Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Hio pisi ni pisi kweli mkuu...wala huongopi..

Dada yangu alikwama kwenye hilo kanisa,hata umwambie nini haelewi.kila saa biashara yake imefungwa tena ile mida ya biashara. Mara mikesha mara misa za jioni..michango lukuki mpaka nikaona sasa anapotea na sina la kufanya.

Nashukuru sasa hivi amefanikiwa kuchomoka.

Nahisi pia nguvu za giza hutumika humo.



Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
Kuna msichana mmoja anafanya kazi dukani kwangu. Lile duka liko mbali kidogo na lingine ambalo mara nyingi nakuwepo kumbe yule manzi kuna muda anafunga na kwenda kanisani mchana. Nilipojua nikamwambia achague kwenda kanisani au kufanya kazi na jibu nataka sasa hivi ili kama vipi tuachane kiroho safi. Naona hakuwa amezama sana akaamua kubaki kazini na upuuzi kaacha. Haya makanisa yana mchango mkubwa kwenye kuchochea umaskini.
 
Oooh! Pole sana mkuu. Ni vyema kama sister aliweza hatimaye kuponyoka maana huwa siyo kazi rahisi. Jamaa wana nguvu za ajabu!

Tukisema hapa watu wanasema pengine tuna chuki au tunawasema vibaya watumishi lakini ukiona sexual abuse, economic exploitation na psychological manipulation wanazopitia watu waliofanywa mazombie na hawa Biblical motivational
speakers wahuni mpaka unashangaa yaani. Imagine hao vijana wake wa muziki na logistics anaozunguka nao kwenye semina zake hizi za upigaji huwa hawalipi hata senti moja wakati wengine wameoa na wana familia. Anawaambia eti ni lazima wajitolee kwa ajili ya ufalme wakati yeye na mke wake wanaponda raha kwenye 5 Star hotels. Hata huruma kidogo hakuna. Juzi juzi hapa eti ndiyo anawapa one time pay ya 60K Tsh kila mmoja as a courtesy. Imagine vijana wadogo wameacha mishe zao zote za kujiendeleza kimaisha wanahangaika bure. Yaani wake zao ndiyo wanahangaika kuendesha familia huku waume zao wanajitolea kuzunguka na Baba Mchungaji bure huku Baba Mchungaji mwenyewe anapiga mpunga mrefu. Mpaka wanapopigika sana na kuwa disillusioned ndiyo baadhi yao wanachomoka wakiwa depressed na hawajui hata pa kuanzia tena! Inhumane!
Kuna wakati flani kwenye maisha yangu ya dhambi nilienda kwa mganga mida ya asubuhi sasa nikakuta mganga kama kachoka sana. Kumuuliza ndo akasema usiku mzima alikesha anahudumia wachungaji.
 
Nani anamfahamu vizuri pastor Tony kapola.

Kanisa lake liko wapi ?
Nilisikia liko morogoro kutwa yupo Dar,dodoma

Kwanini waumini wake na mke wanavaa nguo za ovyo ?

Inakuaje ameungana na hawa manabii wa uongo matapeli wa zimbabwe ?
ni wale wale tu. ukiona kuna nabii au mchungaji anahubiri hekima ya kibinadamu, huyo sio mchungaji, ni motivational speaker na asemacho hakitoki kwa Mungu. chochote cha kimwili hakiokoi roho. kama akili au hekima ya kidunia ingekuwa na uwezo kuokoa maprofessa na wasomi wengi wasingeenda church, na wachungaji wangekuwa ni wale tu waliosomea saikolojia kama kina chriss mauki n.k, na hao wanasaikolojia wasingekuwa na umuhimu wa kwenda church kwasababu saikolojia na elimu ya kimwili wanayo. ni kwa nguvu za Roho Mtakatifu pekee hata kwa tone moja tu mtu anaweza kubadilika, mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu na anayeongea under the influence ya Roho Mtakatifu hata kwa kauli ya neno moja tu inapasua miamba ndani ya mioyo ya watu na wanabadilika ghafla. hao vijana wengi wanaotoa mahubiri ya sukari na wanaoongea kwa namna ya mwili ni wapiga pesa tu. wao wote pamoja na baba yao nabii.
 
Unaweza kunitajia manabii wa ukweli?
Manabii na mitume wa ukweli waliishia pale Bible ilipofika mwisho wa kuandikwa the rest ni wezi,matapeli,wahuni,wenye tamaa ya vitu vya dunia taja na mengine unayoyajua wewe.

