Kabla sijaenda mbali zaidi,tuanzie hapa "Does infinity exist ?".
Ukijibu kuwa ina exist itabidi uniambie iko wapi na umejuaje,kisha utajua kama na "avoid infinite regression" au naandiks uhalisia.
Hakuna non believer anae weza kuja na hoja hiyo, sababu historia ya nadharia hii inajulikana,yule aliyekuja na nadharia hiyo ameikuta tayari dunia ipo na akili ya kawaida haikubali,kwamba mshindo mkubwa uliotokana na kutanuka kwa dunia,na ukiangalia kwa undani nadharia hii inaonyesha ulazima wa kuwepo kwa muumba,rejea kitabu cha Stephen Hawking "A Brief History of Time"
Anasema Hawking :
“This means that the very beginning of the universe was chosen with great care, if the theory of the hot Big Bang was correct from the beginning of time. It is very difficult to explain why the universe began in this particular way, unless we say concerning that that there was indeed a Creator who wanted to create beings like ourselves” [A Brief History of Time, Hawking, p. 127].
Naona unatumia udhaifu kukosoa uhalisia yaani unatumia matokeo ya "logic" katika "Fallacy of special pleading", kwanza onyesha usahihi wa fallacy kisha ukosoe hoja yangu.
Tofauti ipo kubwa sana,sababu Qur'aan si zao la mwanadamu,Qur'aan ni ukweli mtupu na uhalisia,kuilinganisha Qur'aan na vitabu vingine kunaonyesha wazi ya kuwa huijui Qur'aan.
Ili uone ya kuwa Qur'aan ni ukweli mtupu,nakuwekea aya inayo uliza swali kisha ujibu swali hilo.
Anasema Allah aliye juu :
35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
Stay with me.....
Tu focus kwenye hoja yako uliyoileta hapa
Umesema kuwa kuuliza nani aliyemuumba Mungu (Who created God) ni swali LA kipumbavu kwasababu Mungu hakuumbwa
Mungu ni kitu(something) kwasababu kwa mujibu wa hoja yako ana exist (yupo)
Kwa kubali kuwa Mungu yupo na hakuumbwa ni sawa na kukubali kuwa kitu(something) kinaweza kuwepo (exist) bila kuumbwa (created)
Na hapo hujatupa sababu yoyote kwanini Mungu anaweza tu kuwepo(exist) bila kuumbwa au kuwa na chanzo(cause) pia hujatwambia kivipi inawezekana(how) kitu kikawepo bila kuumbwa au kuwa na chanzo (cause)
Kusema tuu bila hoja,sababu,au mechanism kuwa Mungu yupo bila kuumbwa kunafanya maneno yako kuwa tupu
Na Mimi nikisema kuwa "Ulimwenguu huu" upo tu bila kuumbwa au kuwa na chanzo,utakataa vipi hoja yangu wakati hata wewe umeitumia kwenye case ya Mungu?
Ukisema Ulimwengu lazima uwe na chanzo (cause) lakini Mungu hatakiwi kuwa na chanzo(uncaused) bila kutwambia why & how utakua ume commit fallacy ya special pleading
Pia kuna Mamiliion ya Miungu inayoaminiwa na dini nyingi Duniani,Ni Mungu yupi Huyo unayomzungumzia?
Vishnu?, Krishna, Zeus?,Allah?,Jehovah?,Ra?
Neno "Mungu" ni sawa na neno "Nchi" au "ugonjwa", they are generic
Usiseme naumwa ugonjwa,sema naumwa malaria ili watu wakuelewe
Na ukisema Mungu unayemzungumzia ni " Allah" wa Quran lazima utupe reason kwanini ni yeye na sio Vishnu,Thor, Zeus,Jehovah, au Krishna?
Pia Ku "quote" Quran Ku validate hoja yako ni upuuzi wa kiwango cha juu ambao haufai kwenye mijadala ya namna hii,kwa sababu hata mu Hindu anaweza Ku "quote" Bhagavad Gita Ku prove uwepo wa Mungu Vishnu
Na mu Hindu,kwake kitabu cha Gita ni kitabu kitakatifu kama wewe unavyoiona Quran
Hapa utagundua kuwa,una prefer Quran kama kitabu sahihi kwa sababu kuna 98% chance umezaliwa kwenye familia ya kiislam,sawa na mkristo anayeamini kuwa bibilia ni 100% maneno ya Mungu kwasababu amekulia na kulelewa katika familia au mazingira ya kikristo,ungezaliwa India possibly ungekuwa Muhindu,Jamaica ungekua Rastafarian au China ya miaka ile ungekua Confucian au Buddhist
Kitabu kipi cha dini unakiamini,inategemea umezaliwa wapi na link
Sasa acha ujuha wako tena wa Ku quote Quran
Jenga hoja,jenga fact
Nambie kwanini Mungu asiwe na cause lakini Ulimwengu uwe na cause
Pia unambie how is it possible kitu kuwepo bila kuwa na cause au beginning?