Rafiki kwakua umeomba ushauri basi nitakupatia kama ifuatavyo:
1. Mdada wa kwanza anafaa kabisa kuoa kwani ugonjwa huo unatibika, hata kama itashindikana kupona unatakiwa kuwa rafiki wa pampasi au nepi, vinginevyo uwe unalala kidogo na kushituka ili umpeleke kukojoa kila wakati. ikitokea kasafiri mpe pampasi au umshonee chupi yenye karatasi kwa ndani ili mkojo usivuje.
2. Mdada wa pili hakika atakuumiza kichwa maana uongo huwa hauna tiba, hata hivyo uongo huleta mafarakano, huvunja mahusiano baina ya ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla.
3. Mdada wa tatu ni mzuri kwani ugonjwa wake unaweza kutibika, ila kwakua ni wa wastani hivyo anazidiwa na yule kikojozi, hata hivyo harufu ya mdomo+kwapa utakosa raha kabisaa hasa wakati wa chakula cha wanandoa.
Naomba uoe kikojozi ndugu yangu mambo yote yatakaa vizuri.