Nani ameshawahi kufanya hii kitu?

Nani ameshawahi kufanya hii kitu?

Ambaye ameshawahi kujaza jino lililotoboka, kitaalam wanaita ROOT CANAL naomba anipe uzoefu. Mimi niliwahi kusafisha tu jino la huku mwisho yanaitwa magego 2016 ila sikurudi kulijaza mpaka leo. Sasa linauma hatari mpaka kutafunia kitu haiwezekani tena.
What I know root canal siyo kujaza jino. Ila ni kudisconnect nervous system zinazoingia kwenye jino ili usiwe unapata maumivu...
 
Ambaye ameshawahi kujaza jino lililotoboka, kitaalam wanaita ROOT CANAL naomba anipe uzoefu. Mimi niliwahi kusafisha tu jino la huku mwisho yanaitwa magego 2016 ila sikurudi kulijaza mpaka leo. Sasa linauma hatari mpaka kutafunia kitu haiwezekani tena.

Nishawahi kufanya vyote zaidi ya mara moja kifupi bongo hakuna wataalam wa huduma hizo.. dr anatakiwa akuchunguze jino zaidi ya mwezi kwanza before hajaanza tiba lakini hapa bongo dr siku hiyo hiyo anakuchunguza anakuingiza ma vyuma kinywani anakusafisha anakuziba kwa risasi au kukata mishipa ( root canal) ..wanaleta mzaha na very sensitive part of the body..just toa tu jino bovu otherwise utakua tu mtumwa wa maumivu
 
Afadhali maana nilifikiri ni wale wanafunzi wa Rembo wa Muhimbili ningesema unatuongopea
sitasahau balaa la pale, licha ya mbwembwe nyingi za kuibiana pesa sijui x- Ray mara nini
Bora pale Tandika hawana mbwembwe lakini wanajua kazi.

Unamaanisha kwamba Muhimbili hawapo competent, ni waswahili wanaiba pesa hawana huduma nzuri?
Kwamba wanawaachia wanafunzi kufanya root canal?
 
Nishawahi kufanya vyote zaidi ya mara moja kifupi bongo hakuna wataalam wa huduma hizo.. dr anatakiwa akuchunguze jino zaidi ya mwezi kwanza before hajaanza tiba lakini hapa bongo dr siku hiyo hiyo anakuchunguza anakuingiza ma vyuma kinywani anakusafisha anakuziba kwa risasi au kukata mishipa ( root canal) ..wanaleta mzaha na very sensitive part of the body..just toa tu jino bovu otherwise utakua tu mtumwa wa maumivu

Mimi sipendi kupata mapengo!!
Halafu gego la mwisho kabisa kushoto ndio linaniuma... Sasa nikitoa nitakua natafunaje nyama!!
 
Afadhali maana nilifikiri ni wale wanafunzi wa Rembo wa Muhimbili ningesema unatuongopea
sitasahau balaa la pale, licha ya mbwembwe nyingi za kuibiana pesa sijui x- Ray mara nini
Bora pale Tandika hawana mbwembwe lakini wanajua kazi.

Tandika clinic gani niende kesho.
Juzi nimeenda Ekenywa pale magomen lakin sijaridhika kwa kweli, jinsi nilivomuona yule mng'oa majino alivo.
 
Tandika clinic gani niende kesho.
Juzi nimeenda Ekenywa pale magomen lakin sijaridhika kwa kweli, jinsi nilivomuona yule mng'oa majino alivo.

Kwa matatizo ya meno Nenda kwa Dr Akim pale Samora National Housing.. ni ghali kidogo yule mangi ila one of the best in town!
 
Pia ni kuwa muangalifu wa baadhi ya dawa za meno,mfano ni dawa ya Smokers.Inatoboa meno makuu.

Colgate Original inasaidia kurudisha jino kama lilianza dalili za kutoboka.

Na kuna zile zinauzwa na watu wa network marketing e.i forever living ni balaa


Chopstick from Hong Kong
 
Kwa matatizo ya meno Nenda kwa Dr Akim pale Samora National Housing.. ni ghali kidogo yule mangi ila one of the best in town!

Zamora National Housing... ni posta mjini?
Ana zahanati yake binafsi ama...
How much is he expensive.
Maana hapa nilipo nina Bima na pia naweza kutoa maximum 50,000 cash nipate huduma nzuri.
Nielekeze hiyo Samora Housing location yake kama natokea shekilango
 
Wakuu
ROOT CANAL AU ENDODONTIC TREAMENT ni matibabu kwa ajili ya kutibu kiini au mzizi wa jino.....
Haya matibabu yanatolewa pale ambapo jino limetoboka mpaka kufikia kiini cha jino
Au jino limevunjika au vinginevyo
Daktari anapaswa kukuchoma sindano ya ganzi na kuhakikisha hutasikia maumivu ndipo ataananza kudrill jino
Dhumuni la Haya matibabu ni kuondoa sehemu ya ndani ya jino.... Hii ikiwa ni mishipa ya fahamu na damu(kuliuwa jino)...... Sasa kutegemea na aina ya jino,hali ya mfupa...... Usafishaji Unaweza kufanywa kwa siku moja hadi tatu....
Mfano... Kama kuna usaha kwenye mfupa, Usafishaji utaendelea mpaka pale maumivu yatakapoisha
Mara nyingi meno ya mbele yanafanyiwa root canal na kuzibwa siku hiyo hiyo.... Ukichunguza Haya meno yana mzizi mmoja
Hivyo nirahisi kusafisha tofauti na magego yenye mizizi miwili hadi minne
ANGALIZO
Inashauriwa kumwona dentist walau kila baada ya miezi 6...ili uweze kutunza tabasamu lako.... Usikubali jino litoboke mpaka likazibwe.....
Hata likitoboka...lisifike stage ya root canal.....yani lipiganie lisifike kungolewa.
Pia si kweli meno yanatobolewa na wadudu hivyo jino moja likitoboka halitaambukiza jino jingine. Bali ukitibu jino bovu utapunguza maeneo yanayokusanya mabaki ya chakula(haya ndio hutumiwa na bakiteria kutengeneza acid inayotoboa meno)
Mwisho, usiache matibabu katikati kwani kuna watu wakiona maumivu yamepungua wanajua wamepona....
 
Tandika clinic gani niende kesho.
Juzi nimeenda Ekenywa pale magomen lakin sijaridhika kwa kweli, jinsi nilivomuona yule mng'oa majino alivo.
Ukifika Kituo cha polisi tu, fuata ule mtaa (barabara) yaani unapita Kati ya benki na Kituo cha polisi, nyoosha tu bila kumuuliza yeyote huko mbele upande wa kushoto utakiona hicho kijlhospitali bila kumuuliza yeyote.
 
Zamora National Housing... ni posta mjini?
Ana zahanati yake binafsi ama...
How much is he expensive.
Maana hapa nilipo nina Bima na pia naweza kutoa maximum 50,000 cash nipate huduma nzuri.
Nielekeze hiyo Samora Housing location yake kama natokea shekilango

Mbele kidogo ya TTCL kuna jengo la vioo jamaa ofisi yake ipo.kama sikosei ghorofa ya 6 au 7.. kajipanga sana yule jamaa ana vifaa na wasaidizi wengi last time nilitoa jino alitaka elfu 70 ila nilizungumza akashusha mpaka.50.. ila appointment muhimu unaweza kwenda ukakuta pamejaa ukakosa huduma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom