Nani ambaye hujampigia simu kitambo ungependa kumpigia leo?

NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,423
2,414
Salaam/Shalom.

Natumai mu-wazima kabisa, kama mimi vile nilivyo pia.

Lakini huwezi kujua mtu ambaye hamjawasiliana muda mrefu sahizi anaendeleaje...? Watu wangapi hujawasiliana nao kwa kipindi kirefu sana? Je, wapo Hai au Wamekufa....? Wazima au Wanaumwa...?

Siwezi kusema kuwa INAUMIZA SANA kuona mtu anawasiliana na WATU BAKI lakini WATU WAKE WA KARIBU hata salaam hawajulii. Hata mimi hili huwa linanitokea pia.

Sio kwamba eti huwa nakosa salio la kuwapigia HAPANA...! Ila inawiwa vigumu kupoteza salio kwa ndugu ambaye ni SNITCH...! Nimeskia watu wengi tu wakisema "NI HERI YA RAFIKI KULIKO NDUGU". Sasa ndugu wa aina hii ambaye hata hakutakii MEMA hata kumsalimia muda mwengine inakuwiwa vigumu sana. Lakini pia kusahau mpaka unajikuta salio ulilojiunga linaisha hata bila ya kuwapigia watu wako wa karibu...?

Kuna watu wangu wengi tu wa KARIBU na MUHIMU nakuwa sijawasiliana nao muda mrefu sana, ila kuna siku natenga muda nawapigia wote ambao sijawasiliana nao hata mwaka mmoja au miezi kadhaa nyuma, WANA-APPRECIATE SANA.

Wewe unamkumbuka nani ambaye hujampigia muda mrefu ungependa kumpigia LEO au KESHO...?

SALAAM/SHALOM...!
 
Aisee unaweza kuwa na kifurushi mpaka kinaisha you don't care 'bout them, kiukweli ni wengi unajikuta hujawapigia sijui kwa kuwa wao nao pia hawajakupigia?

Hata sijui sababu ni nini aisee.
Inaweza kuwa ni kujisahau au labda mwengine utakuwa hamkuachana vizuri...!
 
Kiukweli nilikuwa napenda sana kuwapigia sana na kuwajulia hali ndugu lakini badala yake ikawa kama kila nikiwapigia nakuwa kwenye interview maana ni full kuniuliza kuhusu maisha yangu na mwisho ndiyo nikawa najikuta natengeneza kundi la omba omba wakati mimi bado nahitaji kusimama imara zaidi ya leo

Finally sasa nimeacha kuwapigia simu nipo tu anayepiga leo nitampigia juma lijalo ila baada ya hapo asahau kuhusu simu yangu .

Toka nimeamua kufanya hivyo naishi kwa amani sana na furaha nimenenepa sana , nilienda jela ndugu hawakujua na nimetoka na bado hawakujua yaani raha tupu , nimeishi kwa raha jela kama hakuna liliyotokea maana hakuna mtu ninayewaza atakuwa anaumia kuhusu mimi .

Ndugu wazuri kuwa ndugu yao ila wabaya kuwa karibu nao .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Aisee pole sana kiongozi, kikawaida binadamu baadhi yao wapo hivyo ukijiweka nao karibu sana inakuwa unaongeza shida nyingi kwa upande wako, watakujazia matatizo yao lukuki kiasi kwamba mpaka unajutia.

Kuna jamaa ilikuwa akipigiwa simu na ndugu zake swali lao kubwa utaskia "UNAOA LINI ETI...?" basi huwa anakereka sana, ikampelekea kutopokea simu zao na hata yeye mwenyewe hawapigii tena siku hizi labda itokee dharura kubwa.
 
Back
Top Bottom