Nani anafahamu iliko hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anafahamu iliko hii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiresua, Feb 2, 2011.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF,

  Mwaka 2006 niliwahi kusikia Mh Rais, JK akitoa hotuba kwa Watanzania akilizunmzia sakata la Richmond. Alieleza kinagaubaga Richmond ni nini, na ni kwa nini walishindwa kuzalisha umeme waliotarajiwa kuuzalisha, alitoa hotuba ndefu kwelikweli kuhusu Richmond,

  Sasa kwa yeyote amabeye aliisikia na pengine anayo, au pia anaweza kututafutia hotuba hii naomba atupatie aiweke pa jamvini ili iweze kujadiliwa.

  Hotuba hii kwa kipindi sikuwahi kuisikia ikijadiliwa au kuhojiwa mahali popote, kwani Mh Raisi alitamka maneno ya kuihalalisha Richmond na kwa ushahidi huu unaonyesha kivuli cha mzimu wa Richmond na hatimaye Dowans kuwa ni nani aliyenyuma ya hili sakata, na je kama unampa uhalali wa kukwepa kuhusika na sakata hili!!!

  nawasilisha
   
 2. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF,

  Mwaka 2006 niliwahi kumsikia Mh Rais, JK akitoa hotuba kwa Watanzania akilizungumzia sakata la Richmond. Alieleza kinagaubaga Richmond ni nini, na ni kwa nini walishindwa kuzalisha umeme waliotarajiwa kuuzalisha, alitoa hotuba ndefu kwelikweli kuhusu Richmond (akiamanisha watanzania kuikubali kampuni feki)

  Sasa kwa yeyote ambaye aliisikia na pengine anayo, au kama anaweza kututafutia hotuba hii naomba atupatie aiweke hapa jamvini ili iweze kujadiliwa.

  Hotuba hii kwa kipindi sikuwahi kuisikia ikijadiliwa au kuhojiwa mahali popote, kwani Mh Raisi alitamka maneno ya kuihalalisha Richmond na kwa ushahidi huu unaonyesha kivuli cha mzimu wa Richmond na hatimaye Dowans kuwa ni nani aliyenyuma ya hili sakata, na je kama unampa uhalali wa kukwepa kuhusika na sakata hili!!!

  nawasilisha
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Nipo nawe mkuu....jambo lolote likiibuka kwenye kaya na mkuu wa kaya kakaa kimya,litasababisha wakuu wa boma za jirani kubaini na mengine wasiyostahili...Kinachosababisha wengi tumbebeshe zigo hili zito Mr President ni ukimya wake! Doawans si mwana haramu hivyo hata mkuu wa kaya akitulia kimya Mwana huyu hawezi mpita kwa kua yeye km si mzazi basi amemlea na ni dhahiri anajua ujira wake kumlea mwana huyu!
   
Loading...