Nani atalikomboa taifa la Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani atalikomboa taifa la Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Aman Ng'oma, Dec 24, 2011.

 1. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 930
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Watanzania wengi tumekaa zaidi kishabiki,mambo ya msingi tunayaacha,wanasiasa wanaiharibu nchi yetu tunashindwa kuwakemea, tunawatazama tu na tunapojaribu kufanya hivyo,hatufanyi kwa dhati,zaidi kinachoonekana ni ushabiki ambao kimsingi hauna tija kwa taifa letu.Wanasiasa wanatutumia kama ngazi kwa ajili kuwanufaisha wao na familia zao,wanashindwa kutuletea maendeleo ya ukweli yatakayomfanya kila mtanzania afurahi kuishi na kuwa mtanzania.Lakini ajabu wanasiasa wanajipendelea wao tu huku watanzania wakibaki masikini wa kutupwa hoehae.Viongozi wetu hawana huruma hata kidogo,kiongozi anakubali alipwe 7,000,000 kwa mwezi ilihali kuna mfanyakazi mwingine analipwa 150,000.Jamani mwanasiasa gani Tanzania ni mzalendo tumkabidhi nchi kisha atutoe kwenye huu umasikini?Asiwe mwenye hulka ya kujipendelea,awe na uchungu na Tanzania na watanzania kwa ujumla.
  Nawasilisha.
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hakuna mwanasiasa mzalendo ,mwanasiasa ni mwanasiasa tu!hii nchi iende mikononi mwa jeshi tu.
   
 3. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtanzania anayefaa ni Bwana William Erio wa PPF.

  Huyu anauchungu sana na wanachama wa PPF hivyo atakuwa na uchungu pia na watanganyika pindi tukimpa nchi aiongoze.

  Huyu hulipwa kamshahara kadogo tu kama Milioni 12 kwa mwezi, Landcruiser VX V8 na dereva, housing allowance ya shs milioni 4 kwa mwezi. Fuel allowance ya shs. 1.2 milion japo ana fully fueled VX, kila baada ya miaka mitatu hulipwa vijisenti vichache kama Group Endowment shs 540 milioni, gratuity shs 108million na samani za nyumbani tshs 60milion.

  Huyu anajitahidi sana kutosafiri sana nje ya nchi, anamzidi kidogo sana Rais wa sasa, 50% ya muda wake wa ajira yuko nje ya nchi na perdiem yake sio kubwa kihivyo, ni analipwa Tshs 1,820,000 (usd 810X1.25X1800) kwa siku kuanzia siku ya kuondoka hadi ya kurudi.

  Safari za ndani ya nch analipwa Tshs 500,000 kwa siku hata kama ni Bagamoyo. Ni kiongozi mzuri atakaye tufaa watanganyika.

  Uzuri mwingine ni ana gene ya uongozi maana ni mjomba wa Rais mstaafu, Bw. Benjemini William Mkapa, kwa hiyo atatufaa wadanyika

  Nawasilisha pendekezo langu.   
 4. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Amina ila kwa wavivu na wezi itakula kwao
   
 5. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  yaani hii nchi ni hakika aina mwenyewe. Hivi hata vitu kama hivi tunashindwa kuyadhibiti? Hivi ni kweli kama yanafanyika na yanafumbiwa macho? Nafikiri imefika kipindi hii nchi itawaliwe na dikteta lkn mwenye uzalendo na kujua nini cha kufanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nguvu ya Umma tuuuuuuuu!!!! Na hakika siku ikifika nawaambia hapatatosha!! Na raia watampa raia mwenye UZALENDO nchi!
   
 7. s

  semako Senior Member

  #7
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni yesu kristo
   
Loading...