Nani atamfunga kinywa Marmo?

Marmo awaponda wanaokusudia kuandamana kuhusu Richmond

Tuesday, 02 March 2010 08:38
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo (pichani), amewashangaa wanaharakati wanaotaka kuandamana kupinga maamuzi ya Bunge juu ya sakata la Richmond na kubeza azma yao hiyo kwa kusema kuwa haitaleta mabadiliko yoyote.
Waziri Marmo aliyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini jana.
Alisema Bunge limekwishamaliza kazi baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa Serikali dhidi ya maazimio 23 ya Bunge katika suala la Richmond na kwamba yale ambayo hayajatekelezwa, yanashughulikiwa na mamlaka husika serikalini.
Alionya kuwa Bunge linafanyakazi chini ya kanuni zake ambazo alisema ni kama sheria za nchi.
Alipoulizwa iwapo Serikali itakutana na wanaharakati ili kujadili suala hilo, alijibu “Sisi tunajaribu kuwaelimisha lakini hatudhani kama maandamano yatatatua jambo lolote," alisisitiza.
Kuhusu Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena katika bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), alisema mambo hayo bado yanashughulikiwa na Serikali.
Muungano wa asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo ya Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct), unawataka wanaharakati hao kuandamana kwa lengo la kuonyesha kutoridhishwa na Bunge.
Wanaharakati hao wanadai kuwa Bunge halikutimiza wajibu katika taarifa zilizofikishwa katika mkutano wake wa 18, kwa kuwa hawakuweka bayana kasoro za Bunge katika kushughulikia masuala ya Richmond, Kampuni ya Ticts, TRL, taarifa ya uchafuzi wa mazingira kwa kemikali za sumu ulioathiri binadamu katika mgodi wa North Mara na ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Loliondo.
Taarifa ya Loliondo haikuwasilishwa bungeni wakati ile ya Ticts na TRL hazikujadiliwa kutokana na kile kilichoelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa taarifa hizo zilikuwa hazijaiva.
Taarifa hizo zimepangwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika Mkutano wa 19 wa Bunge uliopangwa kufanyika Aprili, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
Hilo ndo jambo muhimu sana la kufanywa lakini kwa nchi yetu Tanzania hiyo ni ndoto ya mchana kweupeee, Tanzania hatuna wanasheria(samahani kwa wale nitakaowakwaza), tuna watu wanaojiita wanasheria waliotanguliza matumbo yao front!!
wanasheria wenyewe ndio hao akina marmo na spika sitta, unategemea nini?
TLS yenyewe ndio iko hoi bin taaban, hata siku moja sijawahi kuwasikia wala kuwaona wakiitolea uvivu serikali inapokuwa inafinyanga finyanga haki za watanzania.
Katika hili hatuhitaji wanasheria zaidi yetu sisi wenyewe kuwasema hawa wanasiasa wabinafsi wasio kuwa na heshima kwa watanzania wenzao.
umefika wakati watanzania wote wapenda haki tubadilike, hebu tujaribu kufanya kama mch.Mtikila au Askofu Kakobe japo kwa kuanzia na hili la bunge na richmonduli!!
R.I.P Mchungaji mtikila
 
Nilimsikiliza Sitta kwa makini siku ile alipokuwa anashambulia maamuzi ya mahakamana pale bungeni, alisema Bunge haliwezi kukaa kimya tuu wakati mahakama inajitolea tuu maamuzi yasiyoeleweka.

Huu msimamo wa Sitta ni ubabe ubabe tuu, lakini kwa upande wa Mhe. Marmo, yeye ni ignorance kuhusu power of the people. Nchi hii, watu wakiamua kuandamana, hawahitaji kibali popote cha kuandamana, wanachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa kwa vyombo husika, kama hivyo vyombo vitaona kuna tishio la amani wanaweza kuyazuia maandamano hayo, na sio justification ya kuandamana.

Nadhani tunakokwenda, inabidi wajuzi wa sheria, waje on the open kama pale Maelezo, na kusema 'Sorry Hon. Marmo, "You Are Ignorant!"...of the law!", ili aende mahakamani kudai amekashifiwa, ndipo Mahakama itakapokubali kuwa kwa mtu. mwanasheria kama Marmo, kuwa ignorant of the law ni kitu hatari zaidi kuliko hata aliyemuita ignorant.
Mkuu huwa nakuunga mkono sana. Big up! Hivi hukuwepo pale? Natamani ungekuwepo ukampa kavukavu! Any way, nafarijika kwamba sasa wanahabari wanachukua nafasi yao stahiki katika jamii. Hii itakuwa precedence
 
Back
Top Bottom