Nani atakomesha mila ya 'Sagulaga' Usukumani?

Nani atakomesha mila ya 'Sagulaga' Usukumani?

Ulimkimbia mume mtarajiwa kwa sababu ya mila!?
Hapana,hii niliapia kabisa hata kabla ya kuingia kwenye mahusiano,kila nilipokuwa naenda wanaume wa kisukuma niliwaita kaka,so ukawa kama ukuta uliozuia mahusiano ya intimity.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Acheni kumshambulia mtoa mada. Kuna mila nyingi sana zinafanywa kwa siri.
 
Lol! Very good technique to keep the distance.

Hapana,hii niliapia kabisa hata kabla ya kuingia kwenye mahusiano,kila nilipokuwa naenda wanaume wa kisukuma niliwaita kaka,so ukawa kama ukuta uliozuia mahusiano ya intimity.
 
Wanasiasa waliwaongoza watanzania kupitia bungeni na nje ya Bunge kupinga kwa nguvu zote mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hasa wasichana. Taasisi, Mashirika yasiyo ya serikali, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za dini, watu binafsi walishiriki kwenye vita hii dhidi ya ukeketaji.

Lakini kwa wasukuma kuna mila yao maarufu kwa jina na "sagulaga" ambayo kwa hali yoyote ile ni ukatili lakini pia ni udhalilishaji dhidi ya wanawake. Binti mdogo labda chini ya miaka 14 anafukuziwa na kuzingirwa na wavulana na wakati mwingine na hata vijana wa umri wa miaka 35 mara nyingi akiwa anatokea ngomani na kutakiwa kuchagua mmojawapo ili afanye naye mapenzi.

Cha ajabu ni kwamba binti huyo kwa siku mmoja hutakiwa kwa nyakati tofauti kuchagua mtu zaidi ya mmoja na kufanya naye mapenzi na wakati mwingine huku vijana wanaosubiri "zamu yao" ifike wakisubiria pembeni wakitizama. Si lazima vijana hawa wamuoe binti anayelazimika kuchagua wa kuwa naye kwa siku hiyo!

Jee huu si ubakaji wa ki-kikundi (a Gang rape)? Mabinti hawa wanaolazimika kuishi kwenye mila hii ya kionezi utu wao unaheshimiwa kweli. Tofauti iko wapi kati ya kukeketa na chagulaga? Jee ni mwanasiasa gani ambaye atasimama na kuanzisha harakati za kuitokomeza mila hii Potofu na ya kiudhalilishaji kama ilivyokuwa kwa harakati za kutokomeza ukeketaji nchini mwetu?
Utakuwa umehadithiwa na mtu aliyekuhadithia hajui vizuri kuhusu hilo.
Kwanza jila lenyewe kama si kutamkwa, pia haliandikwi hivyo.
Pili, dhumu ya ngoma hiyo siyo hicho ulichokiongea na hakijawahi kufanyika kitu kama hicho labda kule MTO KATELERO.
Tatu, mila hiyo ishaishaga hata kabla ya mila zenu za kukeketana hazijaanza kuongelewa.
 
Kila kabila miongoni mwetu kuna milla ambazo ni kioja, lakini hizi za watani zangu zimetisha. Kumbe ndo maana usukumani majanga hayachezi mbali, mmeitelekeza mila yenu muhimu ya "chagulaga"
 
Sukuma pure,Mama Somanda na Baba kutoka Magu.Nimekulia Bariadi.
Ndio maana nimekwambia wewe ni chotara...hapo Baba yako tu ndiyo msukuma pure!!Hujui wasukuma wa bariadi wana mzazi mmoja Kutoka SINGIDA?...JIFUNZE KUJUA ASILI YAKO
 
Wewe inavyoonesha umesimuliwa tu halafu unakurupuka kuja kuleta hiyo thread, hiyo mila ilikuwepo miaka ya 1960's, lakn kwa hii miaka haipo na hata ukiwauliza vijana wenye miaka 40 waliozaliwa hiyo kanda hata hawaijui hicho kitu, kilichonifanya nijue kuwa umehadithiwa ni ile neno lenyewe ulivyo liandika "Sagulaga" hilo neno halipo, rudi wakuhadithie upya ndo uje uwadanganye members
..ndugu yangu "RADI DUME"...Wasukuma tunanyanyasika sana na maneno kila kukicha tunasemwa...washamba,tuna magovi,yaani maneno chungu nzima...kisa MShamba ndiyo kashika nchi na Kashika wallet na ujinga ujinga hataki?...Mbona kuna wala punda humu wengi,wala mbwa wengi,wakata visimi mpo na mtuambie cjui huwa mnaenda kuchoma mshikaki....lakini tunanyamaza kwa sababu tunaheshimu kila mtu...watuache kila mtu na mila zake ila hiyo hatuijui
 
Mila number moja kandamizi kisaiokolijia ni ile mwanamke akitumwa kuleta maji ya kunywa ,anatakiwa apige magoti mpaka huyo mtu anaekunywa maji amalize,nyingine mwanamke mbele ya mwanaume ni mdogo hata kama mwanaume ni mdogo kiumri,mwanamke anatakiwa apige magoti anapomsalimia mwanaume kwa mfano mdogo wake wa kiume,always unapiga magoti unapomsalimia mdogo wako wa kiume na anakuambia Ng'waguku,binafsi mimi hii siikubali kabisa na kamwe simpigii magoti mdogo wangu wa kiume.Mila nyingine mbaya kandamizi ni ile ukiolewa ukweni wewe ndo utakuwa kama house girl,na ukiamka asubuhi unapomsalimia mkwe unapiga goti mpaka jini unaganda hapo mpaka salaam ziishe,moja ya sababu iliyonifanya nisiolewe usukumani.
Hahaaaaa,umenifurahishaaaaa,ng'waghuku ilumbhuye.
 
Wewe mtoto acha chuki na wasukuma chagulaga natogagwa ilikuwa miaka 70 mpaka 87 ikaisha kabisa na kuzurula kwangu mikoa ya kanda ya ziwa sijawahi kuiona tena sasa wewe umesimuliwa tu ukaja kupost humu na hizi chuki na wasukuma zimeanza tu mara baada ya MAGUFULI kuwa Rais ni kwanini? Au kwa kuwa wako wengi
..Wanatusema mno roho zao zimejaa sumu........sasa wameungana yaani tunasemwa asubuhi mpaka usiku...mfano huku niliko nilikuwa natambulika kwa jina langu vzr tu...saiv wamenigeuka naitwa Msukuma yaani utadhani sina jina
 
Wewe inavyoonesha umesimuliwa tu halafu unakurupuka kuja kuleta hiyo thread, hiyo mila ilikuwepo miaka ya 1960's, lakn kwa hii miaka haipo na hata ukiwauliza vijana wenye miaka 40 waliozaliwa hiyo kanda hata hawaijui hicho kitu, kilichonifanya nijue kuwa umehadithiwa ni ile neno lenyewe ulivyo liandika "Sagulaga" hilo neno halipo, rudi wakuhadithie upya ndo uje uwadanganye members
Nakuona radiii,hivi vitu bana nishidaaa,ilikuwa wale wanawake wenye viburi na nyodo akizingirwa atalia mpaka macho yamkauke mpaka achague tuu
 
Wanasiasa waliwaongoza watanzania kupitia bungeni na nje ya Bunge kupinga kwa nguvu zote mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hasa wasichana. Taasisi, Mashirika yasiyo ya serikali, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za dini, watu binafsi walishiriki kwenye vita hii dhidi ya ukeketaji.

Lakini kwa wasukuma kuna mila yao maarufu kwa jina na "sagulaga" ambayo kwa hali yoyote ile ni ukatili lakini pia ni udhalilishaji dhidi ya wanawake. Binti mdogo labda chini ya miaka 14 anafukuziwa na kuzingirwa na wavulana na wakati mwingine na hata vijana wa umri wa miaka 35 mara nyingi akiwa anatokea ngomani na kutakiwa kuchagua mmojawapo ili afanye naye mapenzi.

