Nani alimshtua Lowassa?

Alipogusia kashfa ya Richmond huko Dodoma na kuahidi kuizungumzia zaidi tarehe 30/5/2015 huko Arusha,Lowassa alishaingia kwenye 'kumi na nane' za Dr. Harrison Mwakyembe, Samwel Sitta na waliokuwa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge. Kimsingi, hata Lucas Seleli angeibuka na kumwanika Lowassa. Lowassa angeumbuka mchana kweupe kwa kuwekwa hadharani hata yale yaliyofichwa Bungeni mwaka 2008.

Huko Arusha Lowassa hakuthubutu kuelezea kuhusu kashfa iliyomng'oa kwenye Uwaziri Mkuu ya Richmond kama alivyoahidi Dodoma. Nini kilimshtua? Nani alimshtua? Lowassa atambue kuwa anaishi kwenye nyumba ya vioo na hivyo asichokoze ugomvi wa mawe.

Wale walioleta ile ishu ndio wanafiki kwa nini walificha mengine?
 
Tatizo la watanzania tunafanya mambo kwa hisia na mihemko.
Hakuna mahali ambapo Lowasa alisema kuwa atazungumzia ishu ya Richmond Arusha.
Richmond Lowasa alishaizungumzia mara nyingi tangu sikua ile alipojiuzulu.
Na aliizungumzia ndani ya kikao cha chama pale alipoona anakashfiwa na kina Nape na kundi lake kwa gharama za chama.
Lowasa tangu siku ile alipojiuzulu aliweka sawa na watanzania wote wasio na maslahi ya kisiasa na kimadaraka wakamuelewa kuwa alionewa na ndio maana watu wanamuunga mkono na makundi mbalimbali.

Alichosema Lowasa ni kuwa mambo mengine yanayohusu vipao mbele vyake asingependa kumaliza uhondo wa kuyazungumzia pale Dodoma badala yake atayazungumzia Arusha.
Sasa watu bado wanaendelea na hilo suala ili tu kuanzisha malumbano ya kimakundi badala ya mijadala ya kuondoa umaskini.
Hata ukiangalia kwa sasa watanzania hawazungumzii masuala ya kumtaja sijui Mwakyembe ,sijui Sita kama agenda wao wanataka waondokane na umaskini.
Umaskini umewatesa sana watu na wengi wanakoeshwa haki zao kwa sababu ya umaskini na kukosa elimu.
Sasa makundi mengine ya kisiasa yanashindwa kujipanga baala yake wanakuja na hadithi za nani ni hasimu wa nani!

Lowasa angekua ni fisadi na Mwakyembe na Samweli Sita wana vielelezo vyote vya kumtia hatiani wasingeendelea na hadithi za kusema kuwa ni fisadi tu huku wakimwomba mwenyezi Mungu ili Lowasa afe ,badala yake wangempeleka mahakamani ili ahukumiwe.

Ni mwanasheria gani asiyejua kuwa chombo cha kutoa hukumu ni mahakama. Iweje wao kama wanasheria na tena mawaziri waendelee kupita kuwema tutatoa vielelezo vyote.
Je,inakuaje wapenda haki wanaficha vielelezo vya wahalifu?
Je,kama ni kweli kama Mwakyembe na Sita watakuwa na vielelezo vya wizi unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma halafu wakaamua kuvificha kwa ajili ya kuvitumia kwa manuafaa yao ya kisiasa kwa nini tuendelee kuwaamini hawa watu wanafiki na wabinafsi?

Kuungwa mkono kwa namna yoyote sio jambo jepesi kama watu wanavyotuambia .
Miaka kumi Sita na Mwakyembe wanatumia gharama za serikali na nafasi za uwaziri kujisifia na kuona kila mtu hafai na wao ndio bora lakini bado imekuwa ni vigumu kuingia kwenye mchuano na Lowasa.Pamoja na kuwa Lowasa amewekwa benchi kwa miaka 8 huku kila njama zikitumika kumchafua na kumchonganisha na rais na chama chake lakini bado anaushawishi kwa watanzania kuliko hata hao mawaziri walioko madarakani huku wakishindwa kuwatumikia watanzania kwa vitendo.

100 digits.
Unamsafisha kwa bandiko lako refu au unatuimanisha kuwa yu anafaa sana?




Mimi tatizo langu ni kumpata mtombea mmoja kwa tiketi ya kumchafua mwingine.
Tukiendekeza siasa hizi hatutapata viongozi bora na wenye uthubutu. Ndio maana watanzania tunakua na viongozi wasiokua na uzalendo na waoga na wanafiki.

Hii hali inapelekea mawaziri wengi wakimbilie nje ya nchi kuomba misaada hata ya kujenga vyoo vya shule kwa kuogopa kuwatumia matajiri wa ndani ili tu asije akaambiwa anatafuta madaraka.
Leo hii tunakwenda ulaya kuomba msaada wa kujenga choo cha shule halafu tukishapata pesa hizo tunatatuta mkandarasi kutoka China ili ajenge choo hicho.

Tunataka wanasiasa wanaozungumzia namana ya kuwatumia matajiri wachache wa kitanzania kwanza na rasilimali nyingi tulizo nazo sio kununua magari ya kifahari ya viongozi nali kuinua maisha ya watu ikiwa ni pamoja na viongozi na wananchi wao.
Kwa nini waziri ajiite maskini na serikali maskini wakati matumizi yake ni makubwa na anatembelea gari la serikali lenye thamani ya sh.mil.200.?
Je,huo sio umaskini wa kujitakia?

Kwa nini wasije na hoja za kimaendeleo badala yake wanasubiriana tu kwa kuchafuana na kuendeleza makundi na malumbano yasiyo na lengo la dhati la kuwasaidia wananchi?
 
Ni afadhali ccm ikashindwa kwa kumchagua mtu mwadilifu kuliko kushinnda kwa kumchagua fisadi aliyekataliwa na baba wa taifa hili mtakatifu aliyechukia kushiba kabla ya anaowaongoza hawajashiba. Ccm itawajibika kwa kumteua mungu mtu kuwa amiri jeshi mkuu wa nchi hii
 
Petro E. Mselewa


MAKONGORO NYERERE NA UJASIRI HUU WA NADRA CCM!
Johnson Mbwambo: Toleo la 182 20 Apr 2011
KINACHOJADILIWA kwa sasa, sehemu mbalimbali nchini, si tena kinachoitwa ‘tiba ya ajabu ya Babu wa Loliondo'; bali ni kilichotokea, hivi karibuni, huko Dodoma kinachoitwa ‘kujivua gamba kwa CCM'.
Mitaani, sokoni, kwenye mabaa, vijiweni na hata maofisini kinachozungumzwa sasa na kinachojadiliwa, ni kuhusu yaliyojiri huko Dodoma ambako CCM ‘kilijivua gamba' kwa kuwatosa viongozi wake maarufu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Kote huko maswali kibao yanaibuliwa; Je, ni kweli CCM imefanikiwa kujivua gamba? Je, ni kweli Rais Kikwete kawatosa moja kwa moja maswahiba wake – Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge au ni ‘usanii' wake mwingine? Je, uamuzi wa Dodoma wa kuwataka watuhumiwa hao wajiuzulu nafasi zao za uongozi katika Chama utafuatiwa na hatua za kisheria za vyombo vya kisheria dhidi yao?
Je, CCM sasa kinaweza kujigamba kwamba ni shwari; ilhali aliyeyalea magamba hayo (Kikwete) bado anaendelea kushikilia hatamu za uongozi?

Je, kina Lowassa, Rostam na Chenge wakishajiuzulu nyadhifa zao CCM, kama walivyotakiwa na NEC, watabaki ndani ya chama hicho kama wanachama wa kawaida au wataanzisha chao au watajiunga na vyama vilivyopo vya upinzani?
Haya ni baadhi tu ya maswali mengi yanayoulizwa hivi sasa na wananchi kote nchini wanapojadili matokeo ya kikao hicho cha Dodoma. Ni dhahiri ni maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja ya uhakika, na ni dhahiri ni maswali ambayo ni muda tu ndio utatoa majibu yake. Waingereza wanasema; time will tell.

Vyovyote vile; naandika kumpongeza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, kwa mchangao wake ndani ya vikao hivyo vya CCM ambao ulikuwa ni wa kijasiri, kiungwana, kifalsafa na usio wa kinafiki. Ni mchango ulioweka mbele maslahi ya Taifa kuliko ya kwake binafsi.
Habari za uhakika nilizozipata kutoka kwa waliohudhuria mkutano huo, zinasema kwamba ni yeye pekee aliyekuwa na ujasiri wa kuuanika mbele ya wajumbe udhaifu wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika kuwashughulikia mafisadi ndani ya Chama na ndani ya Serikali.

Ni udhaifu huo wa Kikwete wa kuchelewa kuchukua hatua dhidi yao ambao umekifanya chama hicho kipoteze kwa kasi umaarufu wake kwa CHADEMA. Kwa maneno mengine, kama angelichukua hatua mapema wakati wa awamu yake ya kwanza ya uongozi, pengine mambo ndani ya CCM yasingekuwa shaghalabagala kama yalivyo sasa.


Sitakwenda ndani zaidi kulijadili suala hilo; kwa sababu wachambuzi wengine wamelijadili kwa umahiri mkubwa ndani ya gazeti hili. Isitoshe, kama nilivyoeleza mwanzoni, hoja yangu ya leo ni kupongeza tu ujasiri wa Makongoro Nyerere. Laiti kungekuwa na viongozi wengi jasiri kama yeye ndani ya CCM na ndani ya Serikali…..!
Mtoa habari wetu anasema kwamba wakati wa mkutano huo wa Dodoma, Makongoro alisimama ukumbini na akamtazama, kwa macho makavu, Mwenyekiti Jakaya Kikwete, na kisha maneno yafuatayo yakamtoka kinywani mwake:

"Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule ‘site' wanasema hapana. Atoke. Tena nawe Mwenyekiti ulipokwenda Monduli, ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye (Lowassa), kule ‘site' wakauliza; sasa hii ndiyo nini?"

Rostam simfahamu vizuri. Ninakotembelea yeye hawezi kuja, na mimi anakotembelea siwezi kwenda. Sina ugomvi naye. Lakini kule ‘site' wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema yeye ni kama timu ya mpira iliyokamilika. Watu kwenye ‘site' wakauliza, sasa hii ndiyo nini?"

"Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenti. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye ‘site', si mimi, watu wanasema naye hapana. Ulikwenda pia Rombo, ukamuamsha mkono Mramba, kule kwenye ‘site' watu wakatuuliza; sasa hii ndiyo nini?"

Ndugu zangu, hiyo ni sehemu tu ya mchango mkubwa wa Makongoro Nyerere alioutoa ndani ya vikao hivyo vya CCM vya kujivua gamba, mjini Dodoma. Nina hakika, mpenzi msomaji, utakubaliana nami kwamba Makongoro alionyesha ujasiri mkubwa kwa kumkosoa kiungwana Rais Kikwete ndani ya kikao hicho.

Ni ujasiri ambao ni nadra kuuona siku hizi ndani ya vikao vya juu vya CCM au vya Serikali; kwa maana ya Baraza la Mawaziri. Ni ujasiri mkubwa hasa ukizingatia kwamba wakubwa wetu wengi, hivi sasa, hufurahia kusifiwa tu, na huona raha kuzungukwa na court jesters (waimba sifa na walamba miguu ya wakubwa) ambao hucheka rais anapocheka, hununa rais anaponuna na ambao huwafanya maadui binafsi wa rais kuwa maadui zao pia!

Hawa court jesters hawawezi, kamwe, kumtonya Rais; hata pale inapoonekana dhahiri kwamba anakosea. Ilimradi mambo yao yanakwenda vizuri, watakaa kimya kwa sababu hawataki kumuudhi mkubwa wasijeenguliwa madarakani.

Ndiyo maana anapotokea mtu wa sampuli ya Makongoro Nyerere na kumtazama Rais na Mwenyekiti wa Chama kwa macho makavu, na kisha, kiungwana kabisa na kwa upole kabisa, akamwambia kwamba; "nawe ulikosea", lazima tuupongeze ujasiri wa mtu huyo.

Ninasema hivyo; kwa sababu Rais Kikwete si Mungu au malaika asiyekosea. Rais au Mwenyekiti wa Chama naye pia ni binadamu kama sisi, na hufanya makosa kama sisi, na hivyo ni wajibu wetu kumfahamisha, kiungwana kabisa, pale anapokosea. Ni wajibu wetu kutamka "Mfalme yu uchi" inapotokea kweli "yu uchi".

Ni kwa mantiki hiyo Makongoro Nyerere alisimama na kumwambia ‘Mfalme': "Ulipokwenda Monduli ukainua mkono wake juu (Lowassa) ukasema hujapata kuona kiongozi kama yeye , kule ‘site' wakauliza sasa hii ndiyo nini?"…. ulipokwenda Igunga ukamuamsha (Rostam) mkono ukasema amekamilika kama timu ya mpira; watu kwenye ‘site' wakauliza sasa hii ndio nini?"


Kwa hakika, maneno hayo ya Makongoro yanachoma na kupenya nyoyo. Sina hakika Mwenyekiti Kikwete alijisikiaje wakati Makongoro akiyatamka maneno hayo; lakini nadhani alijutia kitendo kile alichokifanya Rombo, Monduli na Igunga; maana kilimuonyesha mbele ya Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na kwenye mkutano huo, udhaifu wake kama kiongozi.


Kwa mara nyingine tena nimpongeze Makongoro Nyerere kwa kumkosoa Kikwete kipole, kiungwana na kifalsafa. Kwa Watanzania wengine wote ambao hatukuwemo kwenye ukumbi ule, Makongoro alitusemea, alitufikishia hisia zetu kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu.

Makongoro alitumia neno ‘site' (eneo ambako ndiko anakoshinda kusimamia shughuli zake za miradi ya ujenzi) kuwasilisha ujumbe wake, lakini ukweli ni kwamba ‘site' aliyoizungumzia inamaanisha kote nchini. ‘Site' ni sisi sote tulioshangazwa na hatua hiyo ya Kikwete ya kuwakampenia Lowassa, Mramba na Rostam; ilhali wanaandamwa na kashfa nzito za ufisadi.

Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba wakati wa kampeni za mwaka jana za Uchaguzi Mkuu nilipata kuandika, kwenye safu hii, kuhusu kitendo hicho cha Rais Kikwete cha kuwakampenia ubunge watuhumiwa hao wa ufisadi.

Niliandika wakati huo kwamba haingii akilini mwangu (kwa mfano) kwa Kikwete kuusifia utendaji kazi wa Mramba kwenye mkutano wa kampeni Rombo; ilhali Serikali yake anayoiongoza tayari ilishamfikisha mtu huyo mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi, na kesi ilikuwa inanguruma!

Niliandika vilevile kushangazwa kwangu na Rais Kikwete kuwaomba wananchi wa Monduli na Igunga wawape kura za kishindo Lowassa na Rostam; ilhali watu hao wanahusishwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond na Dowans, na hata mmojawao (Lowassa) kulazimika kujiuzulu uwaziri mkuu kwa tuhuma hizo.

Leo, nafarijika kwamba amejitokeza kijasiri Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa (Makongoro), na bila unafiki akamweleza Rais Kikwete (kwa kiungwana kabisa) udhaifu wake aliouonyesha kiuongozi katika suala hilo la mafisadi.

Ni hoja yangu kwamba kama Kikwete angekuwa na washauri makini, bila shaka, wangemweleza mara moja makosa aliyofanya ya kumsifu Mramba hadharani na kumuombea kura kwenye mkutano wa kampeni Rombo na athari zake za baadaye kwa Chama. Nina hakika, pamoja na u-hambiliki wake, angelifikiria mara mbili mbili kabla hajalirejea tena kosa hilo huko Monduli na baadaye Igunga.

Nina hakika vilevile kwamba ni kosa hilo la kuwapigia debe watuhumiwa wa ufisadi wakati wa kampeni, lililochangia kwenye kura chache alizopata kwenye uchaguzi huo ukilinganisha na za mwaka 2005.

Aidha, ni kwa sababu ya kosa hilo hilo watu sasa wanahoji juu ya uwezo wake wa uongozi, na wengi wanajiuliza; kama na yeye si gamba ambalo katika hali ya kawaida lilipaswa nalo kuvuliwa!

Na wananchi wana haki ya kuwa na hisia hizo; maana itakuaje Rais na Mwenyekiti wa CCM (Kikwete) awamwagie sifa kemkem watuhumiwa hao wa ufisadi kwamba ni waadilifu na wachapakazi hodari, na kisha miezi sita baadaye Rais huyo huyo tena aongoze kikao cha chama cha kuwavua uongozi wa CCM watu hao hao kwa tuhuma za ufisadi?!
Kwa nini linapokuja suala la ufisadi tusitilie shaka uwezo wake wa kupima mambo (sense of judgement)? Kiongozi wa nchi anawezaje kuwa na sura mbili katika jambo hilo hilo moja; tena ndani ya kipindi kifupi tu?

Je, tuamini kwamba msimamo wake huu wa sasa (yeye na NEC nzima ya CCM) dhidi ya watuhumiwa hao wa ufisadi, ni wa kudumu na kwamba hataubadili tena huko mbele ya safari?

Je, sasa tuamini kwamba kweli CCM imejivua gamba, na haitawakumbatia tena watuhumiwa wa ufisadi katika ngazi zote? Kama nilivyoeleza mwanzo, haya ni maswali ambayo yatajibiwa na muda tu!
Vyovyote vile; nafarijika kwamba ametokea jasiri (Makongoro) kumweleza hadharani Rais Kikwete udhaifu wake na makosa aliyoyafanya ya kuwakumbatia maswahiba wake hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi; hata kama ni miezi sita imeshapita tangu ayatende, na hata kama tayari yameshaiathiri CCM.

Kwa hakika, mafanikio ya CCM baada ya kujivua gamba, yatategemea mwelekeo wa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete. Sichelei kusema kwamba kama naye hatabadilika (akajivua gamba lake binafsi), CCM itakuwa ile ile ya jana na leo hadi tunaingia uchaguzi mkuu mwingine wa mwaka 2015.

Nihitimishe safu yangu kwa kusema kwamba hata kama kauli zake hizo za Dodoma zitakuja kumponza Makongoro huko mbele ya safari, angalau historia itamtetea kwamba alikuwa na ujasiri wa kutamka: "Mfalme yu uchi" wakati wengine ndani ya ukumbi huo walikwepa kumhusisha na uozo huo wa CCM.

Je; Mheshimiwa Rais kajifunza kitu kutoka katika kosa hilo, na kutoka katika yaliyojiri Dodoma? Ni suala la muda tu tutapata jibu la swali hili.Tafakari.

- See more at: Raia Mwema - Makongoro Nyerere na ujasiri huu wa nadra CCM!
 
Hakuna mwenye nafuu wote tunawadai, Mwakyembe tunamdai hayo aliyoyakalia kuiokoa serikali, Samweli Six kwann alikubali yaletwe baadhi na mengine yaachwe, ila mwisho wa sikuu wakiendelea hv ukweli utafahamika na wote watatu tutawaalani na kizazi chao kwa kutuficha ukweli kwa mda wa miaka 7 na hivyo kuwapa uhalali watawala ambao walikuwa wamepoteza uhalali, kwa ufupi wote ni wasakatonge, ingekua China death penalty ilikuwa halali yao wote watatu!!

Thanks indeed!
 
Katishia nyau na nafikiri ameona upepo ulivyovuma , na kaamua kuingia mitini.

Ile hotuba yake isivyokuwa na mpangilio ndo dalili za kuchanganyikiwa. Waswahili wanasema hata Abson alikuwa Arusha , ujumbe gani kamfikishia haijulikani.

hana public speaking kabisa huyu lowasa. alipagawa na zile kelele za watu
 
Mjadala sasa ni kuhusu nani anayefaa ndani ya ccm.wote waliojitokeza hakuna wa kumbeza.anayembezaLowasa,Mwigulu.Mwandosya au Makongoro ana lake.Hata hivyo naona UKAWA inapotea kwenye rada
 
Waizi hata wakija na maneno matamu kiasi gani,Watanzania tusidanganyike.Mafisadi wengi papa wapo nyuma ya wanaotia nia kigombea Urais
 
Kulingana na shabiki wake anayekwenda kwa jina la Pasco, ni kuwa hakusema kwasababu ameweka akiba ya kujilinda iwapo hatapitishwa na na CCM kugombea urais. Kulingana na Pasco ni kuwa asipopitishwa basi ataweka kila kitu hadharani na atamtaja mhusika

Haya hapa maneno ya Pasco:

Link hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-ndani-ya-ccm-timu-lowassa-nambari-wani.html

asee kwa hiyo huyu jamaa urais ni lazima! hee tutaona mambo,richmond haina mvuto tena ilishaondoka na lowasa kwisha,sasa kipya kipi hata akisema kikwete ndio mhusika,hakuna impact yoyote kwanza mwenzie kashamaliza muda wake,badala yake anajihalibia yeye msaka urais na haupati!

urais kwa lazima ya kupigiwa kura sijawahi kuona,labda afanye kama kagame au museveni atokee msituni na msitu anauweza!? kama zinamshinda ngazi na vikombe vya chai,huyu mtu hayuko normal amechanganyikiwa,hawa wapambe wote ni njaa tu wanapiga pesa zake lakini ukweli wanaujua
 
Watu wanacheza na saikolojia zenu inaitwa "mtupie mbwa mfupa uibe" ndicho kinafanyika plz waiting full movie is loading...............
 
Lowasa ni mzee wa dili lazima ccm impitishe ili kuokoa wenzake wasije kuumbuka ukawa wakichukua nchi'nawashangaa mnaobishana mitandaoni wakat hamfiki hata laki moja wtz zaid ya milion kumi hawajui kutumia mitandao' alafu ndio wapiga kura huko vijijini' kaz ipo
 
Niombe niseme jambo moja siasa zetu zimetawaliwa na chuki na ukanda na hata ukabila wakisirisiri.

Kuna kipindi vijana Wa UVCCM walisema rais hawezi kutoka kazkazini. Aliyesema hivyo hakukemewa kwa ubaguzi, ila aliendelea kuvikwa taji.

Tukijaribu kuona waliyo na baadhi ya watia nia waurais wa CCM, wanaowaunga mkono itashangaa ni watu wa mkoa wake. Mpaka wale wanaoratibu kampeni zao.

Tuyafanye hayo yote, lakini tukae tukijua kwamba nchi hujengwa na walioshikamana pamoja, tena, kwa moyo wa dhati.

Tuepuke siasa mufilisi, uchwara na Maji taka. Tukitumia nguvu nyingi, kuwaminya wanasiasa wengine, na kuwapendelea baadhi, Nina hakika CCM tutapigwa.

Tujitahidi kuwapa Watanzania mahitaji ya moyo yao. Mtu wanayemtaka na kumkubali.

Wengine wanashinda humu JF lakini sina uhakika Kama wamejiandikisha. Tujiandikishe kwenye BVR na tufanye kweli kwenye sanduku la kura.
 
Naamini ana kundi kubwa la magwiji ya siasa za mkakati,hao humuongoza laigwanani katika kila jambo kuelekea uteuzi Wa chama chake,naamini hata hotuba zake huandaliwa kwa umakini mkubwa na huzifanyia mazoezi kabla ya presentation
 
Back
Top Bottom