Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerer ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hauyuko hai. mawazi ya Nyerere ya wakiti nhuo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi, ;lakini leo hii yanakublika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru ma kujitegemea.
Wewe kweli Kichuguu👍👍👍, ila, siyo kweli kwamba wanafalsafa wanaendelea kuishi hata kama wamekufa? Mawazo yao yanaendelea kusaidia vizazi na vizazi?
 
Nobel hutolewa kwa mtu aliye hai tu. Leo hii Nyerere ana vigezo vya kuipata lakini anakosa sifa kwa vile hayuko hai. Mawazo ya Nyerere ya wakati huo yalikuwa hayakubaili nchi za Magharabi; lakini leo hii yanakubalika wakati yeye mwenyewe hayupo kuyazungumzia. Hasa hili swala la uhuru na kujitegemea!
Ila pia, sina hakika kama Tuzo hii ni ya nchi za Magharibi au ya jumuiya za kimataifa, Alfred B. Nobel ni Mswedish ambayo ni nchi iliyokuwa rafiki wa Tz wakati huo wa mawazo hayo ya Mwl Nyerere yaliyopingwa na Magharibi yalipokuwa yakitoka.

“Having come into contact with a civilization which has over-emphasized the freedom of the inpidual, we are in fact faced with one of the big problems of Africa in the modern world. Our problem is just this: how to get the benefits of European society – benefits that have been brought about by an organization based upon the inpidual — and yet retain African’s own structure of society in which the inpidual is a member of a kind of fellowship.”

Julius Kambarage Nyerere as quoted in the New York Times Magazine on 27 March 1960. -
 
Umenikumbusha wakati anakabidhiwa nchi na mzee ruksa,Hali ilikuwa mbaya sana.lakini Big Beni akafanya Mambo makubwa
1.kuanzisha TRA
2.shetia ya TISS 1996
3.ete,etc
Alitofautiana na Mwl kimantiki. Mwl aliamini maskini kusaidiwa, Big Ben aliamini maskini kutosubiri mana adondoshewe (toka kwenye hazina za serikali au mtu binafsi) bali anayeweka bidii ya kujikwamua akipewa mana katika sura ya sera na sheria, aliamini maskini wa kweli ni aliyenyimwa uwezo wakati wa uumbaji e.g. mwenye mtindio wa ubongo na ulemavu mwingine unaompunguzia thamani ya ubinadamu wake kwa asilimia kubwa sana. Huyo ndiye Big Ben wa Brisbane, Big Ben wa Gleneagles, Big Ben wa Malta, Big Ben wa Doha, Big Ben wa New york (Baraza kuu la Umoja wa mataifa). Mwanzoni kwenye uongozi wake, akihutubia mikutano na makongamano ya kimataifa, wazungu wa Magharibi walidhani hana jipya na walipoteza hamu ya kumsikiliza wakifikiri ni sura B ya Mwl Mjamaa. Baadaye wakaja kukubali kwamba "Don't judge a book by its cover title"

Jitihada za Big Ben na wenzake wengine kama Mh. Thabo Mbeki, Mh. Meles Zenawi, Mh. Olusegun Obasanjo, Mh. Abdelaziz Bouteflika na wengineo wenye nguvu kama za hawa zilisaidia kuundwa kwa tume ya Afrika ya Mh. Tonny Blair Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, tume ambayo pamoja na mambo mengine ilishughulikia suala la mzigo wa madeni ya Afrika na uwezekano wa misaada zaidi kupatikana, tume ambayo ilikuwa ni muhimu sana kwa wakati huo baada ya ule mpango wa muda mrefu wa HIPC kusuasua katika kutimiza malengo yake.

Big Ben aliona suala ambalo wengi hawakuliona au walidhani lisingeweza kuzaa matunda; lile la ni kwa vipi dunia ya tatu ingesimama na kutekeleza malengo ya MDG ya Umoja wa Mataifa bila ya kuziwezesha nchi hizi za dunia ya tatu? Alipambana na kupata kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa baada ya kazi kubwa ya ushawishi akishirikiana na viongozi wenzake hao ambao uwezo na nafasi zao za ushawishi ni mkubwa pia, lengo likiwa ni kuhakikisha nguvu ya pamoja inatumika katika kufikia matarajio.

Big Ben siku zote alipopata dondoo (wazo), hakuibahilia na kuifanya mali-akili yake binafsi (personal intellectual property), isipokuwa aliamini kusema kwa nguvu moja na sauti moja kama wana wa Afrika hivyo alilazimika kushirikiana na viongozi wenzake wa Afrika dondoo hiyo ambayo wangeijenga na baadaye kuipeleka katika ulingo wa kimataifa wakiwa wamoja. Ninamwona kama kiongozi aliyeabudu umoja badala ya ubinafsi. Kwake mafanikio yaliyotokana na yeye aliyafanya kuwa ya umma mzima.
 
Back
Top Bottom