Cha ajabu ni kwamba binti huyo kwa siku mmoja hutakiwa kwa nyakati tofauti kuchagua mtu zaidi ya mmoja na kufanya naye mapenzi na wakati mwingine huku vijana wanaosubiri "zamu yao" ifike wakisubiria pembeni wakitizama. Si lazima vijana hawa wamuoe binti anayelazimika kuchagua wa kuwa naye kwa siku hiyo!

Jee huu si ubakaji wa ki-kikundi (a Gang rape)? Mabinti hawa wanaolazimika kuishi kwenye mila hii ya kionezi utu wao unaheshimiwa kweli. Tofauti iko wapi kati ya kukeketa na chagulaga? Jee ni mwanasiasa gani ambaye atasimama na kuanzisha harakati za kuitokomeza mila hii Potofu na ya kiudhalilishaji kama ilivyokuwa kwa harakati za kutokomeza ukeketaji nchini mwetu?
Sijaona wala kusikia mambo ya Chagulaga bali huwa nasimuliwa tu. Enzi hizi kweli mtoto wa kike azingirwe mubashara na kulazimishwa kufanya mapenzi? Na UKIMWI wote huu? Na sheria zote hizi za kumlinda? Gang rape? Laivu Usukumani?

Nadhani lengo lako ni kuwachafua Wasukuma. Nakushauri utafute kitu kingine chenye uhalisia. Au unaweza kuongelea ushamba wetu lakini siyo kuzusha mambo yaliyotokomezwa zaidi ya miaka 40 iliyopita!
 
Wasukuma pamoja na kuachana na hiyo mila,lakini naamini mnapokutana kwenye matambiko yenu kuwakumbuka mizimu ya kale lazima mtacheza sagulaga. Safi sana ngosha
 
Niliwahi kuishuhudia hii kule Igunga. Ila mila nyingine za makabila yetu hmmmm! miaka hiyo zilionekana bomba siku hizi zitaonekana ni udhalilishaji wa wanawake.
BAK una miaka mingapi mkuu? Hii mimi nimesimuliwa na wajomba na wako in their 70s na wenyewe ndo walishiriki laivu. Kuna watu wazima sana humu JF eeeh!
 
Hujaelewa yaani unaganda chini mpaka mmalize salaam,na salaam ya kisukuma kwa mkwe ni ndefu,kwani kuna ubaya gani kumsalimia mkwe Nikiwa nimesimama ?and why only mtoto wa kike ndo apige goti ?why mwanaume anapomsalimia mkwe wake,hapigi magoti ?

ulishawahi kujiuliza kwa nini wanafunzi wa Yesu wote walikuwa wanaume?
 
Kwanza,unapoiongelea chagulaga(magoye),purely unakuwa unaiongelea mikoa ya shinyanga na tabora kwa kipindi hicho.hii nikiwa na mana ya wilaya za kazikazini mwa mkoa wa tabora mostly igungana na nzega na hiyo shinyanga yote.

Tamaduni hii ya chagulaga(magoye=kamba),ilikua sana maeneo haya sababu ya ngoma za asili(beni,phubha na nyinginezo).pia mtoto wakike kipindi hicho hakuzingira tu ngomani bali hata kama ameenda kuteka maji mtoni kundi la cijana waliweza kumvizia na kumzingira nakuanza kumdai hiyo chagulaga,hata akiwa ameenda mashineni aliweza pia kumbwa na hilo janga.

Kwa vile ilikuwa ni tamaduni mdada akichelewa kurusi home wazee waliweza kujua kuwa binti amekatwa magoye,hivyo waliweza kutuma hata vijana kwenda kunusueu ile hali.pia wengine waliweza kunusurika kufanyishqa hayo mapenzi ya chagulaga kama ikitokea kwenye lile kundi la wanaume kuna kijana labda inakaa nae kijiji kimoja au jirani,waliweza kuwachagua ili akafanye naw sex then wanafanya kama wanaendabkufanya mambo afu wanaunganisha home.

Sifa moja ya chagula mayu ilikuwa ,ukishamchagua tu mwanaume kesi imeisha wanasambaa kwenda kwenye makundi mengine afu we unaenda na kusex na huyo mwanaume ulie mchagua.

Kilichopelekea chagulaga kupigwa marufuku ni baada ya UKIMWI kuingia ichini.serikali iliweza kupambana vikali sana kuhakikisha mila inatokomezwa.Kabla ya kuingia ukimwi serikali ilijaribu kuzuia hii mila but nguvu ilikuwa ni ndogo sana hivyo iliendelea tu kwa maeneo ya ndanindani.

Hii mila kuizuia ilkuqa ni shughuli pevu mpaka kuna wakati serikali ilitumia jeshi,hii ni kuwa baadaya ngoma kuisha na wanawake kuanza fukwa chagulaga,wanajeshi walikuwa wakivamia hayo makundi ya wnaume na kuchezea mikanga ya jeshi sana na kubebwa kwenye hayo magari ya jeshi na kupelekwa mjini.

Hivyo kusema kuwa hii mila bado ipo sio kweli,ni mda sana isha kufaaa,labda kama mleta hoja anakitu kingine kuhusu wasukuma.
NOTE:Mzaliwa wa shinyanga na tabora wa kipindi hicho ndo anaiilewa vizuri chagulaga kuliko mzaliwa wa mwanza,sababu hizo sehemu ndo zilikuwa kiini cha hiyo mila.
 
Wanasiasa waliwaongoza watanzania kupitia bungeni na nje ya Bunge kupinga kwa nguvu zote mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hasa wasichana. Taasisi, Mashirika yasiyo ya serikali, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za dini, watu binafsi walishiriki kwenye vita hii dhidi ya ukeketaji.



Cha ajabu ni kwamba binti huyo kwa siku mmoja hutakiwa kwa nyakati tofauti kuchagua mtu zaidi ya mmoja na kufanya naye mapenzi na wakati mwingine huku vijana wanaosubiri "zamu yao" ifike wakisubiria pembeni wakitizama. Si lazima vijana hawa wamuoe binti anayelazimika kuchagua wa kuwa naye kwa siku hiyo!

Jee huu si ubakaji wa ki-kikundi (a Gang rape)? Mabinti hawa wanaolazimika kuishi kwenye mila hii ya kionezi utu wao unaheshimiwa kweli. Tofauti iko wapi kati ya kukeketa na chagulaga? Jee ni mwanasiasa gani ambaye atasimama na kuanzisha harakati za kuitokomeza mila hii Potofu na ya kiudhalilishaji kama ilivyokuwa kwa harakati za kutokomeza ukeketaji nchini mwetu?


Naomba uwe specific hii habari wewe uliikuta lini na sehemu gani.

Halafu hapo kweney nyeusi ni uwongo mtupu!. Wale watu walikuwa wanaheshimiana sana. Akichaguliwa mmoja wao, wwengine huondoka na kwenda kutafuta mwingine. Lengo halikuwa kulala na wasichana hapo hapo. Ilikuwa ni mfumo wa kuanzisha mahusiano, wataongea, wataongozana msichana atasindikizwa kwao na wakielewana walikuwa wanaoana.

Usuukumani kubaka lilikuwa ni kosa la jinai. Mbakaji alikuwa anapewa adhabu kali na wengine walikuwa wakiuawa. Unataka kkusema nini? Huyo mtu anakaka zake. Dada yao abakwe, na watu wanafahamika, kitakachotokea dunia intasimulia. Salama ya wabakaji ilikuwa ni pale habari zikifika kwa viongozi ambapo mbakaji alikuwa akiadhibiwa na kuonywa kutokurudia upumbavu.

Mara nyingi wazazi wa vijana walikuwa wakiona vijana wao hawajatulia, walikuwa wakiwaoza mapema ili kuondokana na fedheha za kubaka au kuwapa watto wa watu mimba bila taratibu.

Ninaifahamu sana hii ihistoria ya mila za usukumani. Sema lingine na uache kuwalilnganisha na watu wa musoma na tabia zao za ukatili kwa wanawake na ukeketaji. \usukuma hawana haya mambo ya ukeketa.
 
Back
Top Bottom