Hujajibu swali langu. Hata kama sijaelewa, kutonijibu jwako hakunieleweshi.
Intellectual knowledge ni nini na sensual knowledge ni nini na unazitofautushaje?
Hujajibu swali hili.
Unajinasibu kama unaelewa. Ndivyo unavyojibainisha kwa wafuasi wako humu!
Kwa mtu anayejibainisha hivi anashindwaje kujua intellectual knowledge ni nini na sense knowledge ni nini. Inasikitisha!
Niseme kidogo kuhusu sense knowledge.
Nafahamu unafahamu mfumo wa fahamu wa mtu.
Hapa nazungumzia milango mitano ya fahamu yaani macho, masikio, ulimi, ngozi na pua, na mlango wa kati wa fahamu yaani ugwemgongo, uti wa mgongo na ubongo.
Hii milango miwili ndiyo inayohusika na kupokea, kuchakata, kupeleka na kutafsiri jambo au taarifa zinazoendelea nje na ndani ya mwili. Hii ni kadiri ya baiolojia
Hivyo, hii milango miwili yaani milango mitano ya fahamu (sense organs) na mlango wa kati wa fahamu wa mtu (human central nervous system) ndiyo inahusika na ufahamu.
Nitaeleza kuhusu ufahamu, ikibidi.
Kwa mfano, mlango wa fahamu wa sikio ni kiungo (organ) inayopokea, chakata na kupeleka taarifa au jambo. Vivyo hivyo kwa milango yote ni viuongo kamilifu kadiri ya kazi yake.
Ndiyo katika utaratibu huu (picha ndogo tu ambayo nimeieleza) wa milango ya fahamu yaani milango mitano ya fahamu na mlango wa kati wa fahamu wa mtu hufafanuliwa kama sense knowledge.