Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 954
- 510
Watanzania wengi tumekaa zaidi kishabiki,mambo ya msingi tunayaacha,wanasiasa wanaiharibu nchi yetu tunashindwa kuwakemea, tunawatazama tu na tunapojaribu kufanya hivyo,hatufanyi kwa dhati,zaidi kinachoonekana ni ushabiki ambao kimsingi hauna tija kwa taifa letu.Wanasiasa wanatutumia kama ngazi kwa ajili kuwanufaisha wao na familia zao,wanashindwa kutuletea maendeleo ya ukweli yatakayomfanya kila mtanzania afurahi kuishi na kuwa mtanzania.Lakini ajabu wanasiasa wanajipendelea wao tu huku watanzania wakibaki masikini wa kutupwa hoehae.Viongozi wetu hawana huruma hata kidogo,kiongozi anakubali alipwe 7,000,000 kwa mwezi ilihali kuna mfanyakazi mwingine analipwa 150,000.Jamani mwanasiasa gani Tanzania ni mzalendo tumkabidhi nchi kisha atutoe kwenye huu umasikini?Asiwe mwenye hulka ya kujipendelea,awe na uchungu na Tanzania na watanzania kwa ujumla.
Nawasilisha.
Nawasilisha.