Nani atakomesha mila ya 'Sagulaga' Usukumani?

Mila number moja kandamizi kisaiokolijia ni ile mwanamke akitumwa kuleta maji ya kunywa ,anatakiwa apige magoti mpaka huyo mtu anaekunywa maji amalize,nyingine mwanamke mbele ya mwanaume ni mdogo hata kama mwanaume ni mdogo kiumri,mwanamke anatakiwa apige magoti anapomsalimia mwanaume kwa mfano mdogo wake wa kiume,always unapiga magoti unapomsalimia mdogo wako wa kiume na anakuambia Ng'waguku,binafsi mimi hii siikubali kabisa na kamwe simpigii magoti mdogo wangu wa kiume.Mila nyingine mbaya kandamizi ni ile ukiolewa ukweni wewe ndo utakuwa kama house girl,na ukiamka asubuhi unapomsalimia mkwe unapiga goti mpaka jini unaganda hapo mpaka salaam ziishe,moja ya sababu iliyonifanya nisiolewe usukumani.

Nakusoma.

Hii ya kumpigia magoti mdogo wako ki-umri kisa tu ni mwanaume haiko sawa.

Umetisha, eti hukutaka kuolewa usukumani, ungekuja kwetu Kigoma hakuna hizo complications.
 
Mila number moja kandamizi kisaiokolijia ni ile mwanamke akitumwa kuleta maji ya kunywa ,anatakiwa apige magoti mpaka huyo mtu anaekunywa maji amalize,nyingine mwanamke mbele ya mwanaume ni mdogo hata kama mwanaume ni mdogo kiumri,mwanamke anatakiwa apige magoti anapomsalimia mwanaume kwa mfano mdogo wake wa kiume,always unapiga magoti unapomsalimia mdogo wako wa kiume na anakuambia Ng'waguku,binafsi mimi hii siikubali kabisa na kamwe simpigii magoti mdogo wangu wa kiume.Mila nyingine mbaya kandamizi ni ile ukiolewa ukweni wewe ndo utakuwa kama house girl,na ukiamka asubuhi unapomsalimia mkwe unapiga goti mpaka jini unaganda hapo mpaka salaam ziishe,moja ya sababu iliyonifanya nisiolewe usukumani.
Sasa hizo ni mila kandamizi kweli?kwa hiyo unataka umsalimie mkweo huku umesimama kama mlingoti?
 
Niliwahi kuishuhudia hii kule Igunga. Ila mila nyingine za makabila yetu hmmmm! miaka hiyo zilionekana bomba siku hizi zitaonekana ni udhalilishaji wa wanawake.
Ile mila kanda ya kure juu unachomeka mkuki nje unaingia ndan vipi bado ipo!?..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kubali wasukuma wana mila za hovyo... waafrika karibu wote mila zetu zilikuwa hovyo, makabila mengine wameziacha za hovyo, nyinyi bado mnazikumbatia! Hata wazungu walikuwa na mila zahovyo, with civilization wakaziacha!
Mila ipi ya ovyo hata moja iliosalia ya wasukuma!?..
 
Sijui Mkuu kuna mila nyingine alinihadithia mdada ambaye kwao vijana humsaidia mwenzao kumkamata mrembo na kisha kukaa naye kwake kwa siku mbili au tatu basi harusi ndiyo imeshajipa. Yeye aliviziwa na kilema aliyekuja na wenzie wamsaidie lakini bahati nzuri machale yakamcheza akawahi kusepa. Alidai siku hizi haipo tena ila hakuwa na uhakika wa 100%.

Ile mila kanda ya kure juu unachomeka mkuki nje unaingia ndan vipi bado ipo!?..
 
Sasa hizo ni mila kandamizi kweli?kwa hiyo unataka umsalimie mkweo huku umesimama kama mlingoti?
Hujaelewa yaani unaganda chini mpaka mmalize salaam,na salaam ya kisukuma kwa mkwe ni ndefu,kwani kuna ubaya gani kumsalimia mkwe Nikiwa nimesimama ?and why only mtoto wa kike ndo apige goti ?why mwanaume anapomsalimia mkwe wake,hapigi magoti ?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mila kandamizi zipo nyingi na karibu makabila yote nchi kama sio dunian..
Kuna zile mila za kutokaa sehemu moja na mkweo, kutoshikana mkono na mkweo ama kutokula meza moja na mama mkwe, ukioa au kuolewa lazima ukakae mda fulani ukweni vipi nazo ni haki?..
Lakini kwa aina nyingine hizi mila ndo zinatujenga kuwa na heshima na kutupa utambulisho iwapo zikirekebishwa kidogo na sio kuachwa kabisa!..
Kila kabila lina mila kandamizi tukubali!.
 
Wanasiasa waliwaongoza watanzania kupitia bungeni na nje ya Bunge kupinga kwa nguvu zote mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hasa wasichana. Taasisi, Mashirika yasiyo ya serikali, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za dini, watu binafsi walishiriki kwenye vita hii dhidi ya ukeketaji.

Lakini kwa wasukuma kuna mila yao maarufu kwa jina na "sagulaga" ambayo kwa hali yoyote ile ni ukatili lakini pia ni udhalilishaji dhidi ya wanawake. Binti mdogo labda chini ya miaka 14 anafukuziwa na kuzingirwa na wavulana na wakati mwingine na hata vijana wa umri wa miaka 35 mara nyingi akiwa anatokea ngomani na kutakiwa kuchagua mmojawapo ili afanye naye mapenzi.

Cha ajabu ni kwamba binti huyo kwa siku mmoja hutakiwa kwa nyakati tofauti kuchagua mtu zaidi ya mmoja na kufanya naye mapenzi na wakati mwingine huku vijana wanaosubiri "zamu yao" ifike wakisubiria pembeni wakitizama. Si lazima vijana hawa wamuoe binti anayelazimika kuchagua wa kuwa naye kwa siku hiyo!

Jee huu si ubakaji wa ki-kikundi (a Gang rape)? Mabinti hawa wanaolazimika kuishi kwenye mila hii ya kionezi utu wao unaheshimiwa kweli. Tofauti iko wapi kati ya kukeketa na chagulaga? Jee ni mwanasiasa gani ambaye atasimama na kuanzisha harakati za kuitokomeza mila hii Potofu na ya kiudhalilishaji kama ilivyokuwa kwa harakati za kutokomeza ukeketaji nchini mwetu?
..Wasukuma wapo wengi ainisha ni wasukuma wa maeneo yapi wanafanya hiyo mila...wasukuma halisi ambao hawana uchotara hawana hizo mambo na sijawahi kusikia hizo habari.Kwimba,Misungwi nk.............sijui kama kuna sagula...hebu elezea wasukuma wapi...maana kuna wasukuma chotara
 
Sagulaga inafanywa wapi bado?..zaidi ya minada ya jumamosi usukumani ama sherehe ya kisukuma kila mwaka mwezi wa 7 kure mwanza hakuna ngoma kama hiyo.
Hata hii sherehe hua inaheshimika kitaifa na inapewa hadi udhamini.
 
Hujaelewa yaani unaganda chini mpaka mmalize salaam,na salaam ya kisukuma kwa mkwe ni ndefu,kwani kuna ubaya gani kumsalimia mkwe Nikiwa nimesimama ?and why only mtoto wa kike ndo apige goti ?why mwanaume anapomsalimia mkwe wake,hapigi magoti ?
...Hivi ni Elimu ndio inatukengeusha kiasi hiki au ni kutojitambua tumetoka wapi?...siyo mkwe tu! mkubwa yeyote shurti upige goti chini.....Ulisikia wapi binti kafa akisalimia baba yake kwa sababu ya kupiga magoti....??!...Ujuaji mwingine
 
Mila number moja kandamizi kisaiokolijia ni ile mwanamke akitumwa kuleta maji ya kunywa ,anatakiwa apige magoti mpaka huyo mtu anaekunywa maji amalize,nyingine mwanamke mbele ya mwanaume ni mdogo hata kama mwanaume ni mdogo kiumri,mwanamke anatakiwa apige magoti anapomsalimia mwanaume kwa mfano mdogo wake wa kiume,always unapiga magoti unapomsalimia mdogo wako wa kiume na anakuambia Ng'waguku,binafsi mimi hii siikubali kabisa na kamwe simpigii magoti mdogo wangu wa kiume.Mila nyingine mbaya kandamizi ni ile ukiolewa ukweni wewe ndo utakuwa kama house girl,na ukiamka asubuhi unapomsalimia mkwe unapiga goti mpaka jini unaganda hapo mpaka salaam ziishe,moja ya sababu iliyonifanya nisiolewe usukumani.
Duuu,jamaa nyie ni shiidah.
 
Sasa hizo ni mila kandamizi kweli?kwa hiyo unataka umsalimie mkweo huku umesimama kama mlingoti?
Unasumbuliwa na Msukuma chotara...Baba msukuma na mama kanda flani na binti kasikiliza story za Mama lazima upambane na maneno ya hivi
 
...Hivi ni Elimu ndio inatukengeusha kiasi hiki au ni kutojitambua tumetoka wapi?...siyo mkwe tu! mkubwa yeyote shurti upige goti chini.....Ulisikia wapi binti kafa akisalimia baba yake kwa sababu ya kupiga magoti....??!...Ujuaji mwingine
Hahaaa ndo ushangae sasa mkuu
 
Unasumbuliwa na Msukuma chotara...Baba msukuma na mama kanda flani na binti kasikiliza story za Mama lazima upambane na maneno ya hivi
Sukuma pure,Mama Somanda na Baba kutoka Magu.Nimekulia Bariadi.
 
Wewe inavyoonesha umesimuliwa tu halafu unakurupuka kuja kuleta hiyo thread, hiyo mila ilikuwepo miaka ya 1960's, lakn kwa hii miaka haipo na hata ukiwauliza vijana wenye miaka 40 waliozaliwa hiyo kanda hata hawaijui hicho kitu, kilichonifanya nijue kuwa umehadithiwa ni ile neno lenyewe ulivyo liandika "Sagulaga" hilo neno halipo, rudi wakuhadithie upya ndo uje uwadanganye members
 
Hujaelewa yaani unaganda chini mpaka mmalize salaam,na salaam ya kisukuma kwa mkwe ni ndefu,kwani kuna ubaya gani kumsalimia mkwe Nikiwa nimesimama ?and why only mtoto wa kike ndo apige goti ?why mwanaume anapomsalimia mkwe wake,hapigi magoti ?
Mkuu Victoire comment zako zimenichekesha sana
 
Ulimkimbia mume mtarajiwa kwa sababu ya mila!?

Back
Top Bottom