Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Kwa hiyo wewe unashauri boeing triple 7 itumike kwenye usafiri wa Dar Songea? Makubwa tena makubwa kabisa. Will you please refrain from giving advanced technical advise for something you dont know? Ningeshauri sana wewe na watanzania wengi wanaofungua thread za kijinga kila siku hapa kusemea technical issues za air aviation ambazo hawajui hata abc zake wakae kumya.
Hujaelewa mkuu ndio alietolea trip ya Dar to Songea ndege zingine za kutumia mafuta ya gharama kubwa lazima ziwe kubwa aina kama ya Boing 777. Hoja kubwa ni usahihi wa gharama hiyo ya matumizi ya mafuta
 
Maneno yako ya kweli lakini mleta hoja kasema kile walichosema wao sababu kuu kununua hii ndege ni ulaji wa mafuta ila kama angesema kuwa pia sisi hatuna viwanja vikubwa mikoani vya kupokea ndege kubwa au soko sio kubwa kiasi cha kununua ndege kubwa hilo linaeleweka kabisa lakini wao walichosema ni mafuta tu kwa hiyo mleta hoja ana haki ya kuuliza swali la msingi. Tz viwanja bado na maana ya viwanja sio tu majengo pia kila ukileta ndege kubwa lazima uwe na vitendea kazi vinavyoweza kumudu ndege kubwa kama fire trucks na uwepo wa mafuta ya kutosha. mimi nakubaliana hata hiyo ndege ya watu 75 si ajabu wasijaze.
Asante sana kwa kunielewa vizuri sana tena sana.
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.

EXACTLY NILICHOTAKA KUSEMA. MLETA MADA... KWELI KUNA ABIRIA 450 KWA MKUPUO KWENDA SONGEA ??? KWA VIWANDA NA UZALISHAJI GANI ULIOPO SONGEA.

ANYWAY, WATU WAACHE KU-GOOGLE MAMBO NA NADHANI HAYA MAMBO YAMEKAA KIUAALAMU ZAIDI HIVYO TUWAACHIE WENYEWE. TUWE NA KIPIMO KWENYE KUKOSOA.
 
Ngoja tukupe ufahamu. Na lazima mwelewe tu, maana hakuna jinsi:

• Dar - Songea abiria 75 = trip 1 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 2 mafuta ya TZS 1,000,000

• Dar - Songea abiria 75 = trip 3 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 4 mafuta ya TZS 1,000,000

• Dar - Songea abiria 75 = trip 5 mafuta ya TZS 1,000,000

• Songea - Dar abiria 75 = trip 6 mafuta ya TZS 1,000,000

Kwa hiyo;

Trip ni 6

TRIP abiria 75

Maana yake 75 × 6 = 450 passengers!!

Gharama ya mafuta kwa mujibu wa "Mtukufu" ni;

TZS 1,000,000 kwa safari moja

Safari (trip) ni 6

Kwa hiyo gharama ya mafuta ni;

TZS 1,000,000 × 6 = 6,000,000!!!

Hiyo ni Bombadia Mapanga shaa yenye capacity ya kubeba abiria 75 kwa safari moja!!

Je, Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria 450 kwa mpigo au safari moja?

At least LumumbaB7Bombadia wenzako wameshaelewa na wanakuja na ubishi ktk engo tofauti

Ingalau wenzako wanabisha kuwa, tatizo ni kuwa hakuna uwanja wa kutua Boeing 777 huko Songea lakini kwa ishu ya gharama maana yake wanakubali kuwa "Mtukufu" amedanganywa mchana kweupe!!

NB: Rudia tena kusoma uzi wa mleta mada utaelewa. Naamini hukusoma na kuelewa ndiyo maana umekuja na ubishi usio na kichwa wala miguu!!
Mkuu nikusahihishe kitu...sina chama na wala simtetei yeyote.ila nitasema kilicho cha ukweli. Wazo la kununua bombadier ni sahihi kwa kuangalia kwanza loading factor per leg na operational cost. wengi wa Wanaoponda ununuz wa zile ndege I can assure you ni vilaza wakubwa kwenye field ya usafiri wa anga. kwao cha muhimu ni kuona jet engine na ukubwa wa ndege tu..mengineyo kwao hawayahusu. nenda pale Nairobi uone KQ wamezipak 777 ngap on the ground...kisha mtafute Titus Naikun wa KQ umuulize maswali yako..ukirud humu utakuwa umewaelewa waliofanya uamuz wa kununua hiyo Q400
 
Mkuu nikusahihishe kitu...sina chama na wala simtetei yeyote.ila nitasema kilicho cha ukweli. Wazo la kununua bombadier ni sahihi kwa kuangalia kwanza loading factor per leg na operational cost. wengi wa Wanaoponda ununuz wa zile ndege I can assure you ni ****** wakubwa kwenye field ya usafiri wa anga. kwao cha muhimu ni kuona jet engine na ukubwa wa ndege tu..mengineyo kwao hawayahusu. nenda pale Nairobi uone KQ wamezipak 777 ngap on the ground...kisha mtafute Titus Naikun wa KQ umuulize maswali yako..ukirud humu utakuwa umewaelewa waliofanya uamuz wa kununua hiyo Q400

Hoja kuu ni gharama mkubwa!!

Kwamba, tripu moja ya Bomu ni sawa na abiria 75 tu na gharama kwa engo ya mafuta ni TZS 1,000,000

Lakini ukiwa na Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria 450 kwa mkupuo gharama ya fuel ni less than 6m TZS

Na ili Bomu asafirishe abiria 450 anahitaji kufanya tripu 6 ambazo cost ya mafuta pekee ni sawa TZS 6m kwa culculation za Magufuli!!

Tofauti yake ni nini hapo?

Hili halina ubishi. Labda tufikiri kuhusu factors zingine za kununuliwa kwa Bombadia badala ya jet engine flights mfano wa viwanja nk
 
EXACTLY NILICHOTAKA KUSEMA. MLETA MADA... KWELI KUNA ABIRIA 450 KWA MKUPUO KWENDA SONGEA ??? KWA VIWANDA NA UZALISHAJI GANI ULIOPO SONGEA.

ANYWAY, WATU WAACHE KU-GOOGLE MAMBO NA NADHANI HAYA MAMBO YAMEKAA KIUAALAMU ZAIDI HIVYO TUWAACHIE WENYEWE. TUWE NA KIPIMO KWENYE KUKOSOA.
Sipingi ununuzi wake tena NAPONGEZA SANA, ila najiuliza mtu aliyemdanganya Mkuu wa Kaya kwa kumpa takwimu za uongo za ulaji mafuta.
 
Awali ya yote nichukue fursa hii kumpongeza Mkuu wa Kaya yetu kwa moyo wake wa kizalendo wa kutuletea ndege mbili mpya ili kufufua shirika letu ambalo wenzie walilitafuna na kulifilisi. Japo haohao ndio wanaomshangilia kama vile waliofilisi shirika hilo siyo wao.

Mkuu wa Kaya umedanganywa kuhusu gharama za usafiri wa ndege Dar to Songea. Amesema kuwa ndege za kawaida zinaweza kutumia mafuta ya milioni 28 kutoka Dar to Songea lakini ndege mpya za Bombadier Q400 zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Mimi sio mtaalamu wa ndege lakini taarifa imenifanya kufanya utafiti kidogo

Katika kajiutafiti kangu nimegundua kiwango cha mafuta ya ndege kwa safari hakipo constant. Kinatofautiana kutokana na sababu anuai, kama vile aina ya ndege, umbali wa safari, uzito wa mzigo wa kwenye cabin, kimo kutoka usawa wa bahari, namna ya kupaa. Vyote hivi huchangia utofauti wa utumiaji wa mafuta ktk ndege.

Katika hayo tuchukue moja la aina ya ndege na hayo mengi yawe constant (under ceteris peribus). Mkuu wa Kaya amesema "ndege nyingine" zitatumia mafuta ya mil.28 kutoka Dar kwenda Songea, lakini Bombadier zetu zitatumia mafuta ya milioni 1 tu. Tuchukulie mfano wa ndege aina ya Boeing 777 yenye uwezo wa kubeba abiria hadi 450 (mara 6 zaidi ya Bombadier zetu).
Umbali wa Dar to Songea kwa barabara ni maili 655 sawa na kilomita 1,054. Lakini kwa anga ni maili 364 sawa na kilomita 585. Boeing 777 inauwezo wa kukimbia kwa speed ya maili 590 kwa saa, sawa na kilomita 949 kwa saa. Kwahiyo ikisafiri kutoka Dar to Songea (kilomita 585) itatumia mwendo wa dakika 36 tu.
www.distancecalculator.net

Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
www.askcaptainlim.com

Galoni moja ya mafuta (US liquid gallon) ina lita 3.7 za ujazo. Kwahiyo galoni 1,036 ni sawa na lita 3,836. Bei ya mafuta ya ndege (jet fuel) katika soko la Marekani ni dola 1.38 kwa galoni moja kwa bei ya September 1 mwaka huu. Kwa Tanzania sijui bei ni kiasi gani, lakini tukadirie ni mara mbili ya bei ya Marekani, yani dola 2.76 kwa galoni moja ya lita 3.7.
www.flightdeckfriend.com

Kwahiyo tukitaka kujua gharama za mafuta ya Boeing 777 kutoka Dar kwenda Songea tunachukua galoni 1,036 mara dola 2.76, mara bei ya dola kwa leo ambayo ni TZS 2,182/=. Utapata Shilingi 6,239,123/=. Hii ndio gharama halisi ya mafuta ambayo Boeing 777 itatumia kutoka Dar to Songea.

Maana yake ni kwamba Boeing 777 itatumia mafuta ya milioni 6.2 kupeleka abiria 450 Songea kutokea Dar.

Sasa twende kwenye Bombadier zetu ambazo Mkuu wa Kaya amesema zinatumia mafuta ya milioni 1 tu kwa safari ya Dar - Songea. Bombadier Q400 inatumia mafuta ya milioni 1 kusafirisha abiria 75 tu kutoka Dar to Songea.
Kwahiyo kama kuna abiria 450 wa kwenda Songea, ndege ya Boeing 777 itawabeba wote na itakwenda mara moja tu kwa mafuta ya milioni 6. Lakini Bombadier itabidi iende trip 6 ndipo iweze kuwamaliza. Yani iende kwa mafuta ya milioni 1, irudi kwa mafuta ya milioni 1 (round ya kwanza), iende tena kwa mafuta ya milioni 1 na kurudi kwa mafuta ya milioni moja (round ya pili). Hadi round zote 6 ziishe Bombadier yetu itakua imetumia mafuta ya milioni 12.
Maana yake ni kwamba Bombadier itaenda round 6 na itatumia mafuta ya milioni 12, kubeba abiria walewale ambao wangebebwa na Boeing 777 mara moja tu na kwa gharama ya mafuta ya milioni 6 tu.

NAOMBA NIONGEZEE FACT NYINGINE KUONYESHA KUWA MKUU WA KAYA ALIDANGANYWA.

Kwa kutumia yale makadirio
1 US Gallon = 3.7 Lita

Dhamani ya Dola ni Tshs 2,182

Kwahiyo,
Kama 3.7 Lita = 2.76 US Dolla
1 Lita = 0.8 US Dolla

Kumbuka Bombadier Q400 inatumia Lita 7 @ Maili

Dar to Songea ni 364 Maili

Angalia hapa:

LITA 7 × 364 MAILI × 0.8 DOLA @ LITA × 2182 TSH (Thamani ya Shilingi @ Dola) = 4,447,788.8 TSHS

KWAHIYO;
GHARAMA YA NDEGE TULIYONUNUA KUSAFIRISHA ABIRIA 75 KUTOKA DAR - SONGEA KWA SAFARI MOJA TU NI 4,447,788.8 TSHS.

Nani alimuambia Mkuu wa Kaya ni 1,000,000 TSHS?


ALIYEMDANGANYA MKUU WA KAYA AADHIBIWE....

NAIPENDA TANZANIA NAWACHUKIA WAPIGA DILI.
Uko vizuri
 
fanyeni kazi,kazi kudukua magufuli kaongea nini mpate pa kusemea
Ifike wakati watu tukubali mtizamo tofauti, huwezi danganywa alafu bas ubaki kukubali, mwanadamu anatakiwa kureson Kwa kila kitu maana hata kureson ni Kazi pia, usiye reason we ndo ufanyi kazi
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Point
 
Hata kenya waliosonga mbele kwa safari za anga, safari za ndani hawana uwezo wa kusafirisha watu hata 300. Idadi ni kubwa hiyo, labda kama kuna monopoly ya kufa mtu na safari ziwe kwa intervals
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Msingi ni kuwa Rais anedanganywa........... na hawataacha kumdanganya kwa sababu skiambiwa ukweli ni mbishi!
 
Hadi kufika 12M Q400 itakuwa imerudi ilipotokea (Mf: Dar) na hiyo Boeing 777 IKIRUDI (Return trip) itatumia tena 6M sawa na 12M...!
 
Back
Top Bottom