Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Kuna kipindi JF inakuwa kweli nyumba ya wataalamu na wanaotumia akili na elimu yao. Bandiko hili linawakilisha vyema uwapo wa great thinkers.

Niongeze tu kwa kusema calculations zilizotolewa hapo juu zina assume kwamba abiria hawajali uharaka wa safari ambao uko tofauti kati ya Bombardier na Boeing. Assumptions hii ikilegezwa utaona rais kadanganywa zaidi. Pia hesabu hizo zina assume kwamba gharama ya uendeshaji ndege ni mafuta tu, assumption hii nayo ikilegezwa utakubaliana nami kwamba aliyemdanganya rais hatakiwi kubaki huru mtaani achia mbali kubaki kazini. Kadhalika aliyempa rais hesabu za darasa la saba anadhani kwamba Tz ina abiria infinity ambao wanakiu ya kupanda kwenda kila mkoa Tz may be angefanya research angegundua kwamba ipo mikoa mingine hata mabasi hayaendi maana hakuna shughuli za kibiashara. Angelijuwa hili labda ununuzi wa ndege usingekuwa priority kwa sasa.

Nashangaa kwanini aliyemdanganya rais hajatumbuliwa kwa jambia au shoka!
Na wewe ni great thinker.. Na umeona hiyo ni hoja ya ki great thinker? Aibu hii
 
Mafuta ya ndege hupimwa kwa galoni (US Liquid gallon) ambapo galoni moja ni sawa na lita 3.7 za ujazo. Boeing 777 inatumia galoni 14.4 za mafuta kwa injini moja kwa dakika (1 lg/engine/minute). Boeing 777 ina injini mbili za "Rolls Royce trent 892" zinazotumia galoni 28.8 za mafuta kwa dakika moja (ingia hapa ). Hivyo basi kwa dakika 36 itakazotumia kutoka Dar to Songea itatumia galoni 1,036.
Mkuu nadhani msingi wa hoja yako uko hapo. Kwa maelezo yako Boeng 777 inatumia galon 28.8 kwa dakika. Chanzo chako ni website inaitwa askthecaptain! Siezi kwenda mbali kusema raisi amedanganywa katika jambo ambalo liko very techical halafu hicho ndio chanzo changu cha habari.

Na mimi pia sio mtaalam kama wewe ila simple search imeonesha kuwa Boeng 777 inatumia galon 1 kwa sekunde, inafanya galon 60 kwa dakika. Lakini siwezi kusema mimi niko sawa zaidi ya wewe, sababu sote tunatoa katika vyanzo ambavyo havina uhusiano wowote na Boeng wala havitoi guarantee kuwa information wanazo published ni verified information. Kuishutumu taasisi ya uraisi sio jambo la mzaha mzaha.

Naomba nisaidie kama unayo hiyo reference, mkuu wa kaya alivyosema hiyo Milion 28 na hiyo milioni moja alitoa mchanganua wake? Nimejaribu kufanya marejeo sijapata sehemu nzuri ya UHAKIKA.

Angalizo langu kwako, si kila taarifa inayopatika baada ya kugoogle ni taarifa sahihi. Ukitaka habari za uhakika za Boeng nenda kwenye tovuti ya Boeng. Ukitaka habari za uhakika za Bomberdier nenda kwenye tovuti yao. Mimi binafsi sijaona umuhimu wa kufanya hivyo sababu sijapata sababu ya kutilia wasiwasi kilichosemwa, namba zilizosemwa kama ni sahihi au la, nakubaliana na uamuzi wa kununua ndge ndogo kwa safari za ndani.
 
Acha kujifanya kama zmekruka kichwani, usiangalie typing error ndo uconclude , soma the meaning of thread ndg yangu,
Ukijifanya mjuaji ujiandae kikamilifu, hakuna typing error hapo zaid ya kutojua , umeandika Boeing hiyo Airbus imekujaje hapo mbele? tofauti yako na hao unaowaita nyumbu ni kuwa wewe ni nyumbu wa mwendokasi huoni mashimo
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Na pia je kuna huo uwanja wa kuweza kuhimili ndege kubwa hivyo????
 
Huyu jamaa nadhani alikulia Masaki akaenda US akiwa mdogo so hajui hata geography ya Tz zaidi ya kile alisomaga St Marys
 
Fuel Cost Winner: Bombardier
This Bombardier costs $5.65 less per nautical mile to operate than the Boeing.
Relative to Class Averages:
Turbofan-powered Narrow-body Commercial Passenger Plane: $13.07 per nautical mile
737-800: +$0.1672727273
Turboprop-powered Narrow-body Commercial Passenger Plane: $7.26 per nautical mile
Q400: +$0.335

Bombardier ni cheaper sana kui run, tumuunge mkono mh. Rais
 
Yaani hivi videge vinavyosifiwa kama dunia nzima ndio ndege bora..ngoja zianze safari ndio tutajua udhaifu wake
 
Shida ya mkuu wa kaya anafanya maamuzi ya kibabe pasipo kufanya utafiti kwa kujipa muda. Bt hasara kwake
 
Mleta mada alichofanya ni FACT CHECKING TU, na imeonekana kuwa ni kweli mkuu wa kaya kadanganywa akakurupuka na mafuta ya milioni 28 vs mafuta ya milioni moja. Wadanganyika tujenge utamaduni wa kufanya fact checkings ili tusiwe tunadanganywa kipumbavu. Hakuna ndege inayoenda Dar Songea kwa mafuta ya milioni 28 hata iwe ndege kubwa kuliko zote ya abiria. Mkuu wa kaya ulikurupuka na kudanganya wananchi wako
 
mleta mada anajichizisha mkuu! kwenye andiko lake kaweka kanuni za kufuata wakati wa kufafanua kabla hajafika katikati ya maelezo tayari alishazivunja!
Ile ya mwanzo nilipoandika watu wakahitaji comparison. Sasa nimeweka uwiano kati ya hizo ndege mbili. Ukisoma vizuri utanielewa. Soma tena uelewe mantiki yangu.
 
Na pia je kuna huo uwanja wa kuweza kuhimili ndege kubwa hivyo????
Ukisoma mada yangu utaelewa sababu ya mimi kuandika huu uzi. Soma tena utajua lengo mahsusi la uzi huu.
 
Huyu jamaa nadhani alikulia Masaki akaenda US akiwa mdogo so hajui hata geography ya Tz zaidi ya kile alisomaga St Marys
Hapana, nimekulia kijijini na nimesoma Tanzania.
Soma vizuri na utagundua kitu.
 
Fuel Cost Winner: Bombardier
This Bombardier costs $5.65 less per nautical mile to operate than the Boeing.
Relative to Class Averages:
Turbofan-powered Narrow-body Commercial Passenger Plane: $13.07 per nautical mile
737-800: +$0.1672727273
Turboprop-powered Narrow-body Commercial Passenger Plane: $7.26 per nautical mile
Q400: +$0.335

Bombardier ni cheaper sana kui run, tumuunge mkono mh. Rais
I think you didn't read well the topic. Am with you, but I am against the wrong information given.

Read it again then you will understand what do I mean.
 
Mleta mada alichofanya ni FACT CHECKING TU, na imeonekana kuwa ni kweli mkuu wa kaya kadanganywa akakurupuka na mafuta ya milioni 28 vs mafuta ya milioni moja. Wadanganyika tujenge utamaduni wa kufanya fact checkings ili tusiwe tunadanganywa kipumbavu. Hakuna ndege inayoenda Dar Songea kwa mafuta ya milioni 28 hata iwe ndege kubwa kuliko zote ya abiria. Mkuu wa kaya ulikurupuka na kudanganya wananchi wako
Asante sana tena sana kwa kunielewa vizuri kabisa.
 
Hao abiria 400+ wanaokwenda Songea ni kina nani? Tumia akili hii nyepesi: Why send a nearly empty Boeing to Songea when a Bombardier could fit the purpose? Tatizo lenu sio ndege, ingekuwa kubwa mngeponda, sasa ni ndogo mnaponda. Mbona hamzungumzii mabehewa mapya ya kuifufua Reli ya Kati? Acheni siasa za chuki
Hujamwelewa mtoa hoja hapingi serkali kununua bombardier.hoja yake imejikita kwenye gharama za mafuta ya bombardier kutoka dar to songea sio milioni moja kama rais alivyoambiwa ,mtoa hoja anasema achukuliwe hatua aliyemdanganya rais kwa sababu gharama za mafuta ya bombardier dar to songea ni zaidi ya milioni moja
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Maneno yako ya kweli lakini mleta hoja kasema kile walichosema wao sababu kuu kununua hii ndege ni ulaji wa mafuta ila kama angesema kuwa pia sisi hatuna viwanja vikubwa mikoani vya kupokea ndege kubwa au soko sio kubwa kiasi cha kununua ndege kubwa hilo linaeleweka kabisa lakini wao walichosema ni mafuta tu kwa hiyo mleta hoja ana haki ya kuuliza swali la msingi. Tz viwanja bado na maana ya viwanja sio tu majengo pia kila ukileta ndege kubwa lazima uwe na vitendea kazi vinavyoweza kumudu ndege kubwa kama fire trucks na uwepo wa mafuta ya kutosha. mimi nakubaliana hata hiyo ndege ya watu 75 si ajabu wasijaze.
 
Back
Top Bottom