Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,410
- 38,702
Wanasiasa waliwaongoza watanzania kupitia bungeni na nje ya Bunge kupinga kwa nguvu zote mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake hasa wasichana. Taasisi, Mashirika yasiyo ya serikali, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za dini, watu binafsi walishiriki kwenye vita hii dhidi ya ukeketaji.
Lakini kwa wasukuma kuna mila yao maarufu kwa jina na "sagulaga" ambayo kwa hali yoyote ile ni ukatili lakini pia ni udhalilishaji dhidi ya wanawake. Binti mdogo labda chini ya miaka 14 anafukuziwa na kuzingirwa na wavulana na wakati mwingine na hata vijana wa umri wa miaka 35 mara nyingi akiwa anatokea ngomani na kutakiwa kuchagua mmojawapo ili afanye naye mapenzi.
Cha ajabu ni kwamba binti huyo kwa siku mmoja hutakiwa kwa nyakati tofauti kuchagua mtu zaidi ya mmoja na kufanya naye mapenzi na wakati mwingine huku vijana wanaosubiri "zamu yao" ifike wakisubiria pembeni wakitizama. Si lazima vijana hawa wamuoe binti anayelazimika kuchagua wa kuwa naye kwa siku hiyo!
Jee huu si ubakaji wa ki-kikundi (a Gang rape)? Mabinti hawa wanaolazimika kuishi kwenye mila hii ya kionezi utu wao unaheshimiwa kweli. Tofauti iko wapi kati ya kukeketa na chagulaga? Jee ni mwanasiasa gani ambaye atasimama na kuanzisha harakati za kuitokomeza mila hii Potofu na ya kiudhalilishaji kama ilivyokuwa kwa harakati za kutokomeza ukeketaji nchini mwetu?