Watu wanafanyiwa maigizo hawaelewi,Mungu alikuwa hana sababu ya kuweka mlemavu kama siyo kwa ajili ya kuwajaribu wale aliowapa viungo vyote,mf,kipofu yupo ili mimi mwenye macho yanayoona vizuri nimsaidie kula pale asipoweza kutafuta kula yake kama mimi au nimsaidie pale anapohangaika kufanya kitu eg;kuvuka barabara au kumuepusha na mashimo na kupitia haya napata thwawabu nisipofanya haya napata dhambi lakini anatokea kijana mmoja mvaa suit na mawani ya jua kwa sababu anajua kucheza na maandiko anamleta kwenye banda lake la mabati mtu anaefanana na huyu akiwa tayari ameshampanga namna ya ku-act na kusema "nguvu zake za kinabii zimempa uoni" watu na akili zao wanashangilia wanaenda kutoa shukrani ya hela wakidhani ni kweli.

Yaani watu wanapingana na jinsi Mungu alivyoipanga dunia,maskini Mungu amewaweka ili dunia iwe balanced na kupitia wao watu wafike kwake ila waokota sadaka so called prophet wanaita umaskini ni laana huku wakiwaambia hao maskini wawape sadaka (na hao maskini wanatoa hawajui kama hao wanaowaita walaaniwa ilibidi wapokee kutoka kwao).

Wengine wanafikia hatua ku-act kufufua maiti,Mungu mwenyewe alimuonyesha mwanadamu pale alipokaa katikati yake akijifanya mtu kupitia Yesu kwamba baada ya mishe zote duniani kuna kifo lakini leo mtu anasema amefufua mfu huyu ni nani anapingana na Mungu?wakipewa homework waende Muhimbili au Ocean Road kwenye wagonjwa wa ukweli wanaingilia huku wanatokea huku mbona huko hawathubutu kwenda kuonyesha unabii wao?


Mtaibiwa sana.
 
huyu shetani anakoelekea sasa ni mbali, anaona kama watanzania ni wajinga anaweza kuwafanya chochote. ifike mahali sasa kama nchi tusema enough is enough.
 
Akiangalia mavazi atasali mwenyew na mke wake then nani atalipa bills za kuendesha kanisa
 
huyu shetani anakoelekea sasa ni mbali, anaona kama watanzania ni wajinga anaweza kuwafanya chochote. ifike mahali sasa kama nchi tusema enough is enough.
Nchi haina kipimo Cha kupima usahili wa Imani,Imani ni jambo binafsi
 
Hapana asee, kwa mwakasege nitapinga mpaka dakika ya mwisho, yule mzee naanza kumfahamu tangu anahubiri pale kwenye kiwanja cha shule ya Arusha meru secondary, baadae akahamia pale relini

Tafuta mfano mwingine hata wakina mzee wa upako lusekelo 😆🍺🍻
Ya sirini yaache yalivyo utaelewa kwann sedekia alitangulia
 
Manabii na mitume wa ukweli waliishia pale Bible ilipofika mwisho wa kuandikwa the rest ni wezi,matapeli,wahuni,wenye tamaa ya vitu vya dunia taja na mengine unayoyajua wewe.

Watu wanafanyiwa maigizo hawaelewi,Mungu alikuwa hana sababu ya kuweka mlemavu kama siyo kwa ajili ya kuwajaribu wale aliowapa viungo vyote,mf,kipofu yupo ili mimi mwenye macho yanayoona vizuri nimsaidie kula pale asipoweza kutafuta kula yake kama mimi au nimsaidie pale anapohangaika kufanya kitu eg;kuvuka barabara au kumuepusha na mashimo lakini anatokea kijana mmoja mvaa suit na mawani ya jua kwa sababu anajua kucheza na maandiko anamleta kwenye banda lake la mabati mtu kama huyu na kusema "nguvu zake za kinabii zimempa uoni" watu na akili zao wanashangilia.

Yaani watu wanapingana na jinsi Mungu alivyoipanga dunia,maskini Mungu amewaweka ili dunia iwe balanced na kupitia wao watu wafike kwake ila waokota sadaka so called prophet wanaita umaskini ni laana huku wakiwaambia hao maskini wawape sadaka (na wao maskini wanatoa hawajui kama hao wanaowaita walaaniwa ilibidi wapokee kutoka kwao).

Wengine wanafikia hatua ku-act kufufua maiti,Mungu mwenyewe alimuonyesha mwanadamu pale alipokaa katikati yake akijifanya mtu kupitia Yesu kwamba baada ya mishe zote duniani kuna kifo lakini leo mtu anasema amefufua mfu huyu ni nani anapingana na Mungu?wakipewa homework waende Muhimbili au Ocean Road kwenye wagonjwa wa ukweli wanaingilia huku wanatokea huku mbona huko hawathubutu kwenda kuonyesha unabii wao?


Mtaibiwa sana.
Kila penye feki original ipo.
Mitume na manabii wa kweli wapo wengi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom