Nani alipona tatizo la kuota unafanya mapenzi ndotoni?

Point of No Return 19

Senior Member
Jul 2, 2023
194
455
Hizi za Aina hii zinanitesa Sana Mimi?

Nifanye Nini ili ziweze kuniachia,

Mara kadhaa kwa miaka kadhaa Sasa nasumbuliwa na hizi ndoto za kufanya mapenzi usingizini

Mimi siangalii video za porn

Mimi siongelei Mambo ya ngono

Ila nashindwa kuelewa hii Hali naichukia Sana ,nifanye Nini jamani?
 
Kwa mwanaume ndoto nyevu ni sehemu ya maisha hasa kwa mabachelor lazima kiwango fulani cha mbegu kipunguzwe ili kuweka mizani sawaa

Ila ndoto nyevu zikizidi hapo kuna shida mfano unapata ndoto nyevu siku tatu mfululizo...

Kama unadhani kuna ushirikina Jaribu kutumia chumvi ya mawe chukua kiasi kidogo weka chini ya mto...

Mshana Jr tunaomba uchangie hili
 
Kwa nini mnazilalamikia ndoto nzuri kama hizo!! Tena yule mwingine alisema amekuwa akiota hizo ndoto na wanawake anao wafahamu! Raha iliyoje hii!!
 
Back
Top Bottom