Nani alituloga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani alituloga!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by utiyansanga, Dec 14, 2010.

 1. u

  utiyansanga JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna watu amboa wameshindwa kujiendeleza kama jumuia ni Watanzania!,Pamoja na rasilimali nyingi bado nchi yetu na maskini ,mijadala mingi inayoendelea hapa nchini ni kujadili watu.Kila siku linaibuka jipya.Kama tungekuwa na angalau %50 ya ufahamu tusingekuwa hapa.Mimi sio mchumi (wachumi n) watanikosa nikipotoka!
  Nitatolea mfano wa kilimo cha alizeti na matunda hapa nchini. Kwa wasio fahamu alizeti ni zao ambalo uzalishaji wake gharama yake ni ndogo sana !Katika maeneo mengi (ninayo ya jua )kama DODOMA,SINGIDA,MBULU ,KATESH AU KARATU huhitaji dawa kupata mazao bora ya alizeti.Ukilinganisha gharama za uzalishaji na bei,na mahitaji ya soko ,alizeti inaweza kuwakomboa wakuliam wengi wa Tanzania.Na iwapo serikali itapandisha kodi ya mafuta yanayotoka nje itaweza kuinu kilimo na na viwanda vya alizeti ,...itapanua ajira!
  Njia rahisi ni kupandisha kodi ya mafuta ya nje ,na kuhamasisha watu athari ya ulaji wa mafuta yenye lehemu.Watalamu wa afya wamebainisha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yameanza kuchukua nafasi kama kisababishi kiongozi cha vifo ,na sababu mojawapo ni ulaji mbovu ukiwemo wa mafuta hayo.
  Tunashindwa nini kutumia sababu hii ya kiafya kujiongezea kipato na ajira!
  Leo hii kijijni kwangi lt 20 za alizeti ni 50,000/=!ukileta mjini je
  Kama vile haitoshi mashudu ya alizeti ni chakula bore acaha kuku na .........,what a multiple advantage
  Kama tunaibiwa kwenye madini hata hili latushinda
  Kuhusu matunda pita bara2ni Dar es Salaam hazina ya matunda yanavyooza kwenye nchi ya Wdanganyika wanaojadili siasa kila kukicha bila kuchukua hatua!
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umewahi kumuona mchawi kwa macho yako akiloga ili fulani asiendelee? je DRC nao wamelogwa? Nchi ya nne kwa utajiri wa mali asili duniani! angalia hali ya hiyo nchi! Waafrika akili zetu ndo zimefikia hapo ndugu yangu!
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Unajua sisi wabongo tumeiga sana tabia za waswahili wa pwani. Hatuko siriaz. Maneno mengi mazuri lakini yaliyo tupu. hakuna vitendo. Tunapiga siasa mno kuliko kutekeleza mipango ya maendeleo. Uswahili mwingi uliochanganyikana na ulaghai, ujanja-ujanja wa kutaka kuzidiana kete na kutajirika kwa muda mfupi, nk.
   
 4. u

  utiyansanga JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni akili zetu,basi hao wanaosema Waafrika waliumbwa na akili duni.....lakini mbona NCHI NYINGINE WANANAFUU,hebu angalia Rwanda,Botswana na hata KENYA ANGALAU WANAJITAHIDI ,Mimimsihani kama ni maumbile kuna kitu kimetufikisha hapa!
   
 5. u

  utiyansanga JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli !tabia za watu wapwani ....kwani mbongo ni nani,unapozungumzia watu wa pwani unazungumzia kuanzia Mtwara hadi TANGA ....Zanzibar .....inakuwaje mjanja aige tabia za kiswahili inawezekna basi Wbongo9=(WASIO WA PWANI ) ni mazuzu zaidi(wameiga) kuliko wa pwani
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hatujarogwa wala nini, ni ujinga wetu wenyewe!
   
 7. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sisi watanzania ni wajinga na tutaendelea kuwa wajinga hadi pale kila mtanzania atakapojitambua kuwa ni mjinga na kuamua kutokuwa mjinga.

  Sisi ni Punda na tutaendelea kuwa Punda
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  bado tuna ka ujamaa ndani ya mioyo yetu - ujamaa ndugu ni kama dini. kibaya zaidi viongozi tunaowachagua badala ya kutuwezeshe hata ki fikra sasa wao ndiyo wa kwanza wanajilimbilizia mali na kusign mikataba isiyo na maslahi kwa taifa.

  Bado sina imani kwamba watanzania tu wajinga hapana, ila mfumo wa siasa yetu tangu uhuru ndio umetufikisha hapa tulipo. hatujajua kwamba ujamaa ushakufa kitambo na sasa mfumo ubepari ndiyo unatawala uchumi wa dunia hii.

  Kinachotakiwa mjadala wa kitaifa uandaliwe ili kubadili mawazo yetu kwamba ujamaa ushaisha na sasa kuanzia kaya, mtaa, kata, jimbo lazima kujitafutia maendeleo wenyewe tukisaidiwa na serikali kutuwekea mazingira mazuri ya kujitegemea na kukuza mitaji yetu.


  Kwa mfano wakenya wanajua umuhimu wa ardhi sasa ngoja tuingie kwenye shirikisho uone watakavyokuja kuchukua ardhi ya kilimo then sisi tuwafanyie kazi kwenye mashamba yao. Watafanya hivyo sababu wana Mitaji mikubwa.
   
Loading...