Nani alimwambia Rais Samia asikutane na CHADEMA?

Nani alimwambia Rais Samia asikutane na CHADEMA?

RAIS Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake ya leo amesema aliambiwa asikutane na Chadema kusaka maridhiano.

Kwa kuwa tumeshaamua kuwa taifa la haki, ukweli na uwazi ni vizuri tuwafahamu hao waliomwambia Rais Samia asikutane na Chadema ili tujue malengo yao yalikuwa ni nini.
NI WALE WENYE KAULI YA WATU WAZURI HAWAFI
 
Hao ni wafadhihina wa CCM, ambao hivi Sasa wamenuna, kusikia kuwa Maridhiano baina ya CCM na wapinzani, yametiki[emoji3]
Kwa hiyo mmeridhiana kwamba akimaliza term yake ni zamu yenu?
 
RAIS Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake ya leo amesema aliambiwa asikutane na Chadema kusaka maridhiano.

Kwa kuwa tumeshaamua kuwa taifa la haki, ukweli na uwazi ni vizuri tuwafahamu hao waliomwambia Rais Samia asikutane na Chadema ili tujue malengo yao yalikuwa ni nini.
Unamjua rostam au ujawai kumsikia
 
NI WALE WENYE KAULI YA WATU WAZURI HAWAFI
Kambarage Dec 11, 2022 aliweka bandiko linasema hivi:
Pia Jakaya alionekana kukosoa uongozi wa Rais Samia kama Mwenyekiti wa CCM kwa kusema kuwa katika kipindi chake Jakaya akiwa Rais na Mwenyekiti wa CCM hakutoa nafasi kwa "upuuzi" wa watu kusema uongo ndani ya chama.

Licha ya kusema kuwa siyo utamaduni kwa Rais anayemaliza muhula mmoja kupingwa na wagombea wengine ndani ya chama, alionya kuwa hilo linaweza kutokea "kama mambo yakiharibika sana."
 
Tatizo sio Maraisi wetu bali tatizo lilikuwepo kwenye vyama vya upinzani na haswa chadema ambacho kiligeuka kuwa chama cha wanaharakati!!! kama haitoshi chadema kilikuwa chama cha kuhamasisha vurugu na chuki dhidi ya serikali!!

chadema ili jenga tabia ya ovyo kabisa kwa wanachama wake, kama vile tabia ya ujeuri ukaidi na kutukana viongozi !!

Endapo mwenyekiti Mbowe atarekebisha hiyo tabia kwa viongozi wenzake bila shaka wanachama pia watarekebika na hivyo nchi yetu itasonga vizuri zaidi.
Acha porojo, chama "HALISI" kikuu cha upinzani TZ ni CHADEMA peke yake, aminia, ndio chama pekee ambacho viongozi wake hawana "BEI" ni kiongozi yupi wa chama gani ambacho mama kakutana naye IKULU zaidi ya MBOWE? waliobaki wote ana profile zao, BEI zao zinajulikana toka hapo zamani.... tizama kamati zote za kiserikali watateliwa viongozi wa vyama vingine, wapi uliona wakiteuliwa hawa "MIAMBA" Mbowe, Lisu, Leme, Msigwa au Heche? kwanza unaanzaje? hao wengine wote wanajulikana..... hawana hofu nao mwisho wa kunukuu....
 
Nina wasiwasi na ile inayoitwa Familia ya watu wazuri hawafi kina ZZK, Nape, Januari ndio haikutaka maridhiriano na Chadema hongera SSH kwa kufichua hiyo siri
Ikumbukwe pia kuwa uongozi mpya wa nchi awali ulionyesha dhamira kubwa ya kuondoa uhasama wa kisiasa uliokuwa umetamalaki. Baada ya muda wa miezi michache tu dhamira hiyo ilififia sana na badala yake ukaibuka mtazamo na msimamo mkali. Kwa jambo kubwa kama hili linaloweza kuathiri usalama wa nchi na mustakabali wake bila shaka ushauri unaopewa uzito zaidi ni ule wa vyombo vya usalama. Kuna matukio kadhaa yanayoashiria kuwa chanzo kikubwa cha ushauri huu ni vyombo:
1. Kauli ya "chokochoko" ya harakati za katiba mpya.
2. Nguvu kubwa ya polisi iliyotumika kuzuia makongamano ya katiba mpya.
3 Kesi ya ugaidi
4. Marufuku ya vikao vya ndani vya vyama kinyume na ilivyokuwa siku za nyuma.
5. Matumizi ya nguvu kubwa kutoka Polisi dhidi ya wafuasi wa vyama vya upinzani nchi nzima
6. Jitihada kubwa ya kutaka kuendesha kesi ya ugaidi gizani.
7. Mabadiliko katika uongozi wa vyombo vya usalama.
Kwa vyovyote vile ni vyombo ndivyo viliuaminisha uoongozi wa nchi kwanza, kwamba kulikuwa na watu wenye tuhuma za ugaidi na kwamba ushahidi wa kutosha ulikuwepo. Pili, vyombo pia ndivyo viliuaminisha uongozi wa kisiasa kwamba vyombo vyenyewe vilikuwa na uwezo wa kuzima harakati zote za kisiasa za vyama shindani na hivyo hakuna haja ya mazungumzo.
 
Back
Top Bottom