Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,231
- 111,238
MImi hoja yangu ni kwamba kwann Mwakyembe hakusimamia kwenye kitu anachokiamini na kuwa mnafiki kama kinyonga?Lowasa shutuma zake ni hayo mambo yaliyotokea,ila kwa sasa namsapoti yeye ni mtekelezaji mzuri,sioni CCM mtu nayeweza kumwamini tena zaidi ya LOwasa,sio kwamba nilikua namfagilia Lowasa,ila siku zinavyokwenda naanza kuchambua anayefaa na asiiyefaa
Mkuu kuna uwezekano huwajui vizuri CCM na kama unawajua utakuwa unazifumbia macho sera zao za namna ya kuongoza...
Mosi, kiongozi yoyote wa kitaifa ambaye ni mwanachama wa CCM hutakiwa kuweka kwanza maslahi ya chama, halafu yanafuata maslahi binafsi na mwisho kabisa ndio huja maslahi ya nchi...
Sababu kubwa ya utaratibu huo ni kutokana na madudu ambayo tayari yalishafanyika huko nyuma kiasi kwamba ni ngumu kufanya safisha safisha maana itamgusa kila mtu, hata wale waliopata kuaminiwa na Watanzania...
Asikudanganye mtu, CCM haina mtu aliye msafi hata mmoja isipokuwa ina watu wenye uafadhali machoni pa Watanzania na hata watu hao wakipewa madaraka hakuna jipya litalotokea...
Ndio maana Mwl. Nyerere hakukosea kwa kutamka kuwa upinzani/mpinzani wa kweli ni shurti atokee CCM, hebu jiulize kwa nini hakutamka kuwa mkombozi wa kweli shurti atokee CCM?