kwa style hii ukombozi unaweza kutokea mapema sana, believe me nimeona kama ninamzaba kibao vile
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,301
  Likes Received: 1,058
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo mediocrity yenyewe ninayoongelea. Mtu huyu anayesema kuwa "wananchi hawana uwezo wa kuhoji mamlaka za maadili au za uteuzi ambazo hata Bunge limeshindwa kuzihoji, kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kiutawala" kweli anajua wajibu wake na wa serikali yake. Unfortunately sisi watanzania wenyewe tulivyo mediocre pia tutanyamaza tu na baadaye tutasahau na kuwapoa wapuuzi hawa madaraka tena.
   
 6. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,638
  Likes Received: 4,149
  Trophy Points: 280
  Tanzania,Tanzania,nakupenda kwa moyo wote!Nchi yangu Tanzania Viongozi wako ni werevu sana!

  Hizi zifuatazo chini ndizo kazi kubwa mbili za Mwananchi wa TZ:

  Mosi,kuwapigia kura na kuwaweka madarakni viongozi na wakisha apishwa kazi yako inakuwa imekwishwa huwezi tena hoji wale uliowapigia kura wanakuwakilisha vipi!

  Pili,mwananchi hana nguvu wala haki kuhoji madaraka ya Bunge hasa kile kilichojadiliwa Bungeni,kufanya hivyo ni sawa ni kuvunja sheria na haki za Bunge na waziri husika anakukaripia!

  Mungu akupe maisha marefu Waziri Marmo,na tunakuhitaji tena urudi Bungeni na uteuliwe tena kuwa Waziri!
   
 7. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Wakuu naomba kujua huyu Mh Philipo Marmo ni mbunge wa wapi kweli?
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Make no mistake, aina ya misimamo ya Marmo ndiyo hiyo hiyo kwa vigogo wengi wa serikali ya Tz. That is how they think and believe and you wonder why they keep getting elected!!!!

  And these are just ministers je huyo mkuu wao si atakuwa anajiona mungu mtu in some way!!!!!!!
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,832
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee Mwanakijiji, anachotuambia Mhe. Marmo, ndicho alichokisema Spika Sitta siku akikamilisha huu mjadala wa Richmond pale Bungeni, kuwa jambo ambalo limehitimishwa na Bunge, hakuna tena chombo kingine chenye mamlaka ya kuhoji, yaani wanalifanya Bunge kuwa ni quasi judicial body, maamuzi yake ni final.

  Asichoelewa Marmo na Sitta ndani yake, wananchi wanahaki ya kuhoji jambo lolote mpaka kuihoji katiba yenyewe.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Ni Mbunge wa Mbulu na tuliwahi kugongana kwa maneno wakati anaongoza tume ya Vyama vingi..
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  right on.. lakini mbona wao wanahoji maamuzi ya Mahakama na kuyadharau?

  Hili wazo wanasiasa wengi wetu hawajaelewa, hakuna chombo, taasisi, au entity yoyote iliyojuu ya wananchi!
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Fikra sio mbofu mbofu kwa mwananchi wa kawaida hata kwa Philip Marmo alieongoza kundi la G55 kudai Tanganyika yao.. Longway to go....

  Nkya umesema, mimi nasubiri, for real ntakuwepo kwenye andamano la kwanza la jijini Dar. Yasiishie magazetini.
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,331
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kanga, fulana, kofia, pilau na tuhela ndio zimetufikisha hapa
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,832
  Trophy Points: 280
  Nilimsikiliza Sitta kwa makini siku ile alipokuwa anashambulia maamuzi ya mahakamana pale bungeni, alisema Bunge haliwezi kukaa kimya tuu wakati mahakama inajitolea tuu maamuzi yasiyoeleweka.

  Huu msimamo wa Sitta ni ubabe ubabe tuu, lakini kwa upande wa Mhe. Marmo, yeye ni ignorance kuhusu power of the people. Nchi hii, watu wakiamua kuandamana, hawahitaji kibali popote cha kuandamana, wanachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa vyombo husika, kama hivyo vyombo vitaona kuna tishio la amani wanaweza kuyazuia maandamano hayo, na sio justification ya kuandamana.

  Nadhani tunakokwenda, inabidi wajuzi wa sheria, waje on the open kama pale Maelezo, na kusema 'Sorry Hon. Marmo, "You Are Ignorant!"...of the law!", ili aende mahakamani kudai amekashifiwa, ndipo Mahakama itakapokubali kuwa kwa mtu. mwanasheria kama Marmo, kuwa ignorant of the law ni kitu hatari zaidi kuliko hata aliyemuita ignorant.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Mar 2, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Katika mazingira kama hayo ambayo Marmo anataka kuyajenga, kwa Wanasiasa/wanaharakati wa kisiasa kama kweli wanania inaweza kuwa mwanzo wautungu, nasema hivi kwasababu wanasiasa wetu wengi ama waraharakati wanatabia yakuogopa kuwa mbuzi wakafara, wengi hurudi nyuma kwenye mazingira amabayo Gvt inakataa kuridhia harakati zao.
  sasa nawatakia kila la heri wanaharakati wote, mapambano yote dhidi ya wezi wa mali ya umma na dhidi ya bunge dhalili kama hili.
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni kweli wananchi wako juu ya kila kitu ila tu sio by default bali ni kwa wananchi wenyewe kuelewa hiyo haki yao. Viongozi wote duniani wanapenda wawe juu ya wananchi. Sehemu zingine kama TZ wanafanikiwa na sehemu zingine ni ngumu.

  Nadhani huu ni muda wa wananchi kuchukua madaraka yao tuliyo mpa baba wa taifa ambaye naye akaamua kuwapa ndugu zake wakina Mwinyi , mkapa na wengine na siyo kuyarudisha kwa wananchi
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,616
  Likes Received: 2,260
  Trophy Points: 280
  Nadhani hii inaonyesha dhahiri kuwa serekali haitegemei kura za wananchi kuwepo madarakani, maana wanafanya kinyume na taratibu kwani serakali ni mtumishi wa raia.
   
 18. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,525
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ndani ya JF kuna misimamo thabiti kabisa kama michango ya thread hii inavyoonyesha; lakini ikifika kwenye kura, hatuoni misimamo hiyo ndani ya box la kura.

  Hata ukiangalia matokeo ya uchaguzi wa serikaliza mitaa, vijijini wamefanya mageuzi makubwa kuliko mijini wakati JF huko vijijini haipo.

  MANENO MATUPU HAYAVUNJI MFUPA. Hata hayo maadamano huenda yasifanyike!!
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Kamakabuzi.. tangu JF kuanza hakujafanyika Uchaguzi Mkuu.. so.. wait and see..
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,210
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  huyu marmo bana ananikera sana

  yaani anaoongea ongea tu. wanannchi tuna nguvu na saut, wasitubabaishe na kauli za utawala wa sheria, sheria gan hazizingatii haki na usawa